Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-10 14:58:01    
Shule ya kimataifa iliyoanzishwa katika eneo la ustawishaji wa uchumi na teknolojia la Tianjin

cri
Eneo la ustawishaji wa uchumi na teknolojia la Binhai la Tianjin lililoanzishwa mwaka 1984 ni moja kati ya maeneo ya ustawishaji wa uchumi na teknolojia wa ngazi ya taifa yaliyoanzishwa mapema zaidi nchini China. Katika miaka 20 iliyopita sehemu hiyo imekuwa kituo cha maingiliano ya utamaduni kati ya China na nchi za nje, na watu wengi kutoka nchi za nje wanafanya kazi na kuishi huko pamoja na watoto wao. Ili kuwawezesha watoto hao wa watu wa nchi za nje kupata elimu nzuri, mwaka 1994 eneo hilo lilianzisha Shule ya kimataifa ya eneo la ustawishaji wa uchumi na teknolojia la Tianjin, ambayo inawaandikisha wanafunzi wa China na wanafunzi kutoka nchi za nje.

Shule hiyo yenye eneo la mita za mraba elfu 20 iko kwenye eneo la ustawishaji wa uchumi la Binhai mjini Tianjin, ambapo kuna maabara, maktaba, uwanja na jumba la michezo, na madarasa ya muziki na uchoraji ambayo yote yamefikia vigezo vya kimataifa, na yote hayo yameweka mazingira mazuri kwa wanafunzi. Mkuu wa shule hiyo Bw. Song Kuojun amesema madhumuni ya kuanzisha shule hiyo ni kuondoa matatizo ya kusoma kwa watoto wa watu kutoka nchi za nje wanaofanya kazi katika eneo la ustawishaji wa uchumi na teknolojia la Tianjin. Bw. Song Kuojun anasema:

"Tangu eneo hilo lianzishwe mwaka 1984, limewavutia watu wengi kutoka nchini na nchi za nje, na watu hao wanahitaji kutatua tatizo la shule kwa ajili ya watoto wao. Kutokana na hali hiyo mwaka 1993 eneo hilo liliamua kuanzisha shule hiyo."

Bw. Song Kuojun alisema kuwa uendeshaji wa shule ya kimataifa ya eneo la ustawishaji wa uchumi na teknolojia la Tianjin una umaalum wake pekee, shule hiyo ina sehemu mbili za elimu ya kimataifa na elimu ya China. Kwenye madarasa ya elimu ya kimataifa, wanafunzi wanatumia vitabu vinavyotumiwa katika nchi mbalimbali duniani, na mafunzo kwenye madarasa hayo yanatolewa kwa lugha ya kiingereza; na madarasa kwenye sehemu ya elimu ya China wanafunzi wanapewa mafunzo kwa lugha za kichina na kiingereza. Naibu mkurugenzi wa ofisi ya uongozi wa elimu kwenye shule hiyo ya kimataifa Bibi Cui Min alisema kuwa, shule hiyo inaweka mkazo katika kuendeleza uwezo wa wanafunzi. Alisema :

"Tulipoanzisha shule hiyo wazazi wa watoto na watu wa jamii walikuwa na wasiwasi na mashaka, lakini baada ya watoto wao kuja kusoma kwenye madarasa yetu, walifurahia njia hiyo ya kuwafundisha watoto."

Shule ya kimataifa ya eneo la ustawishaji wa uchumi na teknolojia la Tianjin inaendeshwa kwa kufuata utaratibu mpya wa usimamizi na kiwango cha kimataifa. Hivyo shule hiyo inafanya juhudi za kuongeza mawasiliano kati yake na idara za elimu za nchi mbalimbali, hadi sasa zimeanzisha mawasiliano na vyuo vya nchi mbalimbali zikiwemo Canada na Marekani. Mwanafunzi anayesoma katika shule hiyo Zhou Xiao alisema shule hiyo imempa fursa nzuri ya kujifunza kiingereza akisema:

"Naona kuwa umaalum wa shule hiyo ni kufundisha kwa lugha za kichina na kiingereza, katika shule hiyo wanafunzi wanaweza kupata elimu ya sekondari ya juu sawa na ile ya sekondari za juu nyingine nchini China, pia wanaweza kupata elimu katika mazingira iliyo sawasawa na yale ya elimu ya Australia, ambapo wanaweza kupata fursa za kutosha za kuongea kwa lugha ya kiingereza na walimu kutoka nchi za nje. Baada ya kupata masomo ya kiingereza kwa miaka miwili hadi mitatu katika shule hiyo, wengi kati ya wanafunzi waliohitimu kutoka shule hiyo wanaweza kuingia katika vyuo wanavyotaka kusoma nchini Australia, na kiwango chao cha kiingereza huwa kimefikia kipimo cha kuingia kwenye vyuo vikuu vya Australia."

Shule hiyo vilevile inaweka mkazo katika kukuza uwezo wa wanafunzi kwa sekta zote. Mwalimu kutoka Marekani Bw. Dan Hannen Starr anatoa mafunzo ya ujuzi wa kimaumbile kwenye shule hiyo, alisema:

"Ujuzi wa kimaumbile ni somo la kimsingi linalonahusu mambo mengi, somo hilo huwafurahisha watoto. Mimi hufanya majaribio madogo pamoja nao na watoto hufurahishwa nayo."

Katika Shule ya kimataifa ya eneo la ustawishaji wa uchumi ya Tianjin, walimu wanatilia manaani sana kutoa mafunzo kuhusu ufahamu na utumiaji wa ujuzi wa wananchi na kuwasaidia wanafunzi wapate vizuri zaidi ujuzi. Mwalimu kutoka Australia Bibi Linda anasema:

"Naona kuwa wanafunzi wa China wanasoma kwa bidii kubwa, ambao wana uwezo mkubwa zaidi wa kukumbuka ujuzi kutoka kwa vitabu kuliko kuutumia. Nafikiri hili ni tatizo kubwa linalowakabili baadhi ya wanafunzi wa China, lakini nafurahi sana kuwafundisha, kwani wanafunzi wa China husoma kwa bidii, wakienzi uwezo wao wa ufahamu watakuwa wanafunzi bora zaidi."

Shule hiyo pia inatoa mchango katika kuhimiza maingiliano ya kiutamaduni kati ya China na nchi za nje kwa kupitia mawasiliano kati ya wanafunzi wa China na wa nchi za nje. Mwanafunzi kutoka Alaska ya Marekani Patrick Barney aliwahi kuishi katika nchi nyingine, lakini anaipenda zaidi China, alisema:

"Napenda kujifunza utamaduni wa China, napenda mapishi ya kichina, napenda kushiriki sherehe ya harusi ya kichina, na pia napenda kutafiti tofauti kati ya sehemu mbalimbali nchini China. Wachina wengi ni wakarimu, hata baadhi yao hawajui kuongea kwa kiingireza, tunaweza kubadilishana maoni kwa lugha ya mikono. Shule yetu ni kama familia kubwa, na wanafunzi wananichukulia kama ni rafiki yao."

Mkuu wa shule hiyo Bw. Song Kuojun alisema, shule hiyo itaendelea kufuata kanuni ya kutupia macho siku za mbele, kufanya juhudi za kutoa mafunzo kwa wanafunzi wenye uwezo mkubwa na kuimarisha ushirikiano na mawasiliano kati yake na vyuo mbalimbali duniani, na kujifunza kutoka kwa maarifa duniani ili kutafuta mfumo wa elimu wa aina mpya na njia mpya ya kutoa mafunzo.

Idhaa ya Kiswahili 2006-01-10