Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-12-06 19:46:28    
Mapishi ya nyama ya ng'ombe kwa njia ya kienyeji

cri

Mahitaji: Nyama ya ng'ombe gramu 74, sosi ya pilipili hoho gramu 10, figiri gramu 30, pilipili manga gramu 15, chumvi gramu 2, mafuta gramu 10, sukari gramu 5

Njia:

1. kata nyama ya ng'ombe iwe vipande vipande, chemsha maji tia vipande vya nyama ya ng'ombe ili kuondoa damu halafu vipakue. Kata figili iwe vipande.

2. washa moto, tia mafuta kwenye sufuria mpaka yawe na joto la nyuzi ya 30, tia sosi ya pilipili hoho na korogakoroga, halafu mimina maji, tia vipande vya nyama ya ng'ombe, chumvi, sukari pamoja na pilipili manga, halafu korogakoroga, baada ya kuchemka punguza moto kidogo, baada ya nusu ya saa, weka vipande vya figili kwenye sufuria, tia chumvi na endelea kuchemsha, mpaka maji yakauke kasha pakua. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.

Idhaa ya Kiswahili 2006-12-06