Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-12-22 20:21:52    
Mahojiano na msikilizaji wetu kutoka Tanzania Bw. Frans Ngogo

cri

Ras Frans Ngogo ni mmoja kati ya washindi maalum wa chemsha bongo ya radio china kimataifa kutoka Nchini Tanzania ambaye alipata nafasi ya kuja China kusherekea miaka 65 tangu kuanzishwa kwa radio China Kimataifa.

Ras Manko akieleza jinsi alivyojisikia baada kujulishwa kuwa amekuwa mshindi wa nafasi maalum na amepata nafasi ya kutembelea China alisema; "awali ya yote nilishukuru sana na moyo wangu ulisharidhika kwani nilishajaribu mara nyingi sana katika chemsha bongo na kuishia kuwa mshindi wa kwanza, na sio mshindi maalum, kwa hiyo naweza kusema nilikuwa na asilimia 90 kuwa ningeshinda kwani ni mara yangu ya tatu sasa kushiriki katika chemsha bongo na kupata nafasi ya kwanza, kwa kweli nilijiskia kama nimeshafika Beijing"

Bwana Ras Manko alipata habari za kuwa mshindi kupitia ujumbe wa simu ya mkononi kutoka kwa rafiki yake na msikilizaji mwenzake wa radio wa China Kimataifa bwana Onesmo Mponda kutoka mjini Morogoro, na baadaye ndipo aliweza kuwasiliana na wahusika wa radio China kimataifa. Na zaidi ya Bwana Mponda pia kuna wasikilizaji wengine wengi ambao walimjulisha kuwa amepata nafasi ya mshindi maalum katika chemsha bongo ya radio China kimataifa, na hawa ni pamoja na Mzee Thobias Magaigwa, Chacha Magere, Bwana Girocho Chacha Bwiru, kutoka kikomori, Tarime, na bwana Mogire Machuki wa Kisii nchini Kenya, na bwana Ayub Mtanda, kwa hiyo amewashukuru sana wasikilizaji wenzake hawa. Ras Ngogo aliongeza kuwa ilikuwa rahisi kupata habari za ushindi wake kwa sababu kwa sasa amekuwa maarufu kwa wasikilizaji wa radio China Kimataifa kutokana na kutumiana salamu.

Ras Ngogo akieleza kuhusu ushirikiano kati ya wasikilizaji wa Radio China kimataifa alisema, Radio china kimataifa ndiyo inayowaunganisha, kwa mfano Bwana Onesmo yeye ni mtumaji mzuri wa salaam na msikilizaji mzuri, bwana Mogire Machuki ambaye ni msikilizaji maarufu na ndiye hasa aliyemfanya akaifahamu zaidi Radio China Kimataifa, ingawa anasikitika sana kuona kuwa ameshindwa kufika China, kwa sababu tokea zamani kidogo katika ya miaka ya 1989 na 1992 wakati akiishi Mwanza, aliwahi kumwandikia barua ambayo ndani kulikuwa na karatasi iliyoonesha jinsi alivyoshiriki kwenye chemsha bongo ya wakati ule, na akimshauri bwana Ngongo naye ashiriki kwenye chemsha bongo ya Radio China Kimataifa, kwa hiyo kwa kifupi ndiye aliyemfanya awe msikilizaji maarufu kwa kupitia radio China Kimataifa.

Bwana Ngogo alisema, "Wakati ule radio China kimataifa ilipomtembelea Kisii pamoja na wasikilizaji wengine wa magharibi mwa Kenya, Bw Machiki alinitumia ujumbe zaidi ya mara nne kunialika niende huko, na aliniambia niende hata kama sitapewa nauli ya kurudi basi yeye angenipa. Kwa kweli nilikwenda na nilipata bahati ya kufahamiana na wasikilizaji pamoja na watangazaji wa radio china kimataifa akiwemo Mama Cheni na Zahra.

Ras Ngogo alianza kuisikiliza radio china Kimataifa Miaka 10 iliyopita, na katika kipindi cha nyuma anasema matangazo ya Radio china Kimataifa hayakuwa na nguvu na usikivu wake ulikuwa chini, anafikiri labda hali hiyo ilitokana na kiwango cha sayansi na teknolojia cha wakati huo, lakini kwa sasa radio China kimataifa imekuwa na nguvu na kasi kwani radio pekee inayoweza kuwafanya wasikilizaji kuelewa na kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwa wasikilizaji, alisema kwa mfano tuzo ya kuja China kutalii ni ya kipekee sana na anadhani hii ni radio pekee inayotoa tuzo ya namna hii duniani.

Ras Manko alisema" Kutokana mtu kama yeye ambaye ni mkulima uwezo wake ni mdogo, na hakuwahi kutarajia kuwa siku moja atakuja kutembelea China au hata kwenda Somalia au hata Dubai ambapo ni jirani zaidi na Tanzania, lakini leo hii radio china kimataifa imeweza kumfikisha mashariki ya mbali ambapo China ilipo"

Akieleza kuhusu Klabu yake ya Kemogemba, Ras Manko alisema zamani kabla Radio China kimataifa haijaungana na KBC, walikuwa wanapata matangazo ya Radio China kwa taabu, lakini sasa wasikilizaji wengi katika Klabu yao ya Kemogemba kwa sasa wanaweza kushika mawimbi ya CRI kutoka KBC kupitia masafa mafupi.