Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-19 16:37:25    
Wachina waishio barani Afrika

cri

Katika miaka ya karibuni, China imetoa misaada ya kujenga miradi 720 kwa nchi 49 za Afrika, na kusaini mikataba ujenzi wa miradi 58 ya mikopo nafuu katika nchi 26 za Afrika, ili kutekeleza ujenzi wa miradi hiyo, serikali ya China imewatuma wachina wengi katika nchi za Afrika, wachina hao wametoa mchango mkubwa kwa ujenzi wan chi za Afrika. Mbali na wafanyakazi wa China waliotumwa na serikali ya China katika nchi za Afrika, bado kuna wafanyabiashara binafsi wanaoendesha shughuli mbalimbali katika nchi za Afrika kama vile mikahawa, maduka, zahanati, na makampuni ya aina mbalimbali. Wachina hao waisho katika nchi za Afrika wamekuwa daraja la kuunganisha urafiki kati ya China na Afrika. Katika kipindi hiki cha leo tunawaelezea hadithi za baadhi ya wachina waishio barani Afrika.

Bwana Han Jun ni mzaliwa wa Shanghai, ambao ni mji mkubwa kabisa nchini China, alifika nchini Kenya kabla ya miaka 13 iliyopita, Aliwahi kufungua duka la kuuzia bidhaa zilizotengenezwa nchini China, kuendesha mkahawa wa kichina huko Nairobi. Baada ya Kenya kuthibitishwa kuwa nchi inayoweza kuwapokea watalii wa China, aliacha shughuli nyingine na kusajili kampuni ya utalii ili kuwapokea watalii wa China huko Kenya.

Bwana Han Jun alisema, wakati alipofika nchini Kenya hakuna wachina wengi waliofanya biashara huko, lakini hivi sasa idadi ya wachina waishio nchini Kenya imefikia elfu kadhaa, wenyeji wa huko wamefahamu zaidi na zaidi kuhusu mambo ya China. Hivi sasa kuna makampuni zaidi ya 200 yaliyowekezwa na wafanyabiashara wa China, makampuni hayo yametoa nafasi nyingi za ajira kwa wenyeji wa huko. Bwana Han Jun alisema, wenyeji wa Kenya wanapenda kutafuta kazi katika makampuni yaliyowekezwa na nchi za nje, na makampuni ya China yanapendwa zaidi kutokana na mshahara mkubwa na kuwatendea vizuri wafanyakazi wa kienyeji.

Bw. Han Jun ni mkuu wa shirikisho la wachina waishio nchini Kenya, hivyo licha ya shughuli zake za kibiashara, yeye anatumia wakati mwingi kushughulikia mambo ya shirikisho na wachina wengine waliokumbwa na matatizo ya aina mbalimbali. Kutokana na mchango aliofanya, alikuwa ameteuliwa mara nyingi kuwa mjumbe wa wachina waishio nchini Kenya kushiriki katika mkutano wa wachina waishio nchi za nje wa China unaofanyika mara moja kwa mwaka.

Bw. Xu Hui ana umri wa miaka 37 mwaka huu, lakini ameishi nchini Kenya kwa miaka zaidi ya 10. Baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu alipata fursa ya kufanya kazi nchini Kenya, baada ya kumaliza zamu yake akaamua kubaki na kuanzisha kampuni yake nchini Kenya inayotengeneza televisheni.

Bw. Xu Hui alijumuisha kuwa, Kenya ni nchi nzuri kuwekezwa vitega uchumi kutokana na hali tulivu ya kisiasa, hali nzuri ya kijiografia na kuwa na mafundi wa aina mbalimbali wenye sifa bora. Alisema, hivi sasa ustadi wa nchi nyingi za Afrika wa kutengeneza bidhaa za viwandani na bidhaa za matumizi ya kila siku bado ni chini, hivyo bidhaa zilizotengenezwa nchini China zinapendwa sana na wakazi wa nchi za Afrika kutokana na sifa bora na bei nafuu. Akisema:

"Nchi za Afrika zina fursa nyingi za kujiendeleza kwa wafanyabiashara wa China. Maendeleo ya uchumi wa nchi za Afrika kwa hivi sasa yanalingana na hali ya nchini China katika miaka ya 80 ya karne iliyopita, hivyo hatua zilizochukuliwa na China na uzoefu wa China wa kukuza uchumi unafaa kwa nchi za Afrika."

Kutokana na maendeleo ya uhusiano wa kiuchumi kati ya China na nchi za Afrika, hivi sasa wachina wengi zaidi wanazingatia kwenda katika nchi za Afrika kufanya biashara na kuwekeza vitega uchumi. Bwana Xu Hui alisema ili kufanya biashara vizuri katika nchi za Afrika, wafanyabiashara wa China wanapaswa kufahamu sheria na utamaduni wa nchi za Afrika. Akisema, matatizo makubwa yanayowakabili wafanyabiashara wa China ni kuwa wengi hawafahamu vizuri sheria na utaratibu wa masoko ya nchi za Afrika, hawajui kusema lugha za huko, na hawaelewi utamaduni na desturi za kimaisha za wakazi wa huko.

Bwana Yang Che na mke wake walikuwa wawili miongoni mwa Wachina waliotangulia kwenda barani Afrika kutafuta njia ya kujiendeleza baada ya China kufungua mlango kwa nchi za nje, waliwahi kuendesha zahanati ya kichina, mkahawa wa kichina na duka la kuuzia wanasesere kutoka China, aliwahi kufanya biashara ya tai, magari, kompyuta, nguo na bidhaa za matumizi ya kila siku, yeye pia alikuwa Mchina wa kwanza aliyesajili kampuni ya utalii nchini Kenya.

Bw. Yang Che ni mfanyabiashara anayejua kutupia macho mbele, miaka kadhaa kabla ya China kuwaruhusu Wachina kutalii nchini Kenya, alisajili kampuni ya utalii ya Longren ya Kenya mwaka 1998. Mwanzoni kampuni yake iliwapokea Wachina waliokwenda Kenya kufanya ukaguzi wa soko. Ili kuwafahamisha wachina hali ya vivutio vya utalii vya Kenya, mwaka 2002 kampuni ya utalii ya Longren ya Kenya ilifungua ofisi yake mjini Beijing na kuchapisha vitabu vya picha. Bw. Yang Che mwenyewe alienda katika mashirika mbalimbali ya utalii ya Beijing kutoa mihadhara kuhusu vivutio vya utalii vya Kenya, zana na huduma za utalii nchini Kenya na kadhalika.

Chini ya juhudi za pande mbalimbali, watu wa China walianza kufahamu hatua kwa hatua kuhusu mazingira ya utalii nchini Kenya, na idadi ya watalii wa China wanaoenda kutalii nchini Kenya inaongezeka siku hadi siku.

Kampuni ya Bw. Yang Che ina mabasi madogo matatu na magari madogo kadhaa, pamoja na waongozaji wa utalii wa kichina, inaweza kuwapokea watalii kumi kadhaa kwa mara moja. Bw. Yang Che aliyeishi nchini Kenya kwa miaka 15 anaipenda sana Kenya, alieleza imani yake kuwa, Kenya ina vivutio vizuri vya utalii, kadiri siku zinavyokwenda ndivyo wachina wanavyofahamu zaidi kuhusu vivutio vya utalii vya Kenya, na idadi ya watalii wa China watakaokwenda Kenya kusafiri pia itaongezeka mwaka hadi mwaka.

Idhaa ya kiswahili 2007-01-19