Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-26 17:25:52    
Wachina wametoa mchango kwa bara la Afrika kuingia katika zama mpya za kujiendeleza

cri

Katika miaka 6 au 7 iliyopita wachina laki saba na elfu 50 hivi walikwenda katika nchi za Afrika, na idadi hiyo inaongezeka siku hadi siku. Wafanyabiashara wa China walikuwa wamepeleka fulana, suruali za jeans, televisheni, viyoyozi, motakaa nyepesi na bidhaa nyingine za matumizi ya kila siku katika nchi za Afrika, na kuziuza kwa bei nafuu. Kufika kwa wafanyabiashara wa China barani Afrika kumewanufaisha watu wengi wa Afrika.

Mwandishi wa habari wa gazeti la The Economy la Ujerumani Bwana Diter Snarth aliandika makala ikisema, wachina waishio katika nchi za Afrika wamepeleka bidhaa zilizotengenezwa nchini China, kuendesha mikahawa na zahanati. Pia wameshiriki katika ujenzi wa miji, vituo vya kuzalisha umeme, kujenga barabara na reli, na miradi mingine ya miundo mbinu. Ujumbe wa serikali na wa watu binafsi kutoka China unaonekana hapa na pale katika miji mikuu au miji mikubwa ya nchi za Afrika, serikali ya China inazipa nchi za Afrika mikopo mikubwa yenye riba nafuu, na kusamehe madeni mengi inayozidai. Mwaka 2005 thamani ya biashara kati ya nchi za Afrika na China ilikuwa dola za kimarekani bilioni 35, hili ni ongezeko la mara 20 kuliko lile la kabla ya miaka 10 iliyopita. China imekuwa mshirika mkubwa wa tatu wa biashara wa nchi za Afrika ikifuata Marekani na Ufaransa, na inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2010, China itakuwa mshirika wa kwanza wa kibiashara kwa nchi za Afrika.

Makala hiyo imesema wachina wamewekeza katika sekta nyingi ambazo ni pamoja na kilimo, afya, mawasiliano ya simu, na uchimbaji wa mafuta na madini. Makampuni