Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-12-13 20:39:49    
Kenya kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya maradhi

cri

Profesa Kimani Njugu ambaye ni mwenyekiti wa chama cha kiswahili cha taifa la Kenya na pia anawakilisha nchi ya Kenya katika jumuia ya Afrika mashariki katika ukuzaji wa kiswahili na pia katika uundaji wa rasimu ya baraza la kiswahili la baraza la Afrika mashariki.

Miaka miwili iliyopita Profesor Kimani aliondoka katika chuo kikuu cha Kenyatta alipokuwa muhadhili katika idara ya Kiswahili ya chuo hicho na kwa sasa anafanya kazi katika Shirika la Afya la Afrika kama linavyojulikana AHADI likiwa ni kifupisho cha maneno ya Kiingereza Afrika Health And Develeopment International akiwa ni mwakilishi wa shirika hilo nchini Kenya. Kazi kubwa ya shirika ni kujaribu kutumia sanaa, maandishi na fasihi katika kukuza afya na pia wanatumia vyombo vya habari katika kuendeleza afya ya jamii.

Profesa Kimani amesema kazi wanazofanya katika shirika la AHADI ambalo ni shirika lisilo la kiserikali zinalenga masuala ya afya, na baadhi ya vitabu walivyoandika mpaka sasa ni pamoja na kitabu cha vibonzo, kitabu ambacho kinawasaidia vijana kujiepusha na matatizo ya kiafya kama vile Ngono za mapema na utumiaji wa madawa ya kulevya, na kitabu hiki kinawalenga vijana wenye umri kati ya miaka 10 na miaka 14, na kitabu chenyewe cha ni vibonzo kinaitwa daraja. Kitabu hiki kimeandikwa kwa lugha ya kingereza ili kiweze kuwafikia kwa urahisi vijana wa Kenya, Tanzania na Uganda.

Kitabu cha pili walichotoa ni ambacho kimweza kusimulia kazi walizofanya Bankong nchini Thailand mwaka mmoja uliopita, amacho kinaitwa "Closer to home" kikiwa na maana "karibu na nyumbani" Lengo la kitabu hiki ni kuonyesha kwamba tunapokuwa tunapambana na malazi ni lazima tulenge makazi ya watu, tusilenge nje ya makazi, tujaribu kuongea na wanajamii katika makazi yao. Katika kitabu hicho wamezungumzia unyanyapaa kwa waathirika wa ukimwi, matatizo ya tiba, matatizo ya chakula na mambo mengi yanohusu kudhuia ugonjwa wa ukimwi, hiki ni kitabu cha pili.

Kitabu cha tatu ambacho wameweza kuchapisha kinatokana na mradi walioutekeleza nchini Uganda, mradi ambao lengo lake lilikuwa ni kufanya kazi na vyomba vya habari hasa radio na magazeti ya Uganda katioka kuzungumza na vijana, kitabu kinaeleza hatua walizofuata katika kutekeleza mradi huo, matatizo waliyokumbana nayo na jinsi walivyoweza kuyatatua ili kuwaonyesha wengine watakaopenda kuteleza miradi kama hiyo jinsi wanavyoweza kutekeleza bila ya matatizo yoyote.

Pia wameweza kutoa kanda ya video inayozungumzia baadhi ya mbinu zinaweza kutumiwa ili kuwasaidia vijana kujiepusha na matatizo, kanda hiyo inaitwa "closer to home". Licha ya machapisho wameweza kuandaa mafunzo na warsha ambapo shirika lao liliweza kuwapeleka wasanii takriban 60 kutoka Tanzania, Kenya na Uganda kwenye kongamano la kimataifa la Bangkong ambapo waliweza kuigiza, kutumbuiza vizuri kuonyesha jinsi sanaa inavyoweza kutumiwa ili kuwasaidia wanajamii. Pia waliweza kuwapeleka wasanii na wafanyakazi wa huduma ya afya katika mkutano wa kimataifa Abuja nchini Nigeria mwezi october mwaka jana, pia waliweza kuaanda warsha ya jinsi ya kupambana na ugonjwa wa ukimwi,na mwaka mwezi wa nane wameweza kuwapeleka watu 8 katika kongamano la kimtaifa huko Toronto Canada kuzungumzia mbinu zinazoweza kutumiwa kuwsaidia wanajamii katika kupambana na maradhi.