Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-23 16:51:08    
China yaendelea kujiunga na dunia kwa haraka

cri

China ilijiunga na shirika la biashara duniani, WTO tarehe 11 mwezi Desemba miaka 5 iliyopita, na kuingia kipindi cha ongezeko la kasi la uchumi, ambacho watu mbalimbali duniani wanalishangaa. Katika miaka hiyo michache iliyopita China imepata maendeleo ya pande zote katika uchumi na jamii, na sasa inachukua nafasi ya nne kwa ukubwa wa uchumi na nafasi ya tatu kwa usafishaji wa bidhaa kwa nchi za nje duniani. Licha ya kupata maendeleo ya kasi, China inaendelea kutekeleza sera za kufungua mlango na kujiunga na dunia, na imetoa mchango mkubwa katika ustawi wa uchumi wa dunia.

Takwimu mpya zilizotolewa hivi karibuni na Benki ya Dunia zinaonesha, katika miaka mitano iliyopita tangu China ijiunge na shirika la biashara duniani WTO, wastani wa mchango wa ongezeko la uchumi wa China kwa ongezeko la uchumi wa dunia umefikia 13%, na imekuwa moja ya injini muhimu ya kusukuma ongezeko la uchumi duniani. Mwakilishi wa kwanza wa ofisi ya Benki ya Dunia iliyoko nchini China Bw. Du Dawei alisema,

"Katika miaka 5 iliyopita tangu China ijiunge na WTO, mchango unaotolewa na China kwa ongezeko la biashara ya dunia ni 20%, China ni nchi inayosafirisha bidhaa kwa wingi katika nchi za nje, na pia ni nchi inayoagiza bidhaa nyingi kutoka nchi za nje, ongezeko la uagizaji wa bidhaa ni kiasi cha 25% kwa mwaka, na sasa China imekuwa ni soko kubwa barani Asia hata kwa nchi mbalimbali.

Baada ya kujiunga na WTO, China inafuata kanuni za WTO na kutekeleza ahadi ilizotoa, imefanya marekebisho makubwa kuhusu utaratibu na sera za biashara. Kiwango cha kufungua mlango wa soko la biashara ya bidhaa kwa China kinainuka kwa udhahiri, wastani wa ushuru wa forodha umepungua kutoka 15.3% hadi kufikia 9.9% katika mwaka 2005, kama ilivyoahidi wakati ilipojiunga na shirika la biashara duniani WTO; China inafungua hatua kwa hatua mlango wa soko la biashara ya huduma na kuimarisha nguvu ya utekelezaji wa sheria katika kulinda haki-miliki ya kiujuzi. Licha ya hayo, China imerekebisha sheria na kanuni kadhaa zikiwa ni pamoja na sheria na mitaji ya kigeni na sheria ya biashara ya nje, zaidi ya hayo imebuni, kurekebisha na kubadilisha sheria, kanuni na maagizo ya kisheria zaidi ya 2,000.Mkurugenzi mkuu wa tawi la kampuni ya Motorola la nchini China Bw. Gao Ruibin alisema, baada ya kujiunga na WTO, China imeongeza uwazi wa sheria na sera na imetoa dhamana ya kisheria kwa wawekezaji wa kigeni.

"Kubadilika kwa majukumu ya serikali za China katika ngazi mbalimbali na kuinuka kwa mwamko wa kutoa huduma pamoja na uwazi wa sheria na utaratibu, vimeongeza nguvu ya ushawishi ya mazingira ya uwekezaji nchini China."

Katika miaka mitano iliopita tangu China ijiunge na shirika la biashara duniani WTO, maofisa wa serikali pamoja na kampuni na viwanda vya China, walijifunza kanuni za biashara ya kimataifa na kukuza uwezo wao wa kujilinda. Mwamko kuhusu uchumi wa soko huria unaohimizwa na WTO unazidi kufahamika kwa wachina mwaka hadi mwaka. Waziri wa biashara wa China Bw. Bo Xilai alisema, katika miaka mitano iliyopita, China imepata maendeleo makubwa katika ujenzi wa utaratibu wa soko huria na muundo wa uchumi wa aina mbalimbali, lakini kitu muhimu zaidi kuliko utaratibu ni kuinuka kwa hali ya maisha ya wachina. Alisema,

"Tumeona kuwa katika miaka mitano iliyopita wachina wamepiga hatua kubwa za maendeleo katika utaratibu wa sheria, ajira, hifadhi ya haki-miliki za kiujuzi na kulinda haki zao. Katika miaka hiyo, wanaviwanda wa China wamekuwa na mtizamo wa uvumbuzi na maendeleo na kupanga mpango wa kampuni zao kwa mtazamo wa kimataifa."

Tangu China ijiunge na WTO, imeweza kudumisha ongezeko la kasi la uchumi. Taarifa ya idara ya takwimu inaonesha kuwa, pato la nchini limeongezeka hadi kufikia zaidi ya Yuan bilioni 14.14 katika miezi 9 ya mwanzo ya mwaka 2006 ikiwa ni ongezeko la 9% kutoka Yuan milioni 959 katika mwaka 2001.

Tarehe 11 mwezi Desemba mwaka 2006 ilikuwa siku ya mwisho ya kipindi cha mpito cha miaka mitano baada ya China ijiunge na WTO. Kumalizika kwa kipindi cha mpito siyo mwisho wa ufunguaji mlango kwa China, bali ni kuwa katika siku za baadaye China itaendelea kutekeleza sera za mageuzi na ufunguaji mlango, kuboresha biashara ya pande nyingi na kutatua kwa makini mikwaruzano ya kibiashara.

Idhaa ya kiswahili 2007-01-23