Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-15 19:30:30    
Ziara ya mara ya kwanza ya Rais wa Iraq nchini Syria yafuatiliwa na watu

cri

Rais Jalal Talabani wa Iraq tarehe 14 Januari alifika Damascus kufanya ziara rasmi nchini Syria ambayo ni nchi jirani ya Iraq. Hii ni mara ya kwanza kwa rais Talabani kufanya ziara nchini humo tangu nchi hizo mbili zirudishe uhusiano wa kibalozi mwezi Novemba mwaka jana, pia ni ziara ya kwanza ya rais wa Iraq nchini Syria tangu miaka 27 iliyopita.

Siku hiyo Rais Talabani na Rais Bashar al Assad na viongozi wengine wa serikali ya Syria walifanya mazungumzo ambapo rais Talabani alisema, nchi mbili za Iraq na Syria zimedhamiria kujenga uhusiano mzuri wa pande hizo mbili, na kuanzisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kama vile kwenye sekta ya mafuta, ili kuleta manufaa kwa wananchi wa nchi hizo mbili. Habari zinasema wakati wa ziara hiyo, pande mbili pia zitasaini makubaliano mbalimbali kuhusu usalama na biashara. Ofisi ya rais wa Iraq siku hiyo ilitoa taarifa ikisema, madhumuni ya ziara hiyo ya Rais Talabani ni kutathimini na kuimarisha uhusiano kati ya Iraq na Syria, na hii inalingana na maslahi ya nchi hizo mbili.

Vyombo vya habari vinaona kuwa ziara hiyo ya rais Talabani inafanyika wakati ambapo rais George Bush wa Marekani alitangaza sera mpya kwa Iraq hivi karibuni na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Condoleezza Rice anafanya ziara huku na huko kwenye sehemu ya mashariki ya kati. Ndiyo maana ziara ya rais Talabani nchini Syria inafuatiliwa sana na watu.

Kama inavyofahamika kwa wengi sera mpya za Marekani kwa Iraq alizotangaza rais Bush tarehe 10 Januari si kama tu hazikupokea pendekezo la "kikundi cha utafiti wa suala la Iraq" cha Bunge la taifa, ili kutafuta misaada ya Syria na Iran kuhusu utatuzi wa suala la Iraq, bali ziliendelea kuzilaani Syria na Iran kuunga mkono shughuli za makundi yanayoipinga Marekani nchini Iraq, na kuruhusu kimyakimya watu wenye silaha wa nchi za nje wajipenyeze kuingia Iraq kutoka kwenye nchi zao. Rais Bush alisema jeshi la Marekani nchini Iraq litachukua hatua za kutokomeza kabisa uungaji mkono wa Syria na Iran kwa watu wenye silaha wanaoipinga Marekani nchini Iraq, na kuteketeza mfumo wa kusafirisha silaha na kutoa mafunzo kwa watu wenye silaha nchini Iraq. Maneno hayo yanamaana kuwa, Marekani bado inaunga mkono serikali ya Iraq kuchukua sera za uhasama dhidi ya Syria na Iran. Hivyo wachambuzi kadhaa wanaona kuwa, ziara ya rais Talabani nchini Syria inayofanyika katika hali hiyo inataka kuonesha kuwa kuhusu namna ya kushughulikia uhusiano wa pande mbili mbili kati ya Iraq na Syria na Iran, Iraq inataka kuweka umbali wa kiasi fulani kati yake na Marekani. Kwa Iraq kuboresha uhusiano kati yake na nchi jirani muhimu Syria na Iran, kunasaidia kupunguza migogoro ya kimabavu nchini Iraq, na kusaidia kulinda usalama na utulivu wa Iraq. Mbunge maarufu wa Iraq ambaye ni mkurd Bwana Mahmaoud Othman tarehe 14 alisema, maslahi ya Iraq na Marekani ni tofauti, hali ya uhasama kati ya Marekani, Syria na Iran haisaidii kuboresha hali ya usalama wa Iraq.

Hali halisi ni kwamba madhumuni makubwa ya ziara hiyo ya rais Talabani nchini Syria ni kujadili mambo mengi kuhusu usalama wa mipaka kati ya Iraq na Syria, na kuchukua hatua za kuwazuia watu wenye silaha wasijipenyeze Iraq kwa kuvuka mpaka wa Syria, ili kukatiza njia ya kusafirisha silaha na watu wenye silaha kutoka nje ya Iraq. Ziara ya rais Talabani imeonesha kuwa Iraq inafanya juhudi za kuboresha na kuimarisha uhusiano na nchi jirani zake, ili kujipatia uungaji mkono na misaada kutoka kwenye nchi nyingi zaidi kwa kudhibiti shughuli za kimabavu nchini Iraq, hii hakika itasaidia juhudi za serikali ya Iraq za kulinda usalama na utulivu wa nchi hiyo.