Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-12-15 16:13:17    
Waziri wa habari wa Kenya Mheshimiwa Muthai Kagwe ahojiwa na CRI

cri

Mheshimiwa Kagwe akieleza lengo hasa la safari yake nchini China na pia kuhusu maonyesho ya teknologia ya habari na mawasiliano yaliyofanyika Hong kong hivi karibuni alianza kwa kusema, kwanza nimekuja hapa kuhudhulia mkutano wa ITU,na pia kukutana na makampuni ya mawasiliano tunayofanya nayo kazi nchini Kenya na Afrika ya mashariki kwa ujumla pamoja na kukutana na maofisa wa juu wa serikali ya China wakiwemo waziri wa habari, na waziri wa mawasiliano ili kuweza kuona ni jinsi gani nchi zetu mbili zinaweza kusaidiana na sio kwa nchi mbili tu bali Afrika kwa ujumla.

Akielezea kuhusu mambo yaliyomvutia katika mkutano mkubwa wa kimataifa kuhusu sekta ya mawasiliano ya habari uliofanyika Hong Kong Msheshimiwa Kagwe alisema, kwanza ni teknolojia ya juu ya mawasiliano, maana bila ya kufika sehemu kama hiyo huwezi kuelewa ni kitu gani mnachofanya nyumbani, ni kama waswahili wanavyosema, unaweza kufikiri ni mama yako ndio anajua kupika lakini ukitembea kidogo ndio utajua kuwa kuna wengine wanajua kupika.Kwa kweli maonyesho ya Hong Kong yalikuwa makubwa sana na vilionyeshwa vyomba gani vinavyotumika siku hizi katika sekta ya habari na mawasiliano katika dunia ya leo, kwa hiyo ni muhimu sana kwenda ili kujionea vitu gani vinatumika duniani, watu wanafanya nini huko ulaya, kwa sababu sio lazima tupitie njia ile ile waliyopitia ili kufikia pale walipo, bali tunaweza kuruka mara moja kutoka chini na kuanza kutumia teknologia ya leo badala ya jana.Kwa ujumla kulikuwa na watu wengi sana huko kutoka Afrika wakiwemo rmawaziri ambao walikuja kujionea tupo wapi, tunaenda wapi na kesho tutakuwa wapi.

Mheshimiwa Kagwe aliendelea kusema kuwa katika sekta ya teknolijia ya mawasiliano bado Afrika ipo nyuma na inabidi kujitahidi kusonga mbele, inabidi kuyaweka mambo ya teknolojia ya mawasiliano katika siasa, kwa sababu tumekuwa tunazungumzia sana uzalishaji wa kilimo na kusahau kuweka mawasiliano katika mipango ya nchi zetu, kwa hiyo ni muhimu kuipa kipaumbele teknojia kwa sababu hatuwezi kuendelea bila teknolojia.

Akijibu hoja kuhusu vyombo vya habari vya Kenya kumnukuu akisema China itaisaidia kenya kujenga mfumo wa mawasiliano wa CDMA, waziri Kigwe alisema, kwanza naomba ieleweke kuwa huo sio msaada, ni ushirikiano, sio kwamba upande wa Kenya unapata bure, ni kununua kutoka makumpuni ya China au kupata mkopo na unajenga kitu chako na baadaye unalipa mkopo.Na teknolojia hii ya CDMA ni ile inayoweza kupeleka mawasiliano vijijini bila kutumia waya, maana hivi sasa Kenya, Tanzania na Uganda tuna shida sana ya kuibiwa nyaya kwa sababu watu wanafikiri ile copper katika nyaya ina thamani kubwa hivyo wanaenda kuuza, hivyo tukipata teckolojia hii mpya itatusaidia sana. Tumeshaanza kufanya nao kazi na awamu ya kwanza ya mpango huu utamalizika mwezi March mwaka ujao halafu ndio tutamaliza awamu ya pili.

Mpango huu wa CDMA sio wa nchi zote za Kenya, Uganda na Tanzania bali nchi inchi ina mpango wake, ila mwishowe zinaungana, mtu kutoka kijiji cha Tanzania anaweza kumpigia simu mtu aliyepo katika kijiji nchini Kenya au Uganda, kwa hiyo ingawa kila nchi inafanya mpango wake lakini mwisho itakuwa ni kitu kimoja.

Kuhusu uhusiano kati ya utalii na teknologia ya habari na mawasiliano, mheshimiwa Kagwe alisema,katika dunia ya leo mtu akitaka kutembelea Kenya au Tanzania na hasa mtu aliyepo China au ujerumani na anataka kwenda kutembea masai mara siku hatataka tena kupiga simu ili kupanga safari yake, ataingia katika internet kuangalia sehemu anazotaka kwenda na kama ni kulipa analipa hapo hapo katika internet na pesa zinakwenda Tanzania au Kenya, lakini ilivyo sasa mtu hawezi kulipa katika internet, hivyo analipa hukuhuko ulaya na pesa yote inabaki huko, akija Kenya anakula tu na kununua kinyago kimoja cha ndovu, kwa hiyo faida yote inabaki ulaya.

Kwa hiyo lazima serikali zetu na mabenki hata yale ya binafsi yaweze kufikiria ni kwa namna gani fedha hiyo inaweza kurudi kwetu, kwa mfano tunawafurahia sana watalii kutoka China kwa sababu wanatumia pesa nyingi sana kwetu wanapokuja kutalii.

