Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-12-19 15:56:57    
Naibu mkuu wa benki ya maendeleo ya Asia apongeza maendeleo iliyoyapata China

cri

Naibu mkuu wa benki ya maendeleo ya Asia, Bw. Roluns Greenwood tarehe 11 alipohojiwa na mwandishi wa habari wa shirika la habari la Xinhua aliipongeza China kwa maendeleo iliyoyapata katika miaka mitano iliyopita tangu ijiunge na shirika la biashara duniani, WTO.

BW. Greenwood alisema China kujiunga na WTO kumeleta athari nzuri kwa maendeleo ya uchumi wa China. Katika miaka mitano iliyopita, China imetekeleza ahadi ilizotoa wakati ilipojiunga na WTO, ilianzisha marekebisho mengi kuhusu muundo wa uchumi, na imepata maendeleo hatua kwa hatua. Maendeleo ya kasi ya uchumi ya China yameimarisha imani ya China kwenye jukwaa la dunia. Alisema.

"Kutokana na mageuzi hayo, serikali ya China inapata uungaji mkono mkubwa nchini China, hatua ambayo imeweka msingi kwa China kuendelea kutekeleza sera za mageuzi katika siku za baadaye",

Licha ya kusifu maendeleo ya iliyoyapata China katika mageuzi ya benki, Bw. Greenwood pia alisema kuwa ni muhimu sana kwa China kuendeleza kwa undani mageuzi ya mambo ya fedha, alisema baadhi ya maeneo yanayohitajiwa sana kufungua mlango, ikiwemo sekta ya hisa, ni changamoto inayokabili China katika siku za usoni.

Mbali na hayo Bw Greenwood alisema China ikiwa mmoja wa wanachama wa WTO, kadiri athari yake inavyoongezeka kwenye jukwaa la dunia, ndivyo inavyotakiwa kufanya kazi ya kuongzoza katika kuzindua upya mazungumzo ya Doha.

Alipozungumzia suala la utandawazi wa uchumi, Bw. Greenwood alisema, benki ya maendeleo ya Asia inazingatia sana suala la kukosa uwiano katika maendeleo ya uchumi wa dunia, zikiwa nchi mbili kubwa kabisa za kiuchumi duniani, China na Marekani zimekuwa vyanzo viwili vikubwa vinavyoathiri uwiano wa uchumi wa dunia, kwa China inatakiwa kupunguza usafirishaji wa bidhaa kwa nchi za nje kwa njia ya kuhimiza ununuzi wa nchini kutokana na kupunguza kiasi cha fedha za akiba zilizowekwa benki, kwa Marekani, inatakiwa kuongeza kiasi cha fedha za akiba zinazowekwa benki, kupunguza pengo linalotokea kati ya pato na matumizi kwa njia ya kupunguza matumizi ya fedha.

Bw. Greenwood anaona kuwa katika wiki za karibuni China na Marekani zilikuwa na mazungumzo ya kwanza kuhusu mambo ya uchumi, hiyo ni "habari nzuri ya kusisimua", na inachangia kuimarisha ushirikiano wa pande mbili za China na Marekani na kuhimiza maendeleo tulivu ya uchumi duniani.

Kwenye mkutano wa kazi za uchumi wa taifa, ambao ulifungwa wiki iliyopita, imefahamika kuwa serikali ya China itazingatia na kulishughulikia zaidi kundi la watu wenye kipato kidogo ikiwa ni pamoja na kutoa misaada ya fedha kwa sehemu zilizoko nyuma kimaendeleo katika mwaka kesho, jambo ambalo lilisifiwa sana na Bw. Greenwood.

Alisema uamuzi huo wa serikali ya China unachangia kupunguza tofauti kati ya miji na sehemu ya vijiji nchini China na kuboresha maisha ya watu wenye kipato kidogo. Lakini alisisitiza pia kuwa serikali ya China inatakiwa kuinua kiwango cha utoaji huduma katika uboreshaji wa elimu, matibabu na dhamana ya jamii vya sehemu ya vijiji, alisema kuwa benki ya maendeleo ya Asia pia itaongeza misaada kwa maeneo hayo.

Mbali na hayo alisema, mkazo wa utoaji mikopo wa benki ya maendeleo ya Asia nchini China unaelekea kwenye maeneo muhimu yalithibitishwa katika mpango wa 11 wa maendeleo ya miaka mitano, hususan eneo la uokoaji nishati, ikiwa ni pamoja na kutoa misaada kwa baadhi ya mikoa kujenga miradi ya kutumia nishati endelevu, kubana matumizi ya nishati na kutumia gesi iliyopo kwenye migodi ya makaa ya mawe. Bw. Greenwood alisema 'tunaona, tukifanya hivyo tutaweza kukidhi vizuri zaidi mahitaji ya serikali ya China.

Idhaa ya kiswahili 2006-12-19