|
hivi karibuni mapambano ya kisilaha yamepamba moto nchini Somalia. Tarehe 21 mwezi Desemba jeshi la kundi la muungano wa mahakama za kiislamu, ambalo linadhibiti mji wa Mogadishu, na sehemu kubwa ya nchi hiyo, limetangaza kuwa Somalia imejiandaa kupambana na Ethiopia. Kundi hilo pia limetoa wito wa kutaka wasomali wote wajitokeze kushiriki katika mapambano dhidi ya Ethiopia.
Kuanzia mwaka 1991, Somalia iliingia kwenye hali ya kutokuwa na serikali, isipokuwa sehemu mbalimbali za nchi hiyo zilikuwa zinadhibitiwa na wababe wa kivita. Mwaka 2004 serikali ya mpito ilianzishwa nchini Kenya, ambayo ilihamia nchini Somalia katika mwaka uliofuata. Lakini kutokana na kutokuwa na nguvu ya kutosha, serikali hiyo inashindwa kudhibiti ipasavyo hali ya nchi hiyo. Katika miezi michache ya karibuni, nguvu ya kundi la muungano wa mahakama za kivita iliimarika kwa haraka, na sasa kundi hilo limeudhibiti mji mkuu Somalia pamoja na sehemu kubwa ya nchi hiyo, lakini serikali ya mpito ya nchi hiyo inaweza tu kuendesha shughuli zake katika tarafa ya Baidoa, umbali wa kilomita 250 hivi kaskazini magharibi mwa Mogadishu, na inatishiwa na nguvu inayoongezeka kwa mfululizo ya majeshi ya madhehebu ya kidini. Hivyo serikali ya mpito imetoa wito mara nyingi kutaka jumuiya ya kimataifa itume jeshi la kulinda amani nchini Somalia kuisaidia serikali kuu kutumia madaraka yake; Lakini majeshi ya madhehebu ya kidini yanapinga majeshi ya nchi za kigeni kuingia nchini humo, yakidai kuwa majeshi ya kigeni yatakayoingia nchini Somalia yatachukuliwa kama ni majeshi ya uvamizi. Mwezi Julai mwaka huu, kiongozi wa Kundi hilo alitoa wito wa kuanzisha "vita ya jihad" dhidi ya jeshi la Ethiopia lililoko nchini Somalia kuiunga mkono serikali ya mpito ya nchi hiyo; mwezi Novemba mazungumzo kati ya majeshi ya madhehebu ya kidini na serikali ya mpito yalivunjika, ambapo majeshi ya kidini yalisema sharti la kukurejesha upya mazungumzo ni jeshi la Ethiopia kuondoka nchini Somalia; Tarehe 12 mwezi Desemba, kundi la muungano wa mahakama za kiislamu lilitoa taarifa ya mwisho kwa jeshi la Ethiopia lililoko nchini Somalia na kulitaka liondoke kutoka kwenye nchi hiyo ndani ya wiki moja, la sivyo litashambuliwa na majeshi ya nchi hiyo. Tarehe 19 usiku, mnamo saa mbili tu baada ya kufikia kikomo hicho, majeshi ya madhehebu ya kidini ya nchi hiyo yalianzisha mapambano dhidi ya vituo viwili vya mafunzo vya serikali ya mpito vilivyoko karibu na Baidoa.
Jambo linalosikitisha ni kuwa katika siku yalipotokea mashambulizi ya kijeshi, rais Abdullahi Yusuf wa serikali ya mpito ya Somalia alikuwa na mazungumzo na Sheikh Hassan Dahir Aweyes, kiongozi wa kundi la muungano wa mahakama za kiislamu. Na baada ya mazungumzo hayo, kwenye mkutano na waandishi wa habari Michel alisema, pande mbili zimeahidi kusimamisha vitendo vya uhasama, kurudisha mazungumzo bila masharti na kutafuta kwa pamoja njia ya kisiasa ya kutatua mgogoro wa Somalia. Baada ya mazungumzo yao Bw Aweyes, alisema mapambano ya kisilaha yaliyotokea siku ile kuwa ni "tukio dola la ghafla" tu, tena mazungumzo yamefikia mwafaka.
Lakini 'mwafaka uliofikiwa" haukuonekana katika vitendo vyao. Siku mbili baadaye, mapambano yalienea kwenye sehemu nyingi zaidi, huku malumbano ya kisiasa kati ya serikali ya mpito na majeshi ya kidini pia yakiongezeka. Kila upande ulidai umedhoofisha vibaya nguvu ya upande mwingine. Ofisa wa ngazi ya juu wa wizara ya ulinzi ya serikali ya mpito ya Somalia tarehe 21 alipohojiwa na waandishi wa habari huko Baidoa, alisema jeshi la serikali lilijibu mashambulizi ya majeshi ya kidini, na liliwaua watu 71 na kuwajeruhi wengine 221 wa majeshi ya kidini. Lakini msemaji wa kundi la mahakama za kiislamu huko Mogadishu alisema, hivi sasa jeshi la kundi hilo limeteka tarafa ya Idale iliyoko kusini magharibi mwa Baidoa, na liliwaua askari 70, ambao wengi wao ni askari wa Ethiopia. Lakini Ethiopia ilikanusha kuwa ilishiriki kwenye mapambano hayo, na kusema kuwa Ethiopia haina askari wengi nchini Somalia isipokuwa waalimu wachache wanaotoa mafunzo kwa wanajeshi wa serikali ya mpito.
Mapambano katika siku zilizopita yalisababisha vifo na majeruhi ya watu wengi, miili mingi ilikuwa imesambaa kwenye barabara ya tarafa ya Idale, ambayo ni moja ya sehemu zilizokumbwa na mapambano. Mkazi mmoja wa huko alisema, wakazi wa huko sasa wamekimbia makazi yao ili kujiepusha na vita.
|