Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-23 16:53:51    
Ujenzi wa vijiji vipya vya ujamaa waendelezwa vizuri nchini China

cri

Mwaka 2006 ni mwaka ambao ujenzi wa vijiji vipya vya ujamaa nchini China ulianza. Katika mwaka huo wakulima wa China licha ya kufurahia kupata mavuno mazuri ya kilimo, pia walifurahishwa na zaidi na maendeleo yaliyopatikana katika ujenzi wa vijiji vipya.

Bw. Liu Hongwei mwenye umri wa miaka 43 ni mkulima anayeshughulikia zaidi uzalishaji wa nafaka kwenye kijiji cha Xing shisi, mkoani Helongjiang, sehemu ya kaskazini mashariki mwa China, maisha ya watu wa familia yake yanatetegemea mazao ya mahindi na maharage. Bw. Liu Hongwei anapata mavuno mazuri kwa kutegemea kumwagilia maji mashamba yake kwa mtambo na kulima mashamba kwa njia ya kisayansi, ongezeko la mavuno ya chakula ya mwaka huu limemfurahisha zaidi:

"Mwaka 2006, nilipanda mazao ya chakula kwa hekta 80, wastani wa uzalishaji wa maharage katika kila hekta ni kiasi cha tani 2.5, na wastani wa uzalishaji wa mahindi katika kila hekta ni kiasi cha tani 7.5. Uzalishaji wa mahindi kwa mwaka 2005 haukuwa mzuri, ulikuwa ni kiasi cha tani 6 tu kwa hekta."

Hali kadhalika mkulima Ma Yanlin, ambaye ni mkazi wa kijiji cha Daping kilichoko mkoani Gansu, sehemu ya kaskazini magharibi mwa China anafurahi zaidi kuliko wakati wowote katika mwaka 2006. Kijiji cha Daping ni kijiji chenye upungufu wa maji, katika mwaka 2006 kila familia ya wakulima wa kijiji hicho ilijenga shimo la kuvuna maji ya mvua kwenye ua wa nyumba, ambalo lilisaidia sana kuboresha hali ya upungufu wa maji. Bw. Ma Yanlin alisema kwa furaha:

"Mashimo yaliyojengwa ili kuvuna maji ya mvua yanatusaidia sana sisi wakazi wa sehemu ya milimani, hapo zamani tulikwenda kutafuta maji kwenye mabonde, tulipata maji ya kunywa katika bwawa tulilochimba. Polepole, maji ya bwawa yalipungua na sisi tulianza kukabiliwa na shida ya maji ya kunywa na ya kunyweshea mifugo yetu. Baada ya kila familia kuchimba shimo la maji kwenye ua wa nyumba, sasa shida yetu ya maji ya kunywa imeondolewa kabisa."

Mwaka 2006, kulikuwa na mambo mengi ya kufurahisha. Watu waliona barabara nzuri zimejengwa hadi vijijini, ujenzi wa vijiji unaendelezwa kwa kufuata mpango wa kisayansi, watoto wa vijijini hawana wasiwasi wa kutoweza kwenda shule kutokana na matatizo ya kiuchumi: Katika mwaka 2006 wanafunzi walioko katika kipindi cha elimu ya lazima kwenye sehemu ya magharibi mwa China walisamehewa karo na ada nyingine ya shuleni isipokuwa gharama za uchapishaji wa vitabu vya kiada tu, ambapo wanafunzi milioni 50 wa sehemu ya vijiji wamenufaika na sera hiyo.

Mabadiliko hayo yanatokana na serikali kuu na serikali za mitaa za China kuimarisha utekelezaji wa sera za "kuunga mkono na kusaidia kilimo", na zilitoa sera nyingine za aina hiyo katika mwaka 2006.

Kwanza kabisa, serikali ya China imeimarisha uungaji mkono wa fedha kwa maendeleo ya sehemu ya vijiji. Takwimu kutoka wizara ya fedha ya China zinaonesha kuwa, fedha zilizotengwa na serikali kuu katika bajeti ya mwaka 2006 kwa ajili ya sehemu ya vijiji na wakulima zilifikia Yuan bilioni 339.7, zikiwa ni ongezeko la Yuan bilioni 42.2 kuliko mwaka uliotangulia. Fedha hizo hasa zilitumika kuwasaidia wakulima wa sehemu zinazozalisha nafaka, kuwasaidia kununua mbegu bora na mitambo ya kilimo ya kisasa. Mwaka 2006 serikali za China katika ngazi mbalimbali zilitenga fedha nyingi ili kutatua tatizo la kupata maji ya kunywa na usalama wa maji ya kunywa, pamoja na ujenzi wa miundo-mbinu kwenye sehemu ya vijiji. Katika mwaka 2006 serikali ya China ilisema, kuanzia mwaka 2007 itaacha kutoza ada zote shuleni kwa wanafunzi wa sehemu ya vijiji walioko katika kipindi cha elimu ya lazima, isipokuwa gharama ya kununua vitabu vya kiada, kutekeleza utaratibu mpya wa tiba za ushirikiano wa sehemu ya vijiji kote nchini ndani ya miaka 3, tena ni mara ya kwanza kwa baraza la serikali kutoa nyaraka maalumu za kulinda maslahi halali ya wakulima wanaokwenda kufanya vibarua mijini.

