Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-02 15:13:29    
Magari yenye hataza ya China yaoneshwa kwenye maonesho ya magari ya kimataifa ya Beijing

cri

Maonesho ya magari ya kimataifa ya mwaka 2006 ya Beijing yalifungwa tarehe 27 mwezi Desemba, vitu vilivyofuatiliwa sana na watu kwenye maonesho hayo ni magari mengi yenye hataza ya China. Magari hayo ya China yalichukua theluthi moja ya magari yote mapya yaliyooneshwa kwenye maonesho hayo, hali hiyo haikuwahi kuonekana kwenye maonesho ya magari yaliyofanyika hapa Beijing katika miaka iliyopita, tena teknolojia muhimu ya injini za magari ilipata mafanikio makubwa. Uvumbuzi wa China katika sekta ya uzalishaji magari ulifanya maonesho ya magari ya Beijing ya mwaka huu kuwa ya kupendeza zaidi.

Maonesho ya kimataifa ya magari ya Beijing yalianza mwaka 1990, ambayo ni maonesho ya kwanza kwa ukubwa nchini China. Huu ni mwaka wa kwanza, ambao kiwango cha maonesho ya magari ya Beijing kimeinuka na kufikia ngazi ya A ya duniani, makampuni makubwa ya kimataifa yalionesha magari yao kwenye maonesho ya Beijing yakitarajia kupanua masoko yao nchini China. Kampuni za magari za China, ambazo ziliweza tu kuonesha magari ya kiwango cha chini yenye hataza ya China kwenye maonesho, mwaka huu zilionesha magari yao ya kiwango cha juu.

Kwenye sehemu iliyoonesha magari ya kampuni ya magari ya Shanghai, ambayo ni moja ya kampuni tatu kubwa za China, mwandishi wetu wa habari aliona magari yenye uvumbuzi wa kampuni ya magari ya Shanghai yenyewe yanayojulikana kwa "Rongwi". Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya magari ya Shanghai Bw. Hu Mao alisema, kufanikiwa kuzalisha magari ya aina hiyo yanayotumia nishati za aina mbili, inaonesha kuwa kampuni ya magari ya Shanghai inajitahidi kuingia kwenye soko la magari yenye bei ya zaidi ya Yuan laki 2, vilevile inaonesha mafanikio ya mwanzo ya njia inayofuata ya kampuni ya magari ya Shanghai ya kununua kampuni kwenye nchi za nje na kuzalisha magari yenye hataza ya China.

"Tunashikilia kutotegemea nchi za nje kwa pande zote, lakini hatupingi nchi za nje kushiriki, kutokiuka kanuni za haki-miliki ya kiujuzi, bali ni kutumia ipasavyo rasilimali za duniani. Kwa kufuata njia hiyo, gharama tunazotumia ni ndogo, magari mapya yanazalishwa kwa haraka, tena tunaweza kupunguza pengo la ubora kati ya magari yetu na ya nchi za nje."

Mwandishi wetu wa habari alifahamishwa kuwa hivi sasa ni makampuni makubwa machache tu ya magari ya kimataifa, ambayo yanamiliki teknolojia ya kisasa ya kuzalisha magari yanayotumia nishati za aina mbili, tena yamezalisha kwa wingi magari ya aina hiyo. Hapo kabla uvumbuzi wa teknolojia ya injini inazotumia nishati za aina mbili ulisitasita, na hakukuwa na magari yanayotumia nishati za aina mbili yaliyooneshwa kwenye maonesho. Kwenye maonesho ya magari ya Beijing ya mwaka 2006 yalioneshwa magari ya aina 9 yenye hataza ya China yanayotumia nishati za aina mbili yakiwemo ya kampuni ya magari ya Shanghai. Hususan ni kuwa kampuni ya magari ya Shanghai imemaliza uvumbuzi wa magari yanayotumia nishati za aina mbili pamoja na uvumbuzi wa mfumo wa udhibiti wa elektroniki, na itazalisha kwa wingi magari ya aina hiyo katika siku chache zijazo.

