Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-24 17:11:11    
Mapishi ya myugwa na kuku

cri

Mahitaji:

Nyama ya kuku gramu 200, myugwa gramu 50, tangawizi, vitunguu maji na vitunguu saumu kila kimoja gramu 5, sukari gramu 19, sosi ya pilipili hoho gramu 5, chembechembe za kuongeza ladha gramu 3, pilipili kima gramu 3

Njia:

1. kata tangawizi, vitunguu maji na vitunguu saumu viwe vipande. Kata myugwa uwe vipande.

2. chemsha maji tia nyama ya kuku endelea kuchemsha kwa dakika 20, halafu uipakue na uikate iwe vipande.

3. chemsha maji tena tia myugwa ndani ya maji mpaka uwe laini upakue halafu weka kwenye maji ya baridi.

4. washa moto tia mafuta kwenye sufuria, tia sukari kwenye sufuria punguza moto uwe mdogo, korogakoroga sukari halafu tia vipande vya tangawizi, vitunguu maji, vitunguu saumu, sosi ya pilipili hoho, pilipili kima kasha korogakoroga, tia vipande vya nyama ya kuku, korogakoroga, mimina maji uliyochemshia nyama ya kuku, baada ya kuchemka, tia chembechembe za kuongeza ladha, tia vipande vya myugwa endelea kuchemsha kwa dakika 15. ipakue na mimina vipande vya vitunguu maji. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.