Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-24 15:04:19    
China kuharakisha ujenzi wa mfumo wa kukabiliana na hali ya dharura katika miji

cri

Wakati maafa makubwa yakiwemo moto, matetemeko ya ardhi, dhoruba, maporomoko ya ardhi na magonjwa ya kuambukiza yakitokea, kama mfumo wa kukabiliana na hali ya dharura katika miji unaweza kuonesha umuhimu wake au la kunahusiana na usalama wa maisha na mali ya wakazi wa miji hiyo. Nidyo kwa sababu hiyo, mfumo huo umekamilika au kupevuka au la ni kigezo kimoja muhimu katika upimaji wa kiwango cha maendeleo ya mji huo.

Mwaka 2003, maambukizi makubwa ya ugonjwa wa SARS yaliibuka nchini China; mwaka 2005 maambukizi ya homa ya mafua ya ndege yalitokea katika baadhi ya mikoa ya China; mwaka 2006, dhoruba kubwa kadhaa ziliikumba kwa mfululizo mikoa ya kusini ya China. Matukio kama hayo yanapima uwezo wa miji ya China kukabiliana na hali ya dharura, pia yanasukuma mbele kazi ya kukamilisha mfumo wa kukabiliana na hali ya dharura katika miji ya China.

Mji wa Beijing uliathiriwa vibaya na maambukizi ya SARS mwaka 2003. viongozi wa mji wa Beijing walitambua kuwa, mfumo ulio wa nyuma wa kukabiliana na maambukizi ya magonjwa ulishindwa kuwafahamisha maofisa husika kwa wakati kuhusu hali ya maendeleo ya maambukizi ya ugonjwa, hii ni sababu kubwa kwa ugonjwa wa SARS kuambukiza kwa kasi katika muda mfupi. Mkurugenzi wa kituo cha upashanaji wa habari cha idara ya huduma za afya ya Beijing Bw. Ju Wensheng alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa,

katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya mji inatilia maanani shughuli za afya ya umma,na kutoa mapendekezo kuhusu kuimarisha shughuli hizo. Serikali ya Beijing imeweka ofisi 13 maalum ikiwemo ofisi ya kukabiliana na hali ya dharura ya afya ya umma. Aidha, wizara ya afya ya China pia inazitaka sehemu mbalimbali zijenge mfumo wa kukabiliana na hali ya dharura ya kiafya kama huo."

Hivi sasa, idadi ya wakazi wa mijini imechukua asilimia 40 ya ile ya jumla ya China, na miji imechukua asilimia 50 ya uzalishaji wa jumla wa viwanda wa China, asilimia 80 ya pato la kodi la taifa na asilimia 90 ya raslimali za elimu ya juu na utafiti wa kisayansi. Kama mfumo wa kukabiliana na hali ya dharura mijini utakamilika ndipo kutaiwezesha miji kukabiliana na changamoto za maafa ya kimaumbile, matukio ya dharura ya afya ya umma na usalama, na kuhakikisha maendeleo ya miji. basi mfumo kamili wa kukabiliana na hali ya dharura mijini ni wa namna gani? Mtaalamu wa hali ya juu wa taasisi ya usalama wa umma katika chuo kikuu cha Qinghua ambaye pia ni mkurugenzi wa maabara ya taifa ya sayansi ya maafa ya moto Bw Fan Weideng alisema:

"ujenzi wa mfumo wa kukabiliana na hali ya dharura mijini ni pamoja na sehemu tatu, ya kwanza ni makao makuu ya uongozi wa shughuli za kukabiliana na hali ya dharura, ya pili ni mfumo wa uungaji mkono wa kimsingi, ya tatu ni mfumo wa matumizi ya jumla."

Bw. Fan Weideng alieleza kuwa, mfumo wa uungaji mkono wa kimsingi ni uungaji mkono wa teknolojia ya upashanaji wa habari, ikiwemo mfumo wa mawasiliano na mfumo wa mtandao wa kompyuta; mfumo wa matumizi ya jumla ni mfumo wa software, zikiwemo maktaba za takwimu, mfumo wa usimamizi wa jumla, mfumo wa usimamizi wa hatari, mfumo wa uhakikishaji wa kukabiliana na hali ya dharura, na mfumo wa uratibu na uongozi. Katika mfumo wa matumizi ya jumla, uendeshaji wa software unategemea data mbalimbali kwenye maktaba, hivyo maktaba za data za takwimu ni sehemu muhimu katika mfumo huo.

Bw. Fan Weideng pia alieleza hatua mbalimbali katika kushughulikia matukio ya dharura. Alisema:

"wakati wa kukumbwa na tukio la dharura, kama kampuni au idara husika hazikuweza kukamilisha kazi zao za kulishuhulikia au zilishindwa kushughulikia kazi husika za tukio hilo, data husika za tukio hilo zitafikishwa kwenye mfumo wa usimamizi katika kituo cha uongozi wa shughuli za kukabiliana na hali ya dharura, idara husika zitafanya tathmini kuhusu tukio hilo, halafu zitaweka mpango mwafaka, hatua ya kwanza ni kutoa taarifa ya tahadhari kwa jamii, ya pili ni kukusanya nguvu ya misaada ya dharura kwenye sehemu ambapo hatari ilitokea."

Hivi sasa katika miji mikubwa ya China, mifumo mbalimbali ya kukabiliana na hali ya dharura inajengwa, ikiwemo usalama wa umma, kuzima moto, matibabu ya dharura, utoaji wa maji, umeme na gesi. Kama hali ya dharura ikitokea, mfumo huo unaweza kushirikisha idara mbalimbali husika kushughukulia kwa pamoja.

Lakini wataalamu pia wameeleza kuwa, ujenzi wa mifumo hiyo nchini China bado unakosa chombo cha kiini cha pamoja, bali mifumo mbalimbali inajengwa kwa lengo la matukio ya aina mbalimbali, kwa mfano mfumo wa kukabiliana hali ya dharura katika michezo ya Olimpiki, kwa ajili ya kupambana na ugaidi au homa ya mafua ya ndege. Kwa hivyo kama masuala mapya yakitokea, mifumo hiyo haiwezi kupanua uwezo wake ili kuyakabili, bali mifumo mipya inapaswa kujengwa. Hali hiyo imeongeza gharama zisizo za lazima. Msimamizi mkuu wa ufundi wa ofisi ya Beijing katika kampuni ya Netgain Systems ya Singapore Bi. Wang Weiping alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari, alipendekeza China kujenga mfumo wa jumla wa kukabiliana na hali ya dharura mijini. Alisema:

"kwa kuwa mfumo huu ni mkubwa na mwenye utatanishi, hivyo unahitaji chombo maalum kinachousimamia ili kupunguza kiwango cha utatanishi wake. Aidha mfumo huo lazima ni uwe na uwezo wa jumla na pia unapaswa kuendelea kufanya kazi kwa muda mrefu."

Hivi sasa, serikali ya China inazingatia kujenga mfumo wa jumla wa kukabiliana na hali ya dharura mijini kwenye msingi wa mfumo wa E-Gov uliojengwa miaka ming iliyopita, ili kutumia mwafaka raslimali na kuinua ufanisi wa kazi.