Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-25 15:53:20    
Vijana wanaojitolea wa China waenda kutoa huduma barani Afrika

cri

Tarehe 24 Januari huko Harare, mji mkuu wa Zimbabwe ilifanyika sherehe moja ya kuwalaki vijana wanaojitolea kutoka China, katika kipindi cha mwaka mmoja vijana hao watafanya shughuli zinazohusiana na mifugo, kilimo, elimu na matibabu nchini Zimbabwe.

Vijana 15 wa China walihudhuria sherehe hiyo, wakivaa suti nyeusi zenye nembo ya vijana wanaojitolea wa China. Kijana mmoja aliwavutia sana watu, yeye anaitwa Xu Benyu aliwahi kufanya kazi ya ualimu kwa muda mrefu katika sehemu ya milimani yenye umaskini ya magharibi mwa China. Kijana huyo alisema "Kujitolea kwenda ng'ambo kuwasaidia wengine ni nia niliyoweka mwaka 2002. Niliwahi kufanya kazi ya ualimu mkoani Guizhou na ninaona huzuni kuwaaga watoto wa huko, lakini kila mtu ana ndoto ambayo inafaa kuyatimiza wakati wa ujana. Nikishirikiana na kijana mwingine anayejitolea, tutafundisha lugha ya Kichina katika chuo cha ualimu cha Harare, nitafanya kila niwezalo katika kazi hii."

Mwezi Novemba mwaka 2006, rais Hu Jintao wa China akifungua mkutano wa wakuu wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika huko Beijing, alitoa ahadi kuwa China itatuma vijana 300 wanaojitolea barani Afrika katika miaka mitatu ijayo. Safari hiyo kutuma vijana kwenda Zimbabwe ni mradi wa kwanza kutelekezwa baada ya China kutoa ahadi hiyo. Vijana hao wana umri wa wastani wa miaka 29, mmoja kati yao ana shahada la udaktari, 6 wana shahada la pili na wengine pia ni wahitimu wa vyuo vikuu. Katika mwaka mmoja ujao wao watapelekwa kwenye vyuo vikuu na shule za ufundi wa kazi nchini Zimbabwe, kufanya shughuli zinazohusiana na mifugo, utengenezaji wa mazao ya kilimo, mafunzo ya lugha ya Kichina, mafunzo ya ujuzi wa kompyuta, mafunzo ya michezo na matibabu ya Kichina.

Katika sherehe hiyo ya kuwalaki vijana wa China, waziri wa vijana na ajira wa Zimbabwe Bw. Ambrose Mutinhiri alieleza kuwa, hatua ya serikali ya China kutuma vijana wanaojitolea nchini Zimbabwe, itaimarisha urafiki kati ya nchi hizo mbili na kukuza uhusiano wa nchi hizo mbili. Alisema "Serikali ya Zimbabwe inawakaribisha vijana wanaojitolea kutoka China. Idara mbalimbali za serikali ya Zimbabwe zitawasaidia vijana hao wa China ili wafanye shughuli zao bila matatizo."

Waziri Mutinhiri aliongeza kuwa, Zimbabwe inatumai kuwa China itatuma watu wengi zaidi wanaojitolea kutoa huduma katika shughuli za upashanaji habari, utamaduni, utalii na matibabu ya Kichina. Alisema serikali ya Zimbabwe inaamini kuwa, vijana hao wa China na shughuli wanazofanya nchini Zimbabwe zitasaidia kuongeza maelewano, maingiliano na ushirikiano kati ya watu wa nchi hizo mbili.

Balozi wa China nchini Zimbabwe Bw. Yuan Nansheng alisema "China na Zimbabwe zina urafiki mkubwa kwa miaka mingi, China siku zote inaichukulia Zimbabwe kuwa ni rafiki mkubwa anayeaminika. Serikali ya China pia imekuwa inaipatia serikali ya Zimbabwe na watu wake misaada inayolingana na uwezo wake. Serikali ya China inaamini kuwa vijana wanaojitolea wa China watatoa mchango katika ujenzi wa Zimbabwe."

Kujenga urafiki, kusaidiana na kupata maendeleo ya pamoja ni lengo la vijana wanaojitolea wa China, ambao wanataka kujenga daraja la kubadilishana utamaduni na hisia kati ya watu wa China na Afrika.

Idhaa ya Kiswahili 2007-01-25