Tarehe 8 helikopta za Marekani zilipiga mabomu dhidi ya watuhumiwa wa kundi la Al-Qaida walioko sehemu ya kusini ya Somalia zikasababisha watu kumi kadhaa kuuawa au kujeruhiwa, kati ya hao wengi ni askari wa vikosi vya makundi ya upinzani ya Somalia.
Tangu mwaka 1991 baada ya Somalia iingie katika hali ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, jeshi la Marekani liliwahi kutumwa nchini Somalia kama ni jeshi la kulinda amani. Mwaka 1993 askari 18 wa Marekani waliuawa mjini Mogadishu walipokuwa wakiwasaka wababe wa vita wa Somalia. Muda mfupi baada ya tukio hilo jeshi la Marekani lililazimika kuondoka kutoka Somalia na Umoja wa Mataifa pia uliacha juhudi za kulinda amani nchini humo, na vita vya wenyewe kwa wenyewe viliendelea hadi sasa. Sasa ni zaidi ya miaka kumi imepita tangu tukio la kuuawa kwa askari wa Marekani litokee, ni kwanini Marekani imepiga mabomu tena dhidi ya Somalia?
Somalia iko katika pembe ya Afrika ambayo ni muhimu kwa mkakati wa vita, na Marekani haijawahi kuacha kuigombea pembe hiyo, hasa katika miaka ya karibuni ambapo mafuta ya Sudan yamekuwa muhimu duniani. Wataalam wanakadiria kuwa, utajiri wa mafuta wa Sudan unachukua nafasi ya pili duniani, nyuma tu ya Saudi Arabia, na mafuta ya Sudan yanasafirishwa nje kupitia ghuba ya Aden, na Somalia iko kwenye upande wa kusini wa ghuba hiyo. Kuimarisha udhibiti wa sehemu hiyo ni hatua muhimu ya Marekani kuhakikisha usalama wake wa mafuta. Mwaka 2002 Marekani ilianza kupanga jeshi lake nchini Djibouti, ambayo ni nchi jirani ya Somalia. Vyombo vya habari vya Uingereza viliwahi kudokeza kuwa Marekani ilikuwa inasaidia kifedha makundi fulani ya Somalia kupitia shirika lake la ujasusi, ikulu ya Marekani haikukanusha wala kukubali habari hizo.
Pili katika mwaka mmoja uliopita, nguvu za kijeshi kati ya makundi tofauti pia zilikuwa na mabadiliko. Tangu mwezi Juni mwaka jana, vikosi vya Muungano wa Mahakama za Kiislamu vilitwaa sahemu nyingi, na katika muda wa nusu mwaka hivi vilishikilia maeneo mengi ikiwa ni pamoja na mji wa Mogadishu na vilidhibiti miji muhimu na bandari. Siasa na sera za Kundi la Muungano wa Mahakama za Kiislamu zinafanana na kundi la Taliban la Afghanistan. Hivi sasa ingawa vikosi vya Kundi la Muungano wa Mahakama za Kiislamu vimelazimika kukimbia, lakini kwa kiasi fulani bado vina msingi wa umma, kwa hiyo kufufuka kwa vikundi hivyo vyenye siasa kali za kidini kunawezekana wakati wowote na ni changamoto kubwa kwa Marekani kuidhibiti Somalia.
Tatu, kuingilia kati kwa Ethiopia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Somalia kumepunguza sana hatari kwa jeshi la Marekani nchini humo. Kwa kweli Marekani haina uwezo wa kutuma askari wengi nchini Somalia ingawa inataka kufanya hivyo. Kwa hiyo Marekani ilipaswa kuomba msaada wa Ethiopia ambayo ina uhusiano mkubwa na Somalia na huku ina uhusiano mzuri na Marekani. Mwezi Desemba mwaka jana kutokana kuungwa mkono na Marekani, Ethiopia ilijiingiza kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Somalia, na kutokana na uingiliaji wa Ethiopia hali ya vita ikawa nzuri kwa serikali ya mpito ya Somalia na katika muda wa nusu mwezi tu sehemu zilizopotezwa zimerudishwa, ukiwemo mji mkuu Mogadishu. Wakati huo Marekani ilipopiga mabomu dhidi ya Somalia inaweza kukwepa hatari ya kutuma askari wengi kwenye pembe hiyo ya Afrika na pia iliweza kutishia nguvu za kupinga Marekani na kuathiri hali ya Somalia.
Wachunguzi wanaona kuwa, kwa sababu Kundi la Muungano wa Mahakama za Kiislamu bado lina msingi fulani wa umma, na ili kutoikasirisha Saudi Arabia yenye uhusiano wa karibu na nguvu za kidini za Somalia, Marekani itatumia zaidi athari yake ya kisiasa badala ya nguvu za kijeshi.
Idhaa ya Kiswahili 2007-01-10
|