mwanzo mwa mwaka 2007 wizara ya ulinzi ya Marekani imethibitisha kuwa, idadi ya vifo vya askari wa Marekani nchini Iraq imefikia 3,000. Licha ya kusherehekea siku ya mwaka mpya, Wamarekani wanaonesha kuwa wamechoka na vita. Katika siku ya kwanza ya mwaka mpya wa 2007, mvua ilinyesha kwenye sehemu ya Washington. Ingawa wamarekani wengi bado walifurahia kuukaribisha mwaka mpya katika mkesha wa siku hiyo, lakini kivuli cha vita ya Iraq ni kama wingu jeusi angani, ambalo limefunika nyoyo za watu. Mjini Washington ambako mvua ilikuwa ikinyesha, mwandishi wetu wa habari kwanza alikutana na mhandisi mmoja wa teknolojia ya audio, ambaye anaona kuwa, lengo la Marekani kuanzisha vita ya Iraq si sahihi, na vifo vya askari 3,000 waliokuwepo nchini Iraq vinamsikitisha sana.
"idadi yoyote ya vifo vya askari ni msiba. Ninatarajia kuwa vifo na majeruhi ya askari wa Marekani nchini Iraq vingeweza kukomeshwa. Nafikiri hivi sasa serikali ya Bush inafikiri kuongeza idadi ya askari wa Marekani nchini Iraq, lakini mimi binafsi ningetaka wapunguze idadi ya askari wa Marekani nchini Iraq, kwani kuweko kwa askari wa jeshi la Marekani nchini Iraq ni kama uchokozi kwa watu wa huko, wala hakutaweza kuwapatia watu wa huko faida yoyote. Endapo jeshi la Marekani linabadilika kuwa nguvu ya uungaji mkono wala siyo nguvu ya mapambano, nitaliunga mkono, lakini hali hiyo ni vigumu kutokea."
Mieuel Elisa ni mmarekani mwenye asili ya Puerto Rico. Alisema matokeo ya jeshi la Marekani nchini Iraq yatakuwa kama ya jeshi la Marekani lililokuwa nchini Vietnam katika miaka ya 70 ya karne iliyopita.
"Watu wetu wengi walikufa huko, tena kulikuwa na wanawake wengi. Tumepoteza muda mwingi nchini Iraq, vita ya huko ni ya kikatili sana, siamini kama Marekani itapata ushindi nchini Iraq isipokuwa kupata baadhi ya rasilimali ya mafuta. Sasa huenda jeshi la Marekani litaendelea kukaa huko hadi siku moja, ambayo watalazimika kuondoka kama ilivyokuwa kwa askari wa Marekani walivyoondoka nchini Vietnam."
Rubani wa ndege ya abiria Bw. Charles Wood alipozungumzia idadi ya vifo vya askari wa jeshi la Marekani kuzidi 3,000, alikosoa sera za Marekani kuhusu Iraq.
"Naona idadi ya vifo vya askari kufikia 3,000 ni habari mbaya sana, ninaona kuwa jeshi la Marekani kuweko Iraq ni kosa, kwani jeshi la Marekani kamwe halitaweza kutimiza lengo lake. Jeshi la Marekani linatakiwa kurudi Marekani, serikali ya Marekani inatakiwa kufiri upya namna ya kutatua suala la Iraq."
Bw. Wood anaona, jeshi la Marekani linatakiwa kuondoka mara moja, wala siyo mwanzoni mwa mwaka 2008 kama ilivyopendekezwa na kikundi cha utafiti wa suala la Iraq, mbali na hayo ili kuzuia hali isizidi kuwa mbaya, jeshi la Marekani litaweza kuondoka Marekani taratibu kwa vipindi. Kuhusu jitihada ya rais George Bush za kurekebisha sera za Marekani kuhusu Iraq, Bw. Wood alisema sera mpya za rais Bush kuhusu Iraq zinatakiwa kuzingatia na kuendana na mwelekeo wa maendeleo ya Iraq na "kuvumiliana", Marekani isipachike azma yake juu ya Iraq.
"Tunapaswa kuwaelimisha, tuwapatie chakula, halafu tuwaache wachague njia yao kwa kutokana na utamaduni wao wenyewe. Hivi sasa maoni ya wamarekani wengi ni kuwa huwezi kuwalazimisha wengine wafanye mambo wasiyotaka, hata kama wamekubali kwa kulazimishwa, lakini hatimaye watarejea kwenye njia yao ya zamani."
Mbali na watu wa kawaida, hali ya kuchoka na vita imeenea hadi kwa askari wa jeshi la Marekani. Uchunguzi mpya unaonesha, katika jeshi la Marekani nchini Iraq ni 35% tu ya askari wanaounga mkono sera za rais Bush kuhusu Iraq, wakati 42% yao hawakubaliani na sera zake. Idadi ya askari wa Marekani wanaoamini Marekani itapata ushindi wa vita imepungua hadi 50% kwa hivi sasa kutoka 83% ya hapo zamani.
|