Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-12 18:47:42    
Kujitahidi kujenga ukoo mkbuwa kuwa nufaishana pamoja na matokeo ya ushirikiano

cri

Mkutano wa 12 wa wakuu wa Umoja wa Asia ya kusini mashariki, Mkutano wa10 wa wakuu wa nchi 10 za Umoja wa Asia ya kusini na China, Japan na Korea ya kusini, Mkutano wa 10 wa wakuu wa nchi 10 za Umoja wa Asia ya kusini mashariki na China pamoja na Mkutano wa pili wa wakuu wa nchi 16 za Asia ya mashariki itafanyika huko Cebu, katikati ya Philippines kuanzia tarehe 13 hadi 15 mwezi huu.

Mkutano wa 12 wa wakuu wa Umoja wa Asia ya kusini mashariki utafanyika kwanza, ambapo viongozi wa nchi 10 za Umoja wa Asia ya kusini mashariki watajadili kuhusu kubuni katiba ya umoja huo, biashara na uwekezaji, kuimarisha ushirikiano katika mapambano dhidi ya ugaidi, mazungumzo ya pande 6 ya suala la nyuklia la peninsula ya Korea na masuala mengine makubwa yanayohusiana na usalama wa sehemu hiyo na maendeleo ya siku za baadaye. Mkurugenzi wa ofisi ya Taasisi ya utafiti wa uhusiano wa kimataifa ya China Bwana Zhai Kun alisema:

"Katiba ya Umoja wa Asia ya kusini mashariki" ni kanuni itakayotungwa kwa ajili ya maendeleo ya muda mrefu ya umoja huo katika siku za usoni. Nchi 10 za Umoja wa Asia ya kusini mashariki ziliamua pamoja kuanzia mwaka 2003 kuwa, zitajenga umoja huo kuwa umoja unaolingana na Umoja wa Ulaya ambao utakuwa na sehemu tatu, yaani umoja wa uchumi, umoja wa usalama na umoja wa kijamii na utamaduni. Zikitaka kujenga umoja kama huo, nchi hizo zinatakiwa kuwa na ushirikiano wa karibu zaidi na kuwa mshikamano mkubwa zaidi, ili kutoa nguvu za pamoja katika kukabiliana na changamoto na matishio ya aina mbalimbali.

Katika Mkutano wa 10 wa wakuu wa nchi 10 za Umoja wa Asia ya kusini mashariki pamoja na nchi tatu za China, Japan na Korea ya kusini pamoja na Mkutano wa 10 wa nchi 10 za Umoja wa Asia ya kusini mashariki pamoja na nchi ya China, China na Umoja wa Asia ya kusini mashariki zitajadili namna pande mbili zitakavyotekeleza maoni ya pamoja yaliyofikiwa mwezi Novemba mwaka jana, ambapo China itatoa mapendekezo halisi kadha wa kadha, ili kuimarisha na kuinua zaidi uhusiano wa kimkakati na kiwenzi kati ya China na Umoja wa Asia ya kusini mashariki. Bwana Zhai Kun anaona kuwa, kwenye mikutano hiyo China na Umoja wa Asia ya kusini mashariki zitaendelea na juhudi za kuzihimiza China na Umoja wa Asia ya kusini mashariki zianzishe eneo la biashara huria. Akisema:

Kuanzisha eneo hilo la biashara huria, tunaziwezesha bidhaa nyingi zaidi za Umoja wa Asia ya kusini mashariki ziingie kwenye soko la China, ambapo uwekezaji wa China mwingi zaidi pia utaingia kwenye nchi za Asia ya kusini mashariki; kwa nchi za Asia ya kusini mashariki, nchi hizo zinatakiwa kukabiliana na hatari za aina mbalimbali kutokana na utandawazi wa uchumi duniani, pia zinataka kutafuta soko jipya na chanzo cha mitaji, basi China itakuwa mwezi wao mzuri. Kama China na nchi za Umoja wa Asia ya kusini mashariki zitatangulia kuanzisha eneo la biashara huria, basi zitaweza kuhimiza ujenzi wa eneo la biashara huria kati ya Umoja wa Asia ya kusini mashariki na Korea ya kusini, na kati ya umoja huo na Japan, ili kusaidia maendeleo ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi za kanda ya Asia ya mashariki.

Na Bwana Zhai Kun amesema, Mkutano wa wakuu wa nchi 10 za Umoja wa Asia ya kusini mashariki pamoja na nchi tatu za China, Japan na Korea ya kusini ni utaratibu halisi kuliko Mkutano wa wakuu wa nchi 16 za Asia ya mashariki, kwani hata kama ushirikiano kati ya nchi za Asia ya mashariki utafanyika kwa namna gani, bado unawataka wakuu wa nchi za Asia ya mashariki wazingatie kwa makini zaidi ili kuthibitisha mwelekeo wa ushirikiano huo.

Idhaa ya Kiswahili 2007-01-12