Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-10 16:40:35    
China yafanya juhudi kuhimiza wananchi wapate huduma za kikimsingi za afya

cri

Umuhimu na mchango wa huduma za afya kwa maendeleo ya jamii na uchumi umekuwa mada muhimu iliyofuatiliwa na watu wengi kwenye kikao cha 6 cha mkutano wa 16 wa Chama cha Kikomunisti cha China uliofanyika hivi karibuni. Mkutano huo umeamua kuwa, kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kimsingi za afya ni wajibu muhimu wa serikali ya China. Katika siku za baadaye, China itaendelea kutatua matatizo ya wananchi ya kupata matibabu ili kusukuma mbele utaratibu mpya wa ushirikiano wa matibabu vijijini na kuendeleza huduma za matibabu mitaani katika miji ya China.

Utaratibu mpya wa ushirikiano wa matibabu vijijini ni utaratibu wa huduma za afya ulioanzishwa vijijini nchini China mwaka 2003. Lengo la utaratibu huo ni kuhakikisha wakulima wanapata huduma za kimsingi za afya. Utaratibu huo umeamua kuwa kila mkulima atoe yuan 10 kwa mwaka, na serikali za miji na serikali kuu ya China zatoe yuan 20 kwa ajili ya kila mkulima. Fedha hizo zinaunda mfuko wa huduma za afya. Wakati wakulima wanaoshiriki kwenye ushirikiano wa matibabu vijijini wanapoumwa, watapata malipo ya matibabu ya kiasi fulani.

Bw. Huang Jianguo ambaye ni mkulima wa mji wa Changshu mkoani Jiangsu, ni mmoja kati ya wakulima wanaonufaika na utaratibu huo. Kabla ya sikukuu ya mbara mwezi mwaka jana, alipata ugonjwa wa moyo na kufanyiwa operesheni mjini Shanghai. Gharama ya operesheni yake ilikuwa ni zaidi ya yuan elfu 50, ambayo ni karibu akiba yake yote. Wakati alipoumwa kaa aliokuwa anawafuga wote walikufa, hivyo familia yake haikuwa na mapato. Wakati familia yake ilipokata tamaa, ofisi ya ushirikiano wa matibabu ya kijiji chake ilimletea malipo ya matibabu yake. Bw. Huang alisema jambo hilo lilimfanya atambue umuhimu wa utaratibu wa ushirikiano wa matibabu vijijini. Alisema,

"Baba yangu alinisaidia kulipa yuan 20 niliposhiriki kwenye ushirikiano wa matibabu, wakati huo nilidhani kuwa nitaweza kulipiwa pesa chache tu za matibabu. Baada ya kufanyiwa operesheni ya moyo, mfuko wa ushirikiano wa matibabu ulinilipia karibu yuan elfu 20. Nilitumia fedha hizo kununua kilo elfu kadhaa chakula cha kaa na kaa wachanga. Fedha hizo zilinisaidia sana kuanzisha tena uzalishaji mali."

Kutokana na kutegemea fedha hizo, Bw. Huang alianzisha tena ufugaji wa kaa, katika mwaka huo alipata mapato zaidi ya yuan elfu 20, na amefanikiwa kutatua matatizo yake.

Utaratibu mpya wa ushirikiano wa matibabu vijijini umehakikisha wakulima wanapata huduma za kimsingi za matibabu. Hivi sasa utaratibu huo unatekelezwa katika asilimia 40 ya vijiji nchini China, na wakulima zaidi ya milioni 200 wananufaika na utaratibu huo. Bw. Wu Haizan ambaye ni mkulima wa mji wa Weihai mkoani Shandong anafurahishwa na utaratibu huo, na kuona kuwa utaratibu huo umepunguza mzigo kwa wakulima.

"Siku moja nilikwenda kuonana na madaktari, na nilitumia yuan 64. Lakini nililipiwa asilimia 30 ya gharama ya matibabu siku za baadaye. Ni rahisi kupata malipo hayo, ilinibidi nisubiri dakika moja au mbili tu."

