Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-12-15 16:08:06    
Bw. Luo Hong anayeangalia bara la Afrika kwa kamera yake

cri

Kwenye ofisi ya Bwana Luo Hong ambaye ni meneja mkuu wa kampuni ya Holiland inayotengeneza keki, zinatandika picha nyingi za mandhari ya kimaumbile na wanyama pori alizopiga barani Afrika.

Kampuni ya Holiland inajulikana sana nchini China, sasa imekuwa na mitaji zaidi ya Yuan za Renmimbi bilioni moja na matawi zaidi ya 600 nchini kote. Lakini mwenyekampuni huyo Bwana Luo Hong anapenda zaidi upigaji picha, baada ya kumaliza shule aliwahi kujifunza upigaji picha kwa miaka miwili katika kampuni moja ya upigaji picha.

Baada ya kupata mafanikio makubwa katika biashara yake, Bw. Luo Hong bado hajasahau ndoto yake ya kuwa mpiga picha. Mwezi Oktoba mwaka 2001, Bw. Luo Hong alienda Afrika kwa mara ya kwanza kupiga picha za mandhari ya kimaumbile na wanyama pori. Mji wa kwanza Bw. Luo Hong alioutembelea barani Afrika ni Cape Town, Afrika kusini. Alitembelea bustani ya kitaifa ya wanyama pori, na kupiga picha nyingi za wanyama pori. Aligundua kuwa, bara la Afrika si kama tu lina mandhari nzuri, bali pia lina wanyama pori wengi wanaopendeza sana, kuanzia hapo aliwapenda wanyama pori hao.

Mwaka 2002, Bw. Luo Hong alikwenda Kenya kutembelea bustani ya Masai Mara na Namibia. Baada ya kurudi kutoka Afrika alianza kufanya utafiti kuhusu mambo ya Afrika ili kufahamu hali ya hewa, hali ya kijiografia ya nchi za Afrika na tabia za wanyama.

Bwana Luo Hong anajishughulisha mambo anayoyapenda kwa moyo wake zote. Katika miaka mitano iliyopita, kwa jumla alienda Afrika kwa mara 11 kwa ajili ya kupiga picha wanyama pori. Alisema:

" Kuanzia mara ya tatu kutembelea bara la Afrika nilianza kupata hisia kidogo, sasa nimefahamu kabisa namna ya kupiga picha wanyama pori barani Afrika."

Kila alipokanyaga kwenye ardhi ya Afrika, Bw. Luo Hong aliona vizuri sana, nguvu zinazomhimiza kwenda Afrika zinatokana na upendo wake kwa Afrika. Aliandika kwenye tovuti yake ya Blog:

"Afrika ni mbinguni mwa wanyama pori, huko wanaishi aina nyingi za wanyama pori duniani, na kuonesha uzuri wenye masikilizano usiokuwa na kifano kati ya mandhari, binadamu na wanyama."

Bw. Luo Hong aliangalia na kufurahia uzuri wa Afrika kwa kamera yake. Mwaka 2005 picha zake zilianza kuoneshwa ndani ya vituo vya reli ya ardhini mjini Beijing. Mwaka huu ili kuadhimisha siku ya mazingira duniani ya tarehe 5 Juni, shirika la mpango wa mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP lilimwalika Luo Hong aende mjini Nairobi kufanya maonesho ya picha, ambazo zinasifiwa sana na watazamaji.

Bwana Luo Hong pia aliwahi kukutwa na hatari mara kwa mara alipopiga picha barani Afrika. Mara moja alipopiga picha akifuatana na ndovu kike na watoto wake, ndovu kike baada ya kugundua kufuatwa alikasirishwa sana, alinyanyua kichwa chake akipiga makelele makali. Mwongozaji mwenye uzoefu mwingi alimwagiza dereva kurudi nyuma haraka haraka. Baada ya kurudi nyuma kwa mita zaidi ya mia moja hivi, Bw. Luo Hong aliona hali ya kuogopesha, yaani makundi mbalimbali ya ndovu walioitikia makelele ya ndovu huyo kike walikuwa wamezunguza mahali walikokuwepo. Kama hawakuweza kurudi nyuma haraka itakuwa hatari mno.

Mafunzo Bw. Luo Hong aliyoyapata katika safari zake barani Afrika ni kuwa, wanyama wengi pori wa Afrika ni wema kwa binadamu, lakini sharti ni usiwahamasisha kwa kusumbua maisha yao ya kawaida.

Bw. Luo Hong aliwahi kutembelea nchi 6 za Afrika, na kukutana na wakazi wengi za kawaida, picha nzuri aliyopata kuhusu watu wa Afrika ni kwamba, watu wa Afrika wanaishi kwa furaha, tabia zao za kuwa na furaha imemfurahisha yeye, hivyo kila alipokwenda kwenye nchi za Afrika yeye huona furaha mwenyewe. Alisema kuwa, akiwa na wakati mwaka huu, atakwenda tena barani Afrika.

Bw. Huo Hong anapenda wanyama kuanzia utotoni, safari zake za barani Afrika zimempa picha nzuri ya uhusiano wenye masikilizano kati ya watu wa Afrika na wanyama. Alisema:

"Serikali za nchi nyingi za Afrika zinaweka mkazo kuwalinda wanyama pori na kuhifadhi mazingira, zaidi ya hayo wakazi wa Afrika pia wana upendo kutoka moyoni kwa wanyama, mambo hayo yananishangaza kweli."

Akiwa shabiki wa upigaji picha anayefuatilia suala la mazingira, Bw. Luo Hong alieleza matumaini yake kuwa, watu wanapofurahia picha zake, wataweza kusikia mwito wa maumbile kutoka kwa picha alizopiga. Alisema:

"Natarajia kuwa tutaonesha shukurani kwa maumbile, na kufanya mambo mazuri kwa maumbile, tutaishi pamoja na wanyama na maumbile kwa masikilizano."

Idhaa ya kiswahili 2006-12-15