Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-02 14:58:35    
Mikwaruzano ya biashara ya kimataifa yapima uwezo wa China

cri

Wakati sekta za nguo na viatu za China zinapokumbwa na mikwaruzano ya biashara duniani na kutafuta ufumbuzi, sekta za chuma, chuma cha pua, mitambo na elektroniki pia zinakabiliwa vizuizi na kufanyiwa uchunguzi kuhusu kuuza bidhaa kwa bei ya chini, mikwaruzano ya kibiashara inayotokea mara kwa mara inapima uwezo wa serikali na kampuni za China.

Hivi sasa China inachukua nafasi ya kwanza kwa miaka 11 mfululizo kwa wingi wa uchunguzi uliofanyika kuhusu kuuza bidhaa katika nchi za nje kwa bei ya chini, ambapo moja kati ya matukio saba ya uchunguzi yaliyotokea kuhusu kuuza bidhaa kwa bei ya chini duniani lilikuwa ni la China. Takwimu mpya zilizotolewa na wizara ya biashara zinaonesha kuwa, katika miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka 2006, kulikuwa na nchi na sehemu zaidi ya 20, ambazo zilianzisha uchunguzi 70 juu ya China, ikiwa ni pamoja na kupinga kuuza bidhaa kwa bei ya chini na kutoa ruzuku, wingi wa uchunguzi wa aina hiyo haujawahi kutokea katika historia.

Mratibu wa taasisi ya ushirikiano wa kimataifa wa uchumi ya China Bw. Li Xinguang alisema: "Ukweli kuhusu China imekuwa nchi inayohusika na mikwaruzano mingi ya biashara duniani, bila shaka ni changamoto kali kwa China kubadilika kuwa nchi yenye uwezo mkubwa wa kibiashara kutoka nchi yenye shughuli nyingi za biashara."

Kabla ya miaka mitatu iliyopita, mtaalamu mmoja alisema China itaingia kwenye kipindi chenye mikwaruzano ya kibiashara duniani cha miaka 20. Katika mwaka 2006 utaratibu wa biashara wa pande nyingi ulipatwa na shida kubwa katika mazungumzo ya duru la Doha, vizuizi vya kibiashara duniani viliongezeka zaidi. China imekumbwa na mikwaruzano mikubwa ya kibiashara, sasa mikwaruzano hiyo imepanuka hadi kwenye bidhaa za aina nyingine kutoka bidhaa zinazozalishwa kwa kutumia nguvukazi nyingi, kutoka hatua ya kupinga kuuza bidhaa kwa bei ya chini hadi kuweka vizuizi vingi vya aina nyingi za kibiashara na kutoka katika nchi zilizoendelea hadi katika nchi zinazoendelea.

Kutoka televisheni za rangi, viatu na matunda ya strawberry hadi vipuri vya magari, nchi zilizoendelea zilipinga mara kwa mara China kuuza bidhaa kwa bei ya chini, zikijaribu kupunguza bidhaa zilizozalishwa na China kwenye soko la kimataifa. Mwandishi wetu wa habari alifahamishwa kuwa katika miaka miwili ijayo, Umoja wa Ulaya utatoza 16.5% ya kodi ya kupinga kuuza bidhaa kwa bei ya chini kwa viatu vilivyozalishwa nchini China, hatua ambayo itaathiri sana biashara hiyo ya viatu.

Kampuni ya Groupe Royer, ambayo ni ya mfanyabiashara mnunuzi nchini Ufaransa ilipohojiwa na mwandishi wetu wa habari ilisema, safari hii kiasi cha viatu inavyonunua kutoka China kimepungua kwa 85%, ambazo itavinunua kutoka nchi za Thailand na Malaysia.

Shinikizo la vizuizi kutoka nchi zinazoendelea kwa China si dogo ikilinganishwa na ya kutoka Ulaya na Marekani. India, moja ya nchi zilizochukua mara kwa mara hatua ya kupinga kuuza bidhaa kwa bei ya chini duniani, ilianzisha uchunguzi mara kwa mara kuhusu bidhaa zilizosafirishwa na China nchini India. Takwimu kutoka wizara ya biashara zinaonesha kuwa, toka tarehe 1 mwezi Januari hadi tarehe 31 mwezi Julai mwaka 2006, serikali ya India ilianzisha uchunguzi mara saba kuhusu bidhaa za kikemikali, plastiki, vipuri vya magari na CD tupu.

Mtaalamu wa ofisi ya utafiti wa sera ya wizara ya biashara ya China amesema, kanuni za kimsingi za China kuhusu mikwaruzano ya biashara ni kufanya uchambuzi kwa usahihi na kutafuta utatuzi wa kimsingi.

Idhaa ya kiswahili 2007-01-02