Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-03 20:58:47    
Profesa wa Kenya azungumzia juhudi za Kenya katika kuendeleza lugha ya Kiswahili

cri

Profesa Kimani Njogu ambaye ni mwenyekiti wa chama cha kiswahili cha Taifa yaani Chakita-Kenya na pia ni mwakilishi wa Kenya katika jumuia ya Afrika Mashariki katika ukuzaji wa kiswahili na pia katika uaandaji wa rasimu ya baraza la kiswahili la Afrika ya Mashariki.

Kabla ya miaka miwili iliyopita wapenzi wa kiswahili waliokuwa wanafanya utafiti kuhusu kiswahili, walipokuwa wanataka kuonana na Profesa Njogu walikuwa wanamfuata katika chuo Kikuu cha Kenyatta, kwa wakati huu wanaweza kumpata wapi ? Profesa Kimani Njogu alisema;

"Tangu miaka miwili iliyopita niliondoka katika idara ya kiswahili ya chuo kikuu cha Kenyatta na kujiunga na shirika la Afya la Afrika linalojulikana kama AHADI yaani Africa Health And Develepment International ambapo ni mwakilishi wa shirika hilo nchini Kenya"

Kazi kubwa ya shirika la AHADI ambalo ni shirika lisilo la kiserikali ni kujaribu kutumia sanaa, maandishi, na fasihi katika kukuza afya, pia shirika hilo linatumia vyomba vya habari ili kuendeleza afya ya jamii.

Kazi ambazo shirika la AHADI linazifanya zinalenga masuala ya Afya, na hadi sasa vitabu walivyoandika ni pamoja na kitabu cha Vibonzo, kitabu ambacho kinawasaidia vijana kujiepusha na matatizo ya kiafya kama vile ngono za mapema , utumiaji wa madawa ya kulevya, na kitabu hicho kinawalenga vijana wenye umri wa kati ya miaka 10 na 14. Kitabu hicho cha vibonzo kinaitwa Daraja na kimeandikwa kwa lugha ya kiingereza kwa sababu kimewalenga vijana kutoka katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.

Kitabu cha pili walichofanikiwa kukitoa ni kinachoelezea kazi za Shirika la AHADI zilizofanywa Bangkok nchini Thailand mwaka mmoja ulipita, kitabu hicho kinaitwa "Close to Home" kwa kiswahili ikimaanisha "karibu na nyumbani" Lengo la kitabu hicho ni kueleza kwamba tunapopambana na malazi ni lazima tulenge makazi ya watu, tusilenge nje ya makazi ya watu, tujaribu kuongea na wanajamii katika makazi yao. Katika kitabu hicho wameelezea unyanyepa kwa watu wenye virusi vya ukimwi, kimelezea matatizo ya Tiba, vyakula na matatizo mengi kuhusu udhibiti wa ugonjwa wa ukimwi.

Kitabu cha tatu walichoweza kuchapisha kinatokana na mradi walioweza kuutekeleza nchini Uganda,mradi ambao lengo lake lilikuwa ni kuweza kufanya kazi hasa na radio na magazeti ya Uganda ili kuzungumza na vijana, kitabu hicho kinasimuliza hatua zilizochukuliwa na shirika la AHADI katika kutekeleza mradi huo nchini Uganda na matatizo waliyokumbana nayo na namna walivyoweza kuyatatua, kujaribu kuwaeleza wengine wataopenda kufanya miradi kama hiyo jinsi wanaweza kutekeleza miradi hiyo bila ya matatizo.

Pia shirika la AHADI limetoa kanda ya video ambayo inazungumzia mbinu ambazo zitawasaidia vijana kujiepusha na matatizo, mkanda huo unaitwa closer to Home.

Licha ya mafunzo shirika la AHADI limeweza kuandaa warsha na semina nyingi, wameweza kuwapeleka wasanii takribani 60 kutoka Tanzania, Kenya na Uganda kwenda kwenye kongamano la kimataifa la Bangokok ambapo waliweza kushiriki vizuri sana kwa kuigiza, kutumbuiza na kuonyesha jinsi sanaa inavyoweza kuwasaidia wanajamii.Pia wameweza kuwapeleka wasanii na wafanyakazi wa afya katika mkutano wa kimataifa Abuja nchini Nigeria mwaka ulipita ambapo waliandaa warsha ya jinsi ya kupambana na ugonjwa wa ukimwi, na mwaka jana mwezi wa nane waliweza kuwapeleka watu wanane katika kongamano kimataifa la Toronto , nchini ili kuzungumzia mbinu mbalimbali zinazoweza kutumiwa kuwasaidia wanajamii kuweza kupambana na magonjwa, hayo ni baadhi ya mambo ya mambo waliyofanya.

Kwa hiyo shirika hili la AHADI linajaribu kupambana na ugonjwa wa ukimwi kwa kutumia mbinu zinazotilia sana mkazo sanaa, lugha na kuzingatia sana familia, na sio kuzingatia sana maisha ya mitaani,kujaribu kupanua fikra za wanasera na watu wa kawaida jinsi wanavyoweza kubadili maisha yao.