Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-12-20 19:28:35    
Mapishi ya vipapatio vya kuku na pilipili mboga

cri

Mahitaji

Vipapatio vya kuku 20, pilipili mboga gramu 300, tangawizi gramu 150, vitunguu maji, gramu 5, pilipili manga gramu 5, unga wa pilipili hoho kijiko kimoja, mchuzi wa sosi kijiko kimoja, chumvi vijiko vitatu

Njia

1. kata kila kipapatio kiwe vipande vitatu, kata pilipili mboga iwe slesi, kata tangawizi, vitunguu maji viwe vipande

2. washa moto tia mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya vipapatio kwenye sufuria, korogakoroga tia vipande vya vitunguu maji na tangawizi, korogakoroga, tia pilipili manga na unga wa pilipili hoho kwenye sufuria, korogakoroga mimina mchuzi wa soya, tia pilipili mboga korogakoroga, tia chumvi korogakoroga. Ipakue mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.