Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-12-20 16:26:53    
China yarusha satellite mpya ya hali ya hewa ili kuinua uwezo wake wa kutoa tahadhari dhidi ya maafa

cri

Tarehe 8 Desemba, China ilirusha kwa mafanikio satellite ya utafiti wa hali ya hewa ya "Fengyun No.2 D", na kuituliza kwenye mstari wake iliyopangwa kwenye anga ya tropiki. Baada ya siku kadhaa itaanza kufanya kazi na kutuma picha za mawingu. Imefahamika kuwa satellite hiyo mpya ya hali ya hewa itaimarisha uwezo wa China wa kusimamia na kutoa tahadhari kuhusu hali ya hewa inayoweza kusababisha maafa ya kimaumbile.

Kutokana na tofauti ya njia satellite inayozunguka, satellite ya hali ya hewa inagawanywa kuwa aina mbili, ya kwanza ni setilaiti inayozunguka angani juu ya ncha za dunia, kila siku inafanya uchunguzi mara mbili ili kupata data za hali ya hewa duniani, ya pili ni setilaiti inayozunguka kwa mwendo wa dunia kwenye mstari wake kwenye anga ya tropiki, kufanya uchunguzi mfululizo kwenye theluthi mbili ya eneo la dunia. Setilaiti "Fengyun No.2 D" iliyorushwa tarehe 8 Desemba ni setilaiti ya hali ya hewa inayozunguka kwa mwendo wa mzunguko wa dunia kwenye mstari wa angani juu ya tropiki. Kabla ya hapo, China ilirusha kwa nyakati tofauti setilaiti 7 za utafiti wa hali ya hewa, na kuwa moja ya nchi chache zenye setilaiti zinazozunguka kwenye anga ya juu ya ncha za dunia na setilaiti zinazozunguka kwa mwendo wa mzunguko wa dunia kwenye anga ya tropiki.

Mkurugenzi wa kituo cha hali ya hewa cha setilaiti cha China Bwana Yang Jun amefahamisha kuwa, setilaiti "Fengyun No.2 D" ina uzito wa tani 1.39, na imesanifiwa kufanya kazi kwa miaka mitatu. Setilaiti hiyo imezatitiwa kwa vifaa vya kisasa vya aina mbalimbali, ambavyo vitakusanya na kutuma takwimu za ukaguzi kuhusu hali ya hewa, bahari, na maji, pia kufanya ukaguzi kuhusu mionzi ya jua na mwangaza wa anga ya juu. Bw. Yang Jun alisema

"Setilaiti 'Fengyun No.2 D' itashirikiana na setilaiti "Fengyun No.2 C" ili kuinua uwezo wa China wa kufanya ukaguzi kuhusu hali ya hewa, zitainua ufanisi wa ukaguzi na utabiri wa hali ya hewa."

Mbali na hayo, kufanya kazi kwa pamoja kwa setilaiti hizo mbili kutapanua eneo la kukaguliwa. Naibu mkuu wa idara ya hali ya hewa ya China Bwana Yu Rucong amesema, hivi sasa nchi mbalimbali duniani zinajishughulisha na utafiti na ukaguzi wa hali ya hewa kwa kutumia setilaiti, kwa sababu setilaiti ya hali ya hewa ina ubora wake ikilinganishwa na njia nyingine za ukaguzi wa hali ya hewa, ambazo zimefanya kazi muhimu sana katika kukagua mfumo wa hali ya hewa kama vile kimbunga na dhoruba. Bibi Wei Caiying alisema:

"Kwa mfano wakati kimbunga kinapoingia barani, tunaweza kutambua kimbunga hicho kwa kutumia vifaa vilivyowekwa ardhini kama rada, lakini wakati kimbunga kinapokuwa baharini ya mbali, ni setilaiti tu inayoweza kupata taarifa kuhusu hali yake. Kimbunga cha "Chanchu" ni kimbunga kikali kabisa kilichotokea katika miongo kadhaa iliyopita, nguvu yake ilifika 17, kama siyo setilaiti kufanya uchunguzi na kuripoti kwa wakati, kingeleta madhara makubwa zaidi. Kutokana na kupata utabiri sahihi kwa wakati, serikali za mikoa ziliweza kuwahamisha wakazi milioni kadhaa na kupunguza hasara kubwa kwa maisha na mali za wananchi."

Licha ya hayo idara za hali ya hewa za China kila mwaka zimekagua maafa ya kimazingira kwa kupitia setilaiti za hali ya hewa kama vile maafa ya moto na dhoruba ya mchanga, na kutoa huduma kwa wakati kwa serikali na idara katika ngazi mbalimbali kukinga na kupambana na maafa hayo. Bwana Fang Xiang kutoka kituo cha setilaiti ya hali ya hewa cha China amesema, mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu, setilaiti ya hali ya hewa ilifaulu kukagua na kuripoti maafa kubwa ya moto kwenye misitu yaliyotokea katika mkoa wa Mongolia ya Ndani na mkoa wa Heilongjiang.

Imefahamika kuwa setilaiti "Fengyun No.2 D" itaanza kufanya kazi rasmi baada ya miezi mitatu au sita. Licha ya kufanya utafiti wa hali ya hewa, setilaiti "Fengyun No.2 D" pia imechukua jukumu la kutoa huduma za hali ya hewa kwa ajili ya michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008 ya Beijing, hasa mabadiliko ya hali ya hewa wakati wa ufunguzi na ufungaji wa michezo hiyo na kwenye siku za michuano muhimu.

Bw. Yu Rucong alisema kurushwa kwa setilaiti hiyo si kama tu kumeinua uwezo wa China wa kutoa tahadhari ya maafa ya kimaumbile, bali pia itatoa huduma bora ya mambo ya hali ya hewa kwa China. Akisema

"Setilaiti za hali ya hewa za China ni setilaiti muhimu za mfumo wa ukaguzi wa shirika la hali ya hewa duniani WMO. Baada ya kufaulu kurusha setilaiti hiyo, tutajitahidi kujenga mfumo wa takwimu zinazoletwa na setilaiti kwa ajili ya idara mbalimbali nchini China, pia kwa ajili ya kubadilishana tarakimu na nchi nyingine ili kuinua kiwango cha huduma za hali ya hewa duniani."

Hivi sasa Australia, Japan, Singapore, Malaysia, Philippines na Korea ya kusini zinatumia takwimu zilizokusanywa na setilaiti za China. Habari zinasema hivi sasa China iko mbioni kutafiti na kutengeneza setilaiti ya hali ya hewa yenye uwezo mkubwa zaidi na kupangwa kurushwa mwaka 2012.

Idhaa ya kiswahili 2006-12-20