Mbali na kujitahidi kuingia kwenye soko la magari ya kiwango cha juu, kuoneshwa kwa magari ya dizeli na magari yanayotumia nguvu ya betri yenye hataza ya China kunaonesha azma ya China ya kuvumbua magari ya aina mpya yenye hataza ya China. Wataalamu wa sekta ya magari wamesema, kutokana na kukabiliwa na upungufu wa nishati na uchafuzi kwa mazingira ya kimaumbile, kuzalisha magari yanayobana matumizi ya nishati na kuhifadhi mazingira ya asili ni njia ya maendeleo endelevu ya sekta ya uzalishaji wa magari.

Mhandisi wa kampuni ya magari ya umeme ya Donggeng Bw. Li Zhaoming alimweleza mwandishi wetu wa habari aina ya magari yanayobana matumizi ya petroli na kuchangia hifadhi ya mazingira.

"Magari hayo ni yenye injini ya petroli ya 1.6L, ingawa nguvu ya injini ni kilowati 78 tu, lakini tumeongeza mota moja ya kilowati 28, hivyo mfumo wa nguvu yake unaweza kufikia uwezo wa injini ya 2.0L, lakini matumizi ya petroli ya magari hayo ni sawa na injini ya 1.6L, au hata chini zaidi ya hapo."

Umaalumu mwingine wa magari yenye hataza ya China yaliyooneshwa kwenye maonesho ya kimataifa ya magari ya Beijing ni kuwa magari hayo yanatumia mafanikio ya uvumbuzi wa teknolojia muhimu ya magari. Kwa mfano injini mpya za kampuni ya magari ya Chery zimefikia kiwango cha juu duniani kwa kutumia teknolojia ya kuongeza nguvu ya mkandamizo kwa injini za turbo. Magari madogo ya kampuni ya Changan yanayojulikana kwa "Benben" yanapendwa na watu kutokana na kutumia injini za 1.3L zilizovumbuliwa na wahandisi wa China.

Aidha, kuoneshwa kwenye maonesho ya magari kwa aina kadhaa za magari ya sport kumeonesha hatua imara ilizopiga sekta ya uzalishaji magari ya China kwenye njia ya uvumbuzi wa China yenyewe. Magari ya sports ni yenye teknolojia ya kiwango cha juu zaidi, kwa kiwango fulani yanaonesha ubora na nguvu ya teknolojia ya viwanda vya magari. Kwenye maonesho ya magari ya mwaka huu, kampuni binafsi ya magari ya Geely, ilionesha magari ya aina yanayojulikana kama "Upepo", ambayo yana umbo la kama ndege za kivita zisizoweza kugunduliwa na rada, pamoja na uwezo wa kudhibiti gari kwa sauti ya maneno. Magari ya spots yanayojulikana kwa "Biyadi F8" ni aina pekee ya magari yenye kifuniko cha sehemu ya juu inayofunguka nchini China, ambayo inafunguliwa kwa sekunde 25 tu. Hivi sasa hapa duniani ni kampuni za magari ya BMW na Benz tu zina teknolojia ya aina hiyo. Naibu meneja wa idara ya mauzo ya kampuni ya magari ya Biyadi, Bw. Sun Xu alipoeleza sifa za magari ya aina hiyo, alisema,

"Ufunguo wa magari yetu hayo si wa kawaida, ufunguo wake ni aina ya saa inayovaliwa mkononi, mwenye gari anapokaribia gari lake, gari linaweza kumtambua na kufungua mlango wa gari, mwenye gari akibonyeza kitufe, gari linawaka."

Maonesho ya kimataifa ya magari ya Beijing yalianza kufanyika miaka 16 iliyopita, maonesho ya mwanzoni yalionesha magari maarufu ya duniani pamoja na magari yaliyozalishwa na viwanda vya ubia vilivyoko nchini China. Lakini mwaka huu, kampuni nyingi za magari za China zilishiriki kwenye maonesho ya magari, ambayo baadhi ya magari ya kampuni hizo yanasafirishwa kwenye nchi za Ulaya mashariki, Asia ya kusini mashariki, Asia magharibi na Amerika ya kusini.

Katika nusu ya kwanza ya mwaka 2006, ongezeko la magari madogo yenye hataza za China lilifikia 51%, wakati ongezeko la magari ya viwanda vya magari ya ubia nchini China lilikuwa kiasi cha 35%.

Idhaa ya kiswahili 2007-01-02