Baada ya nchi sita za Russia, Marekani, China, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kufanya majadiliano kwa miezi miwili, baraza la usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 23 Desemba lilipitisha kwa kauli moja azimio No. 1737 kuhusu suala la nyuklia la Iran. Azimio hilo lenye lengo la kupiga marufuku mpango wa nyuklia na mradi wa makombora wa Iran, limeonesha maoni na matakwa ya jumuiya ya kimataifa kuhusu suala la nyuklia la Iran, hivyo limeionesha Iran ishara dhahiri. Lakini kutokana na maoni makali ya Iran kuhusu azimio hilo na kutoridhika kwa Marekani kwa azimio hilo, azimio hilo limefungua kipindi kipya cha mabishano kati ya pande mbalimbali husika za suala la nyuklia la Iran, hivyo suala hilo halitatatuliwa kwa urahisi.
Azimio No. 1737 linaitaka Iran iache mara moja shughuli zote za kinu cha maji mazito na kusafisha uranium nzito, kuzitaka nchi mbalimbali zipige marufuku usafirishaji wa vifaa, teknolojia na zana zinazohusika na kusafisha uranium nzito, kinu cha maji mazito na makombora kwa Iran, na kusimamisha matumizi ya mali za watu na makampuni yanayohusiana na miradi ya Iran ya kusafisha uranium nzito na kutengeneza makombora pamoja, na kusimamia kwa makini watu husika wanaoingia na kutoka nchini Iran.
Muswada rasmi wa kwanza wa azimio hilo ulikabidhiwa tarehe 24 Oktoba na Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Pande husika zina tofauti kubwa kuhusu muswada huo, Marekani inaona kuwa, muswada huo haujachukua hatua kali ya kuweka vikwazo dhidi ya Iran, lakini Russia inaona kuwa kuweka vikwazo hakutasaidia utatuzi wa kiamani wa suala la nyuklia la Iran, na ikidai kufanya marekebisho kuhusu muswada huo. Hivyo muswada uliopitishwa tarehe 23 Desemba ulikuwa umefanyiwa marekebisho kwa mara nne.
Iran imetoa maoni makali kuhusu azimio No. 1737, wizara ya mambo ya nje ya Iran tarehe 23 ilitoa taarifa ikisema, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio la kuweka vikwazo dhidi ya Iran ni kitendo haramu, hivyo haitatekeleza azimio hilo lisilo na ufanisi. Rais Ahmadinejad wa Iran tarehe 24 amesema watu wa Iran hawataogopa azimio la kuiwekea vikwazo nchi hiyo, Iran itaendelea na mpango wake wa nyuklia. Amesema nchi za magharibi zingeweza kuzungumza kwa amani na Iran yenye teknolojia ya nyuklia. Mjumbe wa kwanza wa mazungumzo ya nyuklia wa Iran Bwana Larijani tarehe 24 ametangaza kuwa, kuanzia siku hiyo Iran itaweka mashinepewa nyingine 3000 za kusafisha uranium nzito huko Nantaz. Bunge la Iran siku hiyo limezindua mchakato wa dharura, kuitaka serikali izingatie upya kufanya ushirikiano na shirika la nishati ya atomiki duniani, na kujitoa kutoka kwenye mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia.
Vyombo vya habari vya nchi za Ulaya vimeona kuwa, viongozi wa Iran wamelifanya jambo la kumiliki teknolojia ya nyuklia kama silaha nzuri ya kuzuia tishio la kijeshi na shinikizo la kisiasa kutoka nchi za magharibi, na kuzifanya rasilimali zake za mafuta kama karata muhimu, na kuchukulia kujiingiza kwenye matope kwa Marekani nchini Iraq kama ni fursa yake nzuri ya kuendeleza mpango wa nyuklia, pamoja na watu wa Iran waungane mkono kuhusu mpango wa nyuklia, hivyo Iran haitalegeza msimamo wake.
Naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bwana Nicholas Burns amesema watu wa Iran ni lazima wafahamu kuwa watatoa gharama kubwa kwa ajili ya kuendeleza mpango wa nyuklia, Marekani inatumai kuwa azimio No. 1737 litaweka mazingira kwa jumuiya ya kimataifa kuweka vikwazo vikali zaidi dhidi ya Iran.
Vyombo vya habari vya Ulaya vimedhihirisha kuwa, kupitishwa kwa azimio No.1737 kumefungua duru jipya la malumbano kati ya Iran na Marekani. Wakati Iran haitaki kutekeleza azimio No.1737, huenda Marekani itahimiza kuchukua hatua kali zaidi za kuweka vikwazo dhidi ya Iran. Jambo hilo si kama tu litazusha upinzani mkali kutoka kwa Iran, bali pia litaonesha tofauti za pande husika duniani.
|