Utaratibu mpya wa ushirikiano wa matibabu umesukuma mbele maendeleo ya huduma za afya vijijini. Wakati huo huo serikali ya China imetenga fedha nyingi zaidi kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu ya matibabu vijijini, sera kuhusu kutoa mafunzo kwa madakari vijijini na madaktari wa mijini kufanya kazi vijijini pia zimetolewa. Hatua hizo zimeboresha hali ya matibabu na afya vijijini.

China inawapatia wakazi wa mijini huduma za kimsingi za afya kwa kusukuma mbele maendeleo ya idara za matibabu za mitaani, yaani kujenga vituo vya huduma za afya vya mitaani ambavyo vinafanya kazi ya kutibu magonjwa ya kawaida na magonjwa ya muda mrefu. Kama wagonjwa hawawezi kutibiwa katika vituo hivyo wanakwenda hospitali kubwa.

Wakazi wa mijini wanaweza kufika kwenye vituo vya huduma za matibabu kwa kutembea kwa dakika 15 tu, hali hiyo imewapa wakazi wa mijini urahisi wa kupata matibabu. Mwandishi wetu wa habari alipofanya mahojiano katika mtaa mmoja mjini Beijing, wakazi wa huko walisema baada ya kituo cha afya cha mtaani kujengwa, imekuwa ni rahisi kwao kupata matibabu na wamenufaika na kituo hicho.

"Kabla ya kituo hicho kujengwa ilinibidi niende kwenye hospitali zilizoko mbali."

"Ingawa kituo hicho cha matibabu ni kidogo, lakini kina madaktari hodari."

Kazi ya vituo vya afya na matibabu vya mitaani ni kutibu magonjwa ya kawaida na magonjwa ya muda mrefu, wagonjwa ambao hawawezi kutibiwa katika vituo hivyo wanaweza kutibiwa katika hospitali kubwa. Aidha wagonjwa waliotibiwa katika hospitali kubwa wanapopona wanaweza kurudi nyumbani na kutibiwa katika vituo vya afya vya mitaani. Utaratibu huo unaweza kuboresha matumizi ya huduma za afya, kupunguza shinikizo kwa hospitali kubwa na kutatua matatizo ya kupata matibabu katika hospitali kubwa, pia unaweza kupunguza gharama za matibabu na kuwanufaisha wananchi. Vituo vya matibabu na afya vya mitaani pia vinaweza kutoa huduma za kimsingi za matibabu na afya nyumbani kwa wakazi, na kutoa huduma za afya kwa siku mfululizo, kwa mfano vinaweza kuweka kumbukumb za wagonjwa wa shinikizo kubwa la damu, na kufanya uchuguzi kila baada ya muda fulani.

Kikao cha 6 cha mkutano wa 16 wa Chama cha Kikomunisti cha China uliofanyika hivi karibuni kimetoa shabaha ya kujenga jamii yenye uwiano. Kuhakikisha wananchi kupata huduma za kimsingi za afya ni sehemu muhimu ya kutimiza shabaha ya kujenga jamii yenye masikilizano. Ni kazi kubwa kwa China ambayo ni nchi yenye idadi kubwa ya watu, kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za matibabu. Waziri wa afya wa China Bw. Gao Qiang alimwambia mwandishi wa habari kuwa, serikali ya China kwanza itatenga fedha nyingi zaidi kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kimsingi za afya, na baadaye kuinua kiwango cha huduma za afya hatua kwa hatua.

"Kazi muhimu ya kusukuma mbele maendeleo ya huduma za afya ni kusukuma mbele huduma za afya vijijini na mitaani, kuendeleza idara za afya kwenye ngazi ya shina, na kuwapatia wakazi huduma za kimsingi za afya zenye usalama na usawa, na baadaye kuendeleza idara kubwa za matibabu za kiwango cha juu kwenye kimsingi hiyo."

Idhaa ya Kiswahili 2007-01-10