Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-12-11 20:28:37    
Kwa nini rais wa Iraq anaipinga sana taarifa iliyotolewa na "kikundi cha utafiti wa masuala ya Iraq" cha Marekani

cri

Rais Jalal Talabani wa Iraq kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika huko Baghdad tarehe 10 mwezi Desemba, alikosoa taarifa iliyotolewa na "kikundi cha utafiti wa masuala ya Iraq" cha bunge la Marekani akisema, taarifa hiyo si ya haki na usawa, na baadhi ya vifungu vyake vitaathiri vibaya mamlaka na katiba ya Iraq. Vyombo vya habari vinaona kuwa watu wana mashaka na kitendo cha rais Talabani kupinga taarifa hiyo, lakini kuna sababu za yeye kufanya hivyo.

Kitu anachokosoa sana rais Talabani ni kupinga kuathiriwa kwa kanuni ya katiba ya "utaratibu wa shirikisho" wa Iraq kutokana na marekebisho ya sera ya Marekani kuhusu Iraq, rais Talabani anaona kuwa taarifa hiyo imeathiri mamlaka na katiba ya Iraq. Bw. Talabani ni mkurd. Wakurd wanaoishi kwenye sehemu ya kaskazini mwa Iraq walikandamizwa katika kipindi cha utawala wa Saddam Hussein, baada ya vita ya ghuba ya mwaka 1990, nchi washirika zilianzisha sehemu iliyopigwa marufuku ndege kuruka, sehemu hiyo ya wakurd ilikuwa katika hali ya kujiendesha kutokana na ulinzi wa jumuiya ya kimataifa, na iliondokana na udhibiti wa utawala wa Saddam kwa kiwango cha juu. Baada ya vita ya Iraq, mchakato wa kisiasa nchini Iraq ulithibitisha katika katiba kanuni ya utaratibu wa shirikisho na hadhi ya kujiendesha mambo kwa wakurd. Hususan ni kuwa sehemu ya kaskazini mwa Iraq ina mafuta mengi ya asili ya petroli, kujiendesha mambo kwa wakurd kuliwaletea pato kubwa kutokana na mafuta ya asili ya petroli, kwa upande mwingine nguvu kubwa ya kiuchumi inatoa dhamana kubwa ya kujitawala kisiasa. Taarifa ya bunge la Marekani inasisitiza kuimarishwa kwa serikali kuu ya Iraq na kuimarisha udhibiti wa rasilimali kubwa ya mafuta ya Iraq, jambo ambalo limeathiri maslahi ya wakurd.

Pili taarifa inapendekeza kuwaruhusu maofisa wa utawala wa Saddam warudishwe madaraka yao, hatua hiyo imewaudhi sana wakurd. Wakurd wanachukia sana ukandamizaji uliofanywa kwao na utawala wa Saddam katika miaka mingi iliyopita. Kabla ya hapo mswada wa katiba mpya ya Iraq uliagiza kupigwa marufuku kwa wanachama wa "chama cha ustawishaji jamii cha kiarabu" kushiriki kwenye shughuli za kisiasa, hii imeonesha vilivyo imani ya wakurd pamoja na waislamu wa madhehebu la Shia kwa serikali, ambao walikandamizwa kama wakurd. Hapo baadaye kutokana na upinzani wa waislamu wa madhehebu la Suni, katiba ilirekebishwa na kupiga marufuku "wafuasi wa kundi la Saddam" kushiriki kwenye shughuli za kisiasa. Wakurd wanadai kulipiza kisasi dhidi ya utawala wa Saddam ili kulinda hadhi na maslahi yao katika utawala mpya. Ni dhahiri kuwa taarifa iliyotolewa na "kikundi cha utafiti wa masuala ya Iraq" cha Marekani imegusa suala nyeti la wakurd na kuwa moja kati ya mambo yanayolaaniwa sana na rais Talabani, kuwa inaharibu katiba ya Iraq.

Siku 2 zilizopita mkuu wa jimbo linalojiendesha la Wakurd Bw Mesud Barzani aliilaani taarifa hiyo akisema, taarifa hiyo inataka kuimarisha serikali kuu ya Iraq, hatua hii inakwenda kinyume na kanuni za utaratibu wa shirikisho na katiba ya nchi, ambayo ni msingi wa kuasisiwa kwa Iraq mpya. Msimamo wa kiongozi huyo unafanana na msimamo wa Bw Talabani. Wachambuzi wamesema, ingawa taarifa iliyotolewa na kikundi cha utafiti wa masuala ya Iraq imetoa mapendekezo mengi kwa serikali ya George Bush ili kuondokana na hali yenye matatizo nchini Iraq, lakini muda mfupi baada ya kutolewa, wakurd waliilalamikia vikali, na kuifanya nchi ya Iraq ikabiliwe na changamoto kubwa. Mapambano ya kimabavu yaliyoko nchini Iraq bado hayajatatuliwa, na mgongano wa madhehebu ya kidini nchini humo unakuwa mkali siku hadi siku. Kuweza kuondokana na hali yenye matatizo mengi nchini Iraq kwa Marekani, kwa sasa limekuwa suala linalofuatiliwa na vyombo vingi vya habari duniani.