Wakati ilipokaribia kuingia mwaka mpya wa 2007, serikali ya China ilifuta kodi ya kilimo iliyokuwa ikitozwa nchini China tangu zaidi ya miaka elfu 2 iliyopita. Mtaalamu wa idara ya utafiti wa maendeleo ya kilimo ya taasisi ya jamii ya China Bw. Hu Biliang alisema, hatua hiyo ni muhimu sana katika kuhimiza maendeleo kwenye sehemu ya vijiji nchini China.

"Mwaka huu serikali imefuta kodi ya kilimo, hili ni jambo kubwa katika historia ya China, kwani imemaliza historia ya kulipa kodi kwa wakulima wanaozalisha mazao ya kilimo iliyodumu kwa zaidi ya miaka 2,600."

Kufuta kodi ya kilimo kote nchini China ni mafanikio makubwa iliyoyapata serikali ya China tangu ilipoanza kufanya mageuzi juu ya utaratibu wa kodi kwenye sehemu ya vijiji mwaka 2000. Pamoja na kupungua kwa aina za kodi, wakulima wa China wamepata manufaa makubwa. Takwimu zinaonesha kuwa, ikilinganishwa na mwaka 1999, baada ya kufutwa kodi ya kilimo, jumla ya Yuan bilioni 125 za kodi zinazolipwa na wakulima wa China zitapungua kwa kila mwaka, kiasi hicho ni kiasi cha Yuan 140 kwa kila mkazi wa sehemu ya vijiji.

Ujenzi wa vijiji vipya umepata maendeleo, wakulima wa China wamefurahi. Lakini China ina idadi ya wakazi wa sehemu ya vijiji milioni 950, hesabu hiyo kubwa inaonesha kuwa ujenzi wa sehemu mpya ya vijiji unakabiliwa na matatizo mengi, hata kama maendeleo makubwa yamepatikana, lakini bado kuna matatizo mengi yanayohitaji wa kuyatatua.

Tukichukulia mfano wa wakulima kwenda kuonana na daktari, kwa sasa ni kwamba utaratibu mpya wa matibabu ya ushirikiano wa sehemu ya vijiji umeanzishwa kwenye baadhi ya sehemu za China, ambao wakulima, serikali za mitaa na serikali kuu zinaanzisha mfuko wa fedha za matibabu wa kuondoa matatizo kwa wakulima kuweza kupata matibabu, hivi sasa zaidi ya wakulima ni milioni 200 wanashiriki kwenye utaratibu huo, kwa kiwango fulani utaratibu huo wa matibabu unaweza kubadilisha hali ya wakulima ya kutopata matibabu, na kuhakikisha kuwa wakulima wanapata huduma za kimsingi kabisa ya matibabu, lakini hivi sasa utaratibu huo unahusisha asilimia 40 tu ya sehemu ya vijiji ya China, na sehemu nyingi za vijijini za nchini China bado hazijapata huduma hiyo.

Mzee Dong Fengyou mwenye umri wa miaka zaidi ya 60 pamoja na mkewe Bibi Si Shujun, wanaishi kwenye kijiji cha Songjia mkoani Jilin, sehemu ya kaskazini mashariki mwa China. Kijiji chao kiko kwenye sehemu ambayo bado utaratibu wa matibabu ya ushirikiano bado haujaanza kutekelezwa. Mzee Dong alimwambia mwandishi wetu wa habari kwa wazee wenye umri mkubwa kama wao wa sehemu ya vijiji, shida kubwa zaidi ni kutokuwa na fedha za kutosha kupata matibabu wanapokuwa wagonjwa.

Naibu mkurugenzi wa idara ya mpango wa maendeleo ya wizara ya kilimo ya China Bw. Zhou Yinghua alisema, wizara ya kilimo ya China itasaidia sehemu ya vijiji iliyoko magharibi mwa China kutatua njia ya kuanzisha sekta maalumu ya uzalishaji mali kwa kufuatana na hali halisi za huko ili kuharakisha hatua za ujenzi wa sehemu mpya ya vijiji kwenye sehemu ya magharibi mwa China, na kupunguza tofauti ya maendeleo kati ya sehemu ya mashariki na magharibi.

Idhaa ya kiswahili 2007-01-23