Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-12-27 19:46:41    
Mapishi ya supu ya maini ya nguruwe

cri

Mahitaji:

Maini ya nguruwe gramu 50, doufu gramu 30, spinachi gramu 10, chumvi gramu 5, unga wa kuongeza ladha gramu 5, tangawizi gramu 5, vitunguu maji gramu 5.

Njia :

1. osha maini ya nguruwe, halafu uyakate yawe vipande. Kata doufu iwe vipande. Kata tangawizi na vitunguu maji viwe vipande.

2. chemsha maji kwenye sufuria, baada ya kuchemka tia vipande vya maini ya nguruwe, doufu, tangawizi na kiasi kidogo cha mafuta, baada ya kuchemka tena, endelea kuchemsha kwa dakika mbili, halafu tia spinachi, tia chumvi na unga wa kuongeza ladha. Korogakoroga tia vipande vya vitunguu maji. Mpaka hapa supu hiyo iko tayari kunywewa.

Idhaa ya Kiswahili 2006-12-27