Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-15 14:56:06    
Msomi mashuhuri wa China Yu Qiuyu

cri

Bw. Yu Qiuyu aliwahi kuwa kijana kabisa kati ya maprofesa wa sanaa na sayansi za jamii nchini China, aliwahi kuwa mkuu wa chuo kikuu na baadaye alikuwa mwandishi anayejitegemea. Amewahi kutembelea sehemu nyingi zenye kumbukumbu za kihistoria na kitabu alichoandika mkusanyiko wa makala zinazoeleza hisia zake kuhusu matembezi yake ni kitabu kinachonunuliwa kwa wingi kabisa kati ya vitabu vinavyosomwa sana nchini China. Mwandishi huyo wa vitabu pia anazungumzwa kutokana na maoni yake ya kukosoa moja kwa moja hali ya sasa ya utamaduni nchini China.

Bw. Yu Qiuyu alizaliwa mwaka 1946 katika kijiji kimoja cha mlimani mkoani Zhejiang, mashariki mwa China. Alipokuwa na umri wa miaka saba kutokana na kusaidiwa na mama yake, alianza kuwasaidia wenyeji wenzake ambao hawakujua kusoma na kuandika kuandika barua na kusaidia wafanyabiashara kufanya uhasibu. Mazoezi hayo yalimwezesha Yu Qiuyu kupata nafasi ya kwanza katika mashindano ya kuandika insha na nafasi ya saba katika mashindano ya hisabati kabla ya kwenda kusoma katika mji wa Shanghai, ufanisi huo ulimwezesha kuondoka kijijini na kwenda kusoma katika mji mkubwa. Alipokumbuka miaka yake hiyo alisema.

"Nilipokuwa na umri wa miaka saba nilianza kuwasaidia wenyeji wenzangu kuandika barua na kufanya uhasibu wa biashara zao, ingawa nilikosa wakati wangu wa kucheza baada ya kutoka shuleni, lakini ilinisaidia sana kielimu. Namshukuru mama yangu, kwa sababu alinifahamisha kuwa utamaduni ni aina ya majukumu, niwe mtu wa kutoa mchango na nisidai chochote kutoka kwenye ardhi hiyo, na nifanye kitu katika maisha yangu na nipige hatua na hatua."

Alipokuwa mtoto maisha yalikuwa magumu, lakini maisha hayo yalimfanya awe jasri wa kukabiliana moja kwa moja na maisha yasiyo ya kawaida hapo baadaye. Baada ya kuhitimu masomo ya fasihi katika Chuo Kikuu cha Tamthilia alianza kushabikia utamaduni wa China na wa dunia. Mwaka 1968 kutokana na ugonjwa alirudi kwenye kijiji kimoja cha mlimani mkoani Zhejiang na kupumzika. Huko vijijini kulikuwa na maktaba moja, alitumia miaka kadhaa ya kuhuisha afya yake kumaliza kusoma vitabu vyote vya kale vya China, baadaye alirudi mjini Shanghai. Katika chumba chake chenye eneo la mita 13 za mraba mjini Shanghai alimaliza kusoma vitabu vyote alivyoweza kupata kwa kununua au kwa kuazima, vilivyoandikwa na wanafikra na wanafalsafa wa nchi za nje. Kutokana na kusoma vitabu vingi alichapisha vitabu vingi kuhusu nadharia ya tamthilia na sanaa ikiwa ni pamoja na vitabu vya "Historia ya Tamthilia", "Historia ya Tamthilia ya China". Mwaka 1985 alikuwa mtu wa kushangaza baada ya kuchaguliwa kuwa profesa kijana kabisa katika China bara. Mwaka 1986 alichaguliwa kuwa mkuu wa Chuo Kikuu cha Tamthilia cha Shanghai kutokana kuandika vitabu vingi vya taaluma. Katika miaka yake ya uongozi, mwanzoni alikuwa hana furaha na uongozi huo, lakini baadaye aligundua kwamba kazi yake inampatia manufaa mengi. Alisema,