Akizungumzia kuhusu tofauti kubwa ya gharama za internet kati ya China na nchi za Afrika Mashariki, waziri Kagwe alisema, jambo linalofanya gharama za internet na mawasiliano kwa nchi za Afrika mashariki kuwa kubwa zinatokana na sababu ya nchi hizo kutumia satellite wakati China inatumia Optical Fiber, ukitumia satellite gharama zinakuwa kubwa sana, na hiyo Optical Fiber ni kuhusu cable ambayo tumeizungumzia sana, na hivi kuna mipango miwili ya kuileta hiyo cable katika Afrika ya Mashariki ambayo iko mbioni kufanyika, mpango wa kwanza ni kuileta cable hiyo kutoka Afrika ya kusini, cable moja itatoka huko kupitia dar es salaam hadi Mombasa na kwenda juu hadi Djibuti na port sudan, na huo mpango unaitwa EAZY. Na mpango mwingine ni wa kujenga cable kutoka Fujaela kupitia china ya bahari mpaka Mombasa, sasa hizo cable zikiwa zimejengwa gharama za internet na mawasiliano zitakuwa chini kabisa kupita hata hapa China

Akieleza maendeleo ya sekta ya habari na mawasiliano katika miaka 43 tangu Kenya ijipatie uhuru wake kutoka kwa waingereza, waziri Kagwe alisema, akikumbuka nyuma kidogo Afrika ya kusini ilikuwa nyuma katika sekta ya mawsiliano na Afrika ya mashariki ilikuwa imepiga hatua, lakini ilifika wakati, sijui hata ni kwa namna gani, katika miaka ya 1975 na 1976 serikali za wakati huo zikaanza kuogopa mambo ya mawasiliano, walikuwa wakisikia teknolojia mpya walikuwa wanafikiri nini teknolojia za kupindua serikali, kwa hiyo walijikinga na maendeleo badala ya kuichukua teckonojia mpya wakaizuia issingie katika nchi zetu, kwa hiyo katika karibu miaka 20 hivi tukawa nyuma kabisa katika katika upande wa teknonojia. Lakini siku hizi sasa makampuni na hasa serikali za nchi za Afrika mshariki zimeamua sasa lazima ziwe na teknolojia ya kisasa na kwa bahati teknolojia ile ya wakati ule ambao sisi tulikuwa tumelala imeshapitwa na wakati kwa hiyo sasa tuna nafasi ya kwenda hata katika dunia ya kesho.

Kuhusu uhusiano na ushirikiano kati ya China na Kenya waziri Kigwe alisema, kwa muda mrefu uliopita macho ya Afrika kwa ujumla yalielekezwa ulaya ya magharibi lakini katika siku hizi Afrika imeanza kufikiri na kuelewa hali ya dunia jinsi ilivyo, na kwa upande wa China tulikuwa hatujuia sana kuhusu uchina na wao walikuwa hawajui sana kuhusu Afrika, kwa hiyo sasa ukiangalia mkutano wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, hakuna mkutano wowote uliofanyika kama huu huko ulaya ahata uingereza kwenyewe ambayo ilikuwa nguvu ya ukoloni, haijawi kuwa na mkutanona Afrika yote katika mkutano mmoja, na sasa mkutano huo raisi wa China aliongea na waafrika wote, alitembelea nchi za Afrika kiwemo Kenya na Tanzania kwa mtazamo mpya, sio kama vile ilivyokuwa inaonekana na macho ya wazungu wa ulaya na Amerika hata ulisoma magazeti na kusikiliza vyombo vya habari kama BBC au CNN utasikia tu Afrika kuna njaa, kuna Aids,ni kama Afrika hakuna watu hai wanaotembea au ni kama waafrika wanasubiri kufa, lakini ukifikiria hayo maneno ndiyo inabidi tubadilishe mtazamo, na ninachowaomba wachina nao wasishikwe na mtego huo wa kufikiri kwamba Afrika haiwezi kujisaidia yenyewe, Ndio maana CRI imefungua kituo cha matangazo nchini Kenya sasa ikiwa nchi ya kwanza Afrika, kwa hiyo sasa ibadilishe mtazamo wa kimagharibi kutangaza vibaya kuhusu Afrika, BBC na CNN wakizungumzia 3% ya watu wenye AIDS nyinyi zungumzieni wale 97% ambao hawana AIDS wachina lazima wawe na macho mengine tofauti na vyombo vya magharibi, na hiyo itasaidia sana uhusiano wetu, vilivile ukiangalia china sasa inaendelea na sisi pia tunaendelea, ukiangalia mipango yao ya baadaye inaewza kutusaidia pia na sisi kwa sababu mipango hiyo inapangwa kulingana na shida walizonazo, na shida zao zinafanana na zetu, lakini wewe ukifuata mipango ya England, shida zao sio kama za kwa kwetu, kwa mfani nilipokuwa naongea na waziri alianiambia kule sehemu za magharibi zina shida ya mawasiliano ya simu, na hii kama katika sehemu za vijiji kule kwetu, kwa hiyo teknologia wanayotumia huko inaweza kusaidia hata sisi, lakini kama ukifuata ya Swatzerland ni mambo ambayo hayalingani.

Idhaa ya kiswahili 2006-12-15