Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-12-05 19:57:25    
Idara za hifadhi za mazingira kuanzisha harakati za kuchunguza bidhaa zisizo na uchafuzi kwa mazingira

cri

Habari kutoka kituo cha uthibitishaji wa bidhaa za kijani cha idara kuu ya mazingira ya taifa zinasema, kamati ya uthibitishaji wa bidhaa zenye nembo ya hifadhi ya mazingira ya China itashirikisha na idara za viwanda, biashara na ubora wa bidhaa kuanzisha kampeni maalumu ya kuchunguza bidhaa zenye nembo za bandia za hifadhi ya mazingira nchini China, vitendo vya kukiuka sheria za kutumia nembo za bandia za hifadhi ya mazingira katika uzalishaji na uuzaji wa bidhaa, kurekebisha utaratibu wa masoko na kuanzisha mazingira bora ya bidhaa zisizo na uchafuzi kwa mazingira kwa wateja.

China ilijenga utaratibu wa uthibitishaji wa bidhaa zisizo na uchafuzi kwa mazingira miaka 12 iliyopita. Takwimu zilizotolewa na kituo cha uthibitishaji cha mazingira cha idara kuu ya hifadhi ya mazingira zinaonesha, hadi hivi sasa aina 55 za bidhaa zikiwemo za vyombo vya umeme vinavyotumika majumbani mwa watu, zana za ofisini, vyombo vinavyotumika maishani mwa watu na vifaa vya ujenzi, zinafuata utaratibu huo. Sasa aina zaidi ya elfu 21 za bidhaa zinazozalishwa na viwanda zaidi ya elfu 11 zimeidhinishwa kutumia nembo za hifadhi ya mazingira za China, thamani ya bidhaa hizo zilizozalishwa kwa mwaka imefikia Yuan bilioni 90 kwa mwaka.

Baada ya kufanya uchunguzi kituo cha uthibitishaji cha mazingira cha idara kuu ya hifadhi ya mazingira kimegundua kuwa baadhi ya viwanda na wauzaji bidhaa wanapata faida kubwa kwa kubandika nembo za hifadhi ya mazingira kwenye bidhaa zao badala ya kufanya mageuzi ya teknolojia na kufanya bidhaa zao kufikia kiwango cha bidhaa zisizoleta uchafuzi kwa mazingira; kugushi hati ya uthibitishaji wa bidhaa za kijani ya China na kubandika nembo ya hifadhi ya mazingira kwenye pakiti za bidhaa; Na kuchapisha alama za bidhaa za kijani kwenye pakiti za bidhaa au maelezo kuhusu bidhaa.

.Vitendo hivyo vya uwongo vinavyoweza kuwadanganya watu vimevuruga utaratibu wa masoko na kupunguza kiwango cha imani ya watu bidhaa zisizo na uchafuzi kwa mazingira, vilevile vimeua juhudi za viwanda vinavyojitahidi kuendeleza uzalishaji wa bidhaa zisizosababisha uchafuzi. Mkurugenzi wa kituo cha uthibitishaji cha mazingira cha idara kuu ya hifadhi ya mazingira Bw. Chen Yanping alisema, "lengo la China la kufuata utaratibu wa uthibitishaji wa bidhaa za kijani ni kuhusisha uungaji mkono wa wateja kwa hifadhi ya mazingira na ununuzi wa vitu wanavyovihitaji katika maisha ya watu, hatua ambayo inanufaisha uboreshaji wa mazingira ya maisha pamoja na ubora wa maisha ya watu".

Kampeni ya kupiga vita nembo bandia za bidhaa za zisizosababisha uchafuzi kwa mazingira inashirikisha idara za viwanda, biashara na sifa ya bidhaa. Naibu mkurugenzi mkuu wa idara ya kulinda haki za wateja ya idara kuu ya viwanda na biashara, Bw. Lu Yangang alisema sheria ya ubora wa bidhaa inaagiza kuwa, wafanyabiashara hawaruhusiwi kugushi au kutumia nembo za ubora za aina mbalimbali bila ruhusa, wanaogushi au kutumia nembo za ubora bila ruhusa, watanyang'anywa bidhaa na mapato yao haramu, na pia wataweza kuadhibiwa kwa kutozwa faini inayolingana na thamani ya bidhaa zinazotumia nembo za bandia, na wale watakaobainika kufanya makosa makubwa zaidi watanyang'anywa leseni zao. Kuimarisha usimamizi wa ubora wa bidhaa na kutoa adhabu kwa vitendo vinavyokiuka sheria vya kuuza na kutumia nembo za ubora wa bandia.

Kuimarisha usimamizi wa ubora wa bidhaa na kupambana na vitendo vya kukiuka sheria vya kuuza na kutumia nembo za bandia kuhusu sifa ya bidhaa, ni moja kati ya majukumu muhimu ya idara ya usimamizi wa viwanda na biashara, habari zinasema matukio yaliyogunduliwa na kuchukuliwa hatua za kisheria na idara hiyo ya kugushi na kutumia bila ruhusa nembo za ubora wa bidhaa na majina ya viwanda vingine, yalizidi elfu 9 mwaka 2005 yakiwa na thamani ya zaidi ya Yuan milioni 100.

Bw. Lu Yangang alisema idara ya usimamizi wa viwanda na biashara itafuatilia bidhaa hafifu zinazotumia nembo za zisizo na uchafuzi kwa mazingira na kuhakikisha kuwa bidhaa hizo zinatolewa sokoni kwa kufuata sheria; Itaendelea kuboresha mfumo wa kutoa malalamiko kwa wateja unaojulikana kama 12315, kuyashughulikia malalamiko ya wateja kwa haraka; na kuimarisha ushirikiano wa idara mbalimbali ili kuunda nguvu moja kubwa ya usimamizi.

Kituo cha uthibitishaji cha mazingira cha idara kuu ya hifadhi ya mazingira kinawaambia watu kuwa, katika siku za baadaye wakitaka kununua bidhaa zisizo na uchafuzi kwa mazingira wanaweza kutumia mtandao wa ununuzi wa bidhaa wa China.

Idhaa ya Kiswahili 2006-12-05