Televisheni ya Iran tarehe 21 mwezi Januari ilitangaza kuwa, kuanzia siku hiyo jeshi la Iran litafanya luteka kwa siku 3. Hiyo ni luteka ya kwanza kuifanya na jeshi la Iran tangu baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lipitishe azimio No. 1737 la kuiwekea vikwazo Iran, ambayo watu wanaichukulia kuwa ni jibu kali kuhusu azimio hilo. Habari zinasema luteka hiyo inafanyika karibu na Garmsar, umbali wa kilomita 100 hivi kusini mashariki mwa Tehran, mji mkuu wa Iran, katika luteka hiyo yatarushwa makombora ya aina za Zalzal na Fajr-5. Makombora ya aina hizo mbili ni ya masafa mafupi, kati ya kilomita 75 na kilomita 400, na lengo la luteka ni kutathimini uwezo wa makombora hayo.
Katika siku wakati luteka hiyo inafanyika, rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran alisisitiza, azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa la kuiwekea vikwazo Iran, kamwe haliwezi kuzuia Iran isipate teknolojia ya nyuklia, hata maazimio kumi ya aina hiyo hayawezi kuathiri sera za uchumi na nyuklia za Iran. Katika mwaka uliopita Iran ilifanya luteka tatu kubwa, na kila mara ilionesha silaha mpya kwa kuonesha nguvu zake za ulinzi, tena kila mara ilifanyika katika wakati ulipotokea mgogoro kwenye uhusiano kati ya Iran na jumuiya ya kimataifa.
Hivi karibuni Iran imekabiliwa na shinikizo kubwa na jumuiya ya kimataifa hususan kutoka Marekani. Hivi karibuni, Marekani ilitangaza sera mpya kuhusu Iraq, zikiwa ni pamoja na kuimarisha nguvu za kijeshi kwenye sehemu ya ghuba. Mbali na hayo, Marekani pia inaishutumu Iran kuingilia kati katika mgogoro wa Iraq, na ilituma jeshi kushambulia ubalozi mdogo wa Iran ulioko huko Arbil na kuwateka nyara wairan watano. Aidha, Marekani ilituma kundi la pili la manowari zenye uwezo wa kubeba ndege za kivita kwenye sehemu ya ghuba na kusafirisha makombora mengi ya aina ya Patriot kwenye sehemu hiyo.
Mbali na shughuli nyingi za kijeshi, hivi karibuni waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bibi Condoleezza Rice alifanya ziara nyingi kwenye sehemu ya mashariki ya kati, akizitaka nchi za sehemu hiyo zishirikiane na Marekani kuitenga Iran, tena alidokeza kuwa Marekani itaimarisha nguvu za vikwazo dhidi ya Iran, wakati waziri mpya wa ulinzi wa Marekani Robert Gates alipofanya ziara nchini Iraq, pia alitoa onyo kwa Iran. Baadhi ya vyombo vya habari vilitoa habari nyingi kuhusu Marekani kujiandaa kufanya mashambulizi ya mabomu dhidi ya zana za nyuklia za Iran katika miezi michache ijayo.
Luteka hiyo ndiyo ilifanyika katika mazingira ambayo Umoja wa Ulaya nao umeweka utekelezaji wa azimio No. 1737 la baraza la usalama kwenye ratiba ya kazi, na mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya tarehe 22 mwezi Januari huko Brussels walikuwa na majadiliano kuhusu Umoja wa Ulaya kupiga marufuku usafirishaji wa vifaa vya nyuklia kwa Iran, na kuchukua hatua za kuzuia fedha zinazohusiana na miradi ya nyuklia zilizoko kwenye akaunti zake barani Ulaya.
Wachambuzi wamesema Iran inataka kueleza mambo mengi zaidi kwa kutumia luteka hiyo. Kwa upande mmoja inataka kuonesha azma yake imara ya kulinda mpango wake wa nyuklia. Tokea mwaka mpya ulipoanza, kiongozi mkubwa wa kiroho wa nchi hiyo Ayatolah Ali Khamenei, rais wa nchi hiyo Mahmoud Ahmedinejad na waziri wa mambo ya nje Bw Manoucher Motaki wamesisitiza mara nyingi katika nyakati tofauti nia ya Iran kuendeleza mpango wa nyuklia, kutorudi nyuma na kutishia hata kwa kujitoa kwenye "mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia".
Kwa upande mwingine serikali ya Iran inatakiwa kutuliza hali ya wasiwasi nchini mwake. Tangu Bw Mahmoud Ahmadinejad alipoingia madarakani, suala la nyuklia la Iran limekuwa likipamba moto, Iran inakabiliana na Marekani kwa uhasama, hatua ambayo imesababisha wasiwasi kwa baadhi ya watu kuhusu usalama wa Iran. Lengo lingine la luteka hiyo ni kuimarisha imani ya watu wa nchi hiyo, na kuona kuwa nchi zenye lengo la kuishambulia Iran zitapata hasara kubwa. Kabla ya hapo rais Mahmoud Ahmadinejad alisema mara nyingi kuwa, Iran ina uwezo wa kujihami, na maneno kuhusu kuanzisha vita ni kuitishia Iran tu. Mwakilishi wa kwanza Iran kwenye mazungumzo ya nyuklia hivi karibuni alisema, jeshi la Iran haliogopi mashambulizi ya jeshi la Marekani, na liko tayari kwa mashambulizi hayo.
Idhaa ya Kiswahili 2007-01-22
|