"Katika miaka kadhaa ya kufanya kazi ya uongozi, nilifahamu kwamba nina majukumu kwa watu nisiowafahamu na wasio na uhusiano wowote na familia yangu, na ufahamu huo unanisaidia sana kufanya kazi yangu ya sasa. Baada ya kushika uongozi nilielewa matatizo ya kijamii yanayoikabili China, na katika fani ya utamaduni lazima niwe mtu wa kuwajibika zaidi. Ingawa nilikosa wakati wa kusoma na badala yake kuwa na mikutano mingi, ingawa nilikosa wakati wa kuandika na kusoma vitabu na badala yake nilikuwa naandika ripoti nyingi za kazi, lakini kwa kweli niliona kazi yangu ilikuwa muhimu sana."

Bw. Yu Qiuyu alisema, safari yake ya kupanda ngazi ya wadhifa ilikuwa shwari, lakini rohoni mwake aliona kama kuna nguvu fulani za kumsukuma azingatie zaidi utamaduni wa China. Aliona utajiri wa China ni utamaduni wake, na kitu kilichopotea ni utamaduni wake vile vile. Kwa hiyo alijiuzulu kazi yake ya kiserikali na kuanza kutafuta kumbukumbu za utamaduni uliopotea nchini China na duniani. Alisema,

"Naridhika na chaguo langu, yaani kutafuta kumbukumbu za utamaduni uliowahi kung'ara katika zama za kale na kuandika hisia zangu kuhusu utamaduni huo na kuathiri Wachina na wengine duniani."

Alitembelea kumbukumbuu zote za utamaduni nchini China kisha aliandika kitabu chake cha "Safari ya Utamaduni". Kitabu hicho kinanunuliwa sana hadi sasa.

Mwwanzoni mwa karne hii Bw. Yu Qiuli alitumaini kwenda kwenye vyanzo vikuu vitatu vya ustaarabu duniani. Mwaka 1999 hadi 2000 alifuatana na waandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Phoenix cha Hong Kong alitembelea nchi zaidi ya kumi za Ugiriki, Misri, Israel, India na nchi nyingine na aliandika kitabu chake cha "Maajabu ya Miaka Elfu Moja" ambacho aliandika mambo aliyoona katika safari yake na maoni yake ya kina kuhusu kumbukumbu alizoziona. Kwa miezi sita alitembelea miji 97 ya nchi 26 na aliandika kitabu chake cha "Msafiri Asiyesimama". Mambo aliyoona yalimfanya atafakari zaidi kuhusu utamaduni wa China. Alisema,

"Bila kulinganisha na utamaduni wa nchi nyingine, siwezi kufahamu utamaduni mkubwa wa China. Nilitembelea miji 97 ya Ulaya nimefahamu nini sifa za utamaduni wetu na nini ni dosari zake, kwa hiyo kwa jumla nilikamilisha fikra yangu kuhusu utamaduni wa China."

Mwazoni mwa mwaka huu, kituo cha televisheni cha Phoenix kilianzisha kipindi cha mazungumzo ya Yu Qiuli kuhusu utamaduni. Kipindi hicho kilimfurahisha kwa kuweza kueleza fikra zake kuhusu matukio, na watu wa zamani mashuhuri. Alisema,

"Utamaduni wa China umeweza kuishi miaka elfu kadhaa, lakini nini siri yake ya kuishi maisha marefu na nini dosari yake katika maisha hayo marefu? Na niwafahamishe watu kwa njia gani ili waelewe kirahisi?"

Bw. Yu Qiuyu alisema, anatofautiana na wasomi wengine wa China, yeye aliunganisha taaluma na hisia zake alizopata mbele ya kumbukumbu halisi. Hivi sasa anashiriki katika vipindi vingi vya televisheni kutoa mihadhara na kueleza ufahamu wake kuhusu utamaduni, kutokana na hayo alisababisha mazungumzo ambayo kwa kuwa profesa anafaa kufundisha darasani au awe mtu anayeshiriki kwenye vipindi vya televisheni. Lakini kwa vyovyote vile amewaelimisha wananchi wenzake kuhusu utamaduni wa China na wa dunia.

Idhaa ya kiswahili 2007-01-15