Mkutano wa siku mbili wa wakuu wa nchi za Afrika, Caribbean na Pasifiki unafunguliwa tarehe 7 mjini Khartoum, mji mkuu wa Sudan. Viongozi wakuu kutoka nchi 79 za Afrika, Caribbean na Pasifiki wakiwemo marais 16 watahudhuria mkutano huo, mada ya mkutano huo ni ushirikiano kwa ajili ya amani, umoja na maendeleo endelevu.
Kwenye mkutano huo viongozi hao watajadili kwa kina "Makubaliano ya Kiuchumi ya Kiwenzi' yatakayoanza kutekelezwa mwaka 2008, na kujadiliana kuhusu kufutwa kwa vipengele vya fursa maalumu kwa bidhaa za nchi hizo kuingizwa katika soko la Umoja wa Ulaya. Pamoja na hayo, mkutano huo utatafuta ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara nje ya Umoja wa Ulaya ili kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi zinazoendelea, na kati ya nchi zinazoendelea na nchi zilizoendelea.
Kundi la Afrika, Caribbean na Pasfiki, ACP ni jumuyia ya kiuchumi, kundi hilo liliundwa mwezi Juni mwaka 1975 katika mkutano wa mawaziri wa nchi za Afrika, Caribbean na Pasifiki uliofanyika mji wa Georgetown, mji mkuu wa Guyana kwa msingi wa "Mkataba wa Lome" uliosainiwa mwezi Februari mwaka 1975, kwenye mkutano huo "Makubaliano ya Georgetwon" yaliahidi kutimiza lengo la "Mkataba wa Lome", na kuimarisha maingiliano na ushirikiano kati ya nchi wanachama wa kundi hilo na kati ya nchi zinazoendelea katika uchumi, biashara na utamaduni na kusukuma kujenga mfumo mpya wa kiuchumi duniani.
Hivi sasa idadi ya nchi wanachama wa kundi la ACP imeongezeka hadi kufikia 79 kutoka 46, kati ya nchi hizo nchi 48 ni nchi za Afrika za kusini mwa Sahara, nchi 16 za Caribbean na nchi 15 za Pasifiki. "Mkataba wa Lome" unachukuliwa kama ni chombo muhimu cha nchi za ACP kufanya mazungumzo na nchi za Umoja wa Ulaya, na pia ni mkataba muhimu katika ushirikiano kati ya Kaskazini na Kusini. Lakini kwenye "Makubaliano ya Cotonou" ambayo ni nyongeza ya "Mkataba wa Lome" Umoja wa Ulaya ulirekebisha sera zake kuhusu misaada kwa nchi za nje, na marekebisho muhimu ni kuunganisha misaada ya kiuchumi pamoja na siasa, yaani Umoja wa Ulaya unapotoa misaada ya kiuchumi unataka kufanya mazungumzo ya kisiasa na nchi hizo kuhusu migogoro, hali ya haki za biandamu, mchakato wa demokrasia na matatizo ya wakimbizi. Umoja wa Ulaya umetoa hatua za kufuta vipengele vya fursa maalumu za kibiashara kwa nchi ambazo hali yake ya haki za biandamu na ufisadi ni mbaya.
Katika siku ambapo utandawazi wa kiuchumi unaoendelea kwa kina duniani, nchi za ACP zinakabiliwa na jukumu kubwa la kuendeleza uchumi, kukomesha umaskini na maendeleo ya jamii. Kwa hiyo wachambuzi wanaona kuwa katika hali ambapo Umoja wa Ulaya umeunganisha misaada ya kiuchumi pamoja na mambo ya kisiasa, mkutano huo wa wakuu wa nchi za ACP unaofanyika katika mji wa Khartoum ni muhimu sana kwa ajili ya kupatanisha misimamo, kuimarisha mawasiliano, kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uhusiano wa kiuchumi nje ya Umoja wa Ulaya, na kutafuta njia mpya ya kuendeleza ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi za kundi hilo ACP.
Idhaa ya kiswahili 2006-12-07
|