Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-11 19:56:02    
Rais George Bush wa Marekani atangaza marekebisho ya sera za Marekani kuhusu Iraq

cri

Tarehe 10 Rais Bush wa Marekani alitangaza kwa njia ya televisheni sera mpya za Marekani kuhusu Iraq ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya askari na kusaidia ukarabati wa Iraq, akitumai kuwa sera hizo mpya zitatuliza vurugu zinazoongezeka nchini humo. Kwenye hotuba hiyo ya dakika 20, Bw Bush alitangaza kuwa Marekani itaongeza askari elfu 20 nchini Iraq ili kusaidia jeshi la usalama la Iraq kulinda usalama. Alisema,

"Tunaongeza askari elfu 20 nchini Iraq, kati ya askari hayo brigedi tano zitatumwa kwenye mji wa Baghdad. Askari hao watashirikiana na askari wa Iraq katika mapambano."

Kwa mujibu wa mpango wake, kundi la kwanza la askari hao litaingia nchini Iraq kabla ya mwisho wa mwezi Januari. Ili sera mpya zitekelezwe, Rais Bush ataomba dola za Kimarekani bilioni 5.6 kwa ajili ya nyongeza ya askari katika ripoti yake ya bajeti itakayowasilishwa bungeni mwezi ujao, na dola za Kimarekani bilioni 1.2 zitatumika katika ukarabati wa Iraq, jumla ni dola za Kimarekani bilioni 6.8.

Kwenye hotuba Rais Bush alikiri makosa yake katika vita vya Iraq na kusema kuwa atawajibika kwa makosa hayo. Alisema,

"Juhudi zetu za kulinda usalama wa Baghdad zimeshindwa. Sababu ni mbili, moja ni kuwa hatuna majeshi ya kutosha kulinda usalama wa Baghdad; na wakati huo jeshi letu lilipotekeleza kazi yake liliingiliwa na mambo mengi ya siasa na madhehebu ya kidini, vitendo vya jeshi letu vilizuiliwa kwa kiasi kikubwa."

Rais Bush alisema majemadari wa Marekani wamejadili sana sera mpya ili kukwepa makosa ya zamani. Na pia alisema waziri mkuu wa Iraq amemhakikishia kuwa serikali ya Iraq haitavumilia tofauti za kisasa na migongano ya madhehebu ya kidini kuharibu harakati za jeshi la Marekani.

Vurugu za Iraq zimeleta shinikizo kubwa kwa serikali ya Marekani, kwenye hotuba Rais Bush kwa mara nyingine ameihimiza serikali ya Iraq itimize lengo lililowekwa na Marekani kuhusu usalama, siasa na uchumi katika muda maalum. Alisema,

"Nimewaambia waziri mkuu na viongozi wengine wa Iraq, ahadi za Marekani zina ukomo. Kama serikali ya Iraq haiwezi kutimiza ahadi zake, itapoteza uungaji mkono wa watu wa Marekani na watu wa Iraq."

Kadhalika Rais Bush alisema serikali ya Iraq inapaswa kuchukua madaraka ya usalama kwenye mikoa yote kabla ya mwezi Novemba.

Kutokana na kukabiliwa na upinzani kutoka chama cha Democrat cha Marekani kuhusu nyongeza ya askari, Rais Bush alionya kuwa kama jeshi la Marekani likiondoka Iraq serikali ya Iraq itaangushwa, na Iraq pengine itafarakana na kutokea hatari ya mauaji makubwa. Alisema,

"Matokeo hayo yatalilazimisha jeshi letu kukaa nchini Iraq kwa muda mrefu na litakabiliwa na maadui wa hatari kubwa zaidi. Ikiwa wakati huu tunaimarisha mshikamano na kuwasaidia watu wa Iraq kushinda mzunguko wa mauaji, itasaidia jeshi la Marekani kuondoka mapema kutoka Iraq."

Kauli ya kupinga Rais Bush kuongeza askari nchini Iraq ni kubwa. Kwa mujibu wa magazeti, wabunge wengi wa chama cha Democrat wanaona hatua hiyo itazamisha Marekani ndani zaidi ya matope ya vita vya Iraq. Kwa hiyo, sera hizo mpya za Rais Bush kuweza au kutoweza kuungwa mkono na bunge na wananchi wa Marekani na kutekelezwa vilivyo, bado haijulikani.

Idhaa ya Kiswahili 2006-01-11