Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-05 14:28:28    
Mwaka muhimu kwa waziri mkuu wa Japan Bw. Shinzo Abe

cri

Januari mosi kwenye hotuba ya "mawazo yangu mwanzoni mwa mwaka mpya" waziri mkuu wa Japan Bw. Shinzo Abe alisisitiza, "katiba imekuwa na miaka 60, sasa ni wakati wa kubadilisha katiba hiyo ili iende na wakati". Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika tarehe 4 waziri mkuu huyo alisisitiza tena kuwa kurekebisha katiba ni lengo lake anapokuwa madarakani. Wakati mwaka 2007 unapoanza tu ameonesha tumaini lake hilo kubwa la kubadilisha katiba. Kwa hiyo mwaka huu utaamua kama waziri mkuu huyo ataweza au hatoweza kudumisha madaraka yake.

Mwaka 2006 waziri mkuu wa Japan Bw. Shinzo Abe alilazimisha bunge la nchi hiyo kupitisha azimio la kubadilisha "idara kuu ya ulinzi" kuwa wizara na sheria kuhusu jeshi la kujilinda na elimu, akitaka kuifanya Japan iwe nchi ya "kawaida". Vyombo vya habari vya Japan vimetangaza kuwa Bw. Shinzo Abe anatumai kuwa mkutano wa bunge utakaofanyika kuanzia tarehe 25 mwezi huu utaweze kupitisha "sheria ya wananchi kupiga kura" ambayo ni hatua ya lazima kwa ajili ya kurekebisha katiba na kutumai wananchi wajadili kuhusu marekebisho ya katiba.

Lakini mwaka huu sio mwaka mwepesi kwa Bw. Shinzo Abe kwani atakabiliwa na hali ya kushuka kwa kiasi cha uungaji mkono, uchaguzi wa madiwani utakaofanyika mwezi Aprili na uchaguzi wa baraza la juu utakaofanyika mwezi Julai. Vyombo vya habari vya Japan vinasema mwaka huu 2007 ni mwaka utakaoamua kama serikali ya Bw. Shinzo Abe inaweza kuendelea au la.

Kwanza, uchaguzi wa baraza la juu utakaofanyika mwezi Julai utakuwa mgumu, kama chama tawala kikishindwa kupata nafasi zaidi ya nusu basi Bw. Shinzo Abe atalazimika kuondoka madarakani. Kutokana na hali ya sasa ni vigumu kusema kama Bw. Shinzo Abe atashinda. Kiasi cha uungaji mkono kwa Bw. Shinzo Abe kiliwahi kufikia 63%, lakini hadi mwishoni mwa mwaka jana kiasi hicho kilipungua hadi kufikia 47%, na kashfa za chama chake na wabunge wa chama hicho zinatokea mara kwa mara. Kama viti vya chama chake tawala vikipungua chini ya nusu katika bunge maazimio yote pengine yatakataliwa na kupitiwa upya na baraza la chini, kwa hiyo shughuli za serikali hazitaweza kukwepa vikwazo.

Pili, uchaguzi wa madiwani utakaofanyika mwezi Aprili pia utakuwa mgumu, na hasa uchaguli wa kujaza viti katika miji ya Fukushima na Okinawa, kama chama chake kitashindwa kuchukua viti hivyo viwili kutakuwa na athari ya moja kwa moja kwa idadi ya zaidi ya nusu katika uchaguzi wa baraza la juu. Kwa hiyo mapambano makali hayawezi kuepukika.

Tatu, Maazimio ya mageuzi kuweza au kutoweza kupitishwa katika bunge ni changamoto kubwa kwa serikali ya Bw. Shinzo Abe, kwa sababu yanasiana na kiasi cha uungaji mkono kwa Bw. Shinzo Abe na kuathiri matokeo ya uchaguzi wa baraza la juu. Lakini kutokana na hali ya sasa pia kuna matatizo ya kupitisha maazimio hayo.

Licha ya matatizo ya nchini pia kuna matatizo ya nchi za nje. Baada ya Bw. Shinzo Abe kushika madaraka, uhusiano kati ya Japan na China umetengemaa kidogo, na hayo ni mafanikio yake, lakini pia anakabiliwa na shinikizo ambalo anaweza tu kupiga hatua za mbele bila kurudi nyuma katika uhusiano huo, lakini namna ya kuboresha uhusiano huo ni mtihani mwingine kwake. Aidha, namna ya kuendeleza uhudiano na nchi za Asia na Ulaya na huku akiendeleza uhusiano mzuri na Marekani, suala la nyuklia la peninsula ya Korea na tukio la Wajapani kutekwa nyara na Korea ya Kaskazini, mgogoro wa ardhi kati ya Japan na Russia, suala la kujiunga na Baraza la Uslama n.k. yote ni matatizo yanayomkabili Bw. Shnzo Abe.

Idhaa ya kiswahili 2007-01-05