Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-19 16:38:47    
Utulivu na maendeleo ya Afrika yasukuma mbele ushirikiano kati ya China na Afrika

cri

Chini ya juhudi za pamoja na utoaji misaada wa jumuiya ya kimataifa, nchi za Afrika zilipata maendeleo makubwa katika sekta za siasa, uchumi na jamii. Na maendeleo ya nchi za Afrika yameleta fursa mpya kwa ushirikiano uliokuwepo kati ya China na Afrika.

Katika historia, bara la Afrika lilikumbwa na vurugu za kivita kwa muda mrefu kutokana na migogoro ya kikabila, kidini na ardhi, hali hiyo iliwahi kuvutia ufuatiliaji mkubwa wa jumuiya ya kimataifa. Hivi sasa nchi za Afrika zimevutia tena uangalifu wa jumuiya ya kimataifa kutokana na maendeleo yake ya kiuchumi na mustakabali mzuri wa kuwekewa vitegauchumi.

Baada ya Angola kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 27 mwaka 2002, pande mbili za kaskazini na kusini za Sudan kusaini makubaliano ya amani mwaka 2004, nchi za Afrika mwaka jana zilipata maendeleo mengine kama vile jeshi la upinzani la Uganda the Lord' Resistance Army lilisaini makubaliano ya kusimamisha hali ya uadui na serikali, na kufanyika kwa mafanikio kwa uchaguzi mkuu wa kwanza nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tangu ipate uhuru kwa miaka 40. Ingawa baadhi ya nchi za Afrika bado zinakumbwa na hali ya wasiwasi, lakini zinashughulikia kuleta amani ya pande zote zikishirikiana na jumuiya ya kimataifa.

Kutokana na kutimiza amani katika nchi nyingi za Afrika, pamoja na kupanda kwa bei za mafuta na rasilimali nyingine, nchi za Afrika ziko katika kipindi kizuri cha kujiendeleza. Katika miaka ya karibuni, wastani wa ongezeko la wastani la uchumi wa Afrika umefika asilimia 5, mwaka 2005 ongezeko hilo lilifikia asilimia 5.5, ambalo ni kubwa kabisa katika miaka 30 iliyopita barani Afrika, hata lilizidi kiwango cha ongezeko la wastani duniani. Ripoti ya mwelekeo wa uchumi duniani uliotolewa mwezi Septemba mwaka jana na shirika la fedha duniani IFM imekadiria kuwa, mwaka 2006 ongezeko la uchumi wa bara la Afrika litakuwa asilimia 5.4, ambapo ongezeko la uchumi wa nchi za kusini mwa Afrika litafikia asilimia 6, na nchi nane zinazozalisha mafuta zilizoko kusini mwa Sahara ikiwemo Nigeria litafikia au kuzidi asilimia 10, miongoni mwa nchi hizo nane, ongezeko la uchumi la Angola litafikia asilimia 25.

Usitawi na mustakabali mzuri wa uchumi wa nchi za Afrika umevutia uwekezaji mwingi wa nchi za nje. Ripoti ya mwelekeo wa uchumi duniani imesema, katika miaka 20 ya mwisho ya karne iliyopita, uwekezaji wa moja kwa moja wa nchi za nje katika bara zima la Afrika ulikuwa dola za kimarekani bilioni kadhaa tu kwa mwaka, mwaka 2004 thamani ya uwekezaji wa nchi za nje barani Afrika ilifikia dola za kimarekani bilioni 18, na ilipofika mwaka 2005 takwimu hiyo ilifikia dola za kimarekani bilioni 30. Vitegauchumi vingi kutoka nchi za nje vimehimiza ongezeko la kasi la uchumi barani Afrika.

Nchi za Afrika pia imepata maendeleo dhahiri ya kijamii. Ripoti kuhusu takwimu za maendeleo ya Afrika ya mwaka 2006 iliyotolewa na benki ya dunia mwanzoni mwa mwezi Novemba mwaka 2006 imesema, nchi nyingi za Afrika zikiwemo Senegal, Msumbiji, Buki Nafaso, Cameroon, Uganda na Ghana zilikuwa zimepata maendeleo mazuri katika kuwasaidia wananchi kuondokana na umaskini. Nchi hizo huenda zitaweza kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa ya kupunguza nusu ya idadi ya watu maskini ifikapo mwaka 2015. Ripoti hiyo imedhihirisha hasa mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya jamii, kama vile kiasi cha watoto wanaoenda kusoma shuleni imeongezeka kwa kiwango kikubwa, idadi ya watu wanaoambukizwa virusi vya ukimwi na idadi ya watoto wachanga wanaokufa imeanza kupungua, na hali ya kukosa usawa kati ya wanawake na wanaume imeboreshwa. Naibu mkuu wa benki ya dunia anayeshughulikia mambo ya Afrika Bwana Gebin Nanka alisema kuwa, Afrika ya hivi sasa ni bara linalojiendeleza kwa bidii, nchi mbalimbali za Afrika zimepata maendeleo dhahiri katika sekta za afya, elimu, biashara na kupunguza umaskini.

Kutulia kwa hali ya jumla ya Afrika na kuendeleza kwa uchumi wa Afrika kumeweka mazingira mazuri ya kuimarisha ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Afrika. Nchi za Afrika zinatilia maanani kujifunza uzoefu China ilioupata katika kujiendeleza, na kutunga sera za kuelekea upande wa mashariki, katika miaka ya karibuni, nchi za Afrika zimetokea tena hali ya kupenda China. Nchi za Afrika ni marafiki wakubwa wa China, ni sehemu muhimu ya mkakati wa China wa kuelekea nje, mkutano wa wakuu wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwezi Novemba mwaka jana umetia uhai mpya kwa ushirikiano huo. Bila shaka maendeleo ya nchi za Afrika yatahimiza ushirikiano kati ya China na Afrika uendelezwe kwa kina na pana zaidi.

Idhaa ya kiswahili 2007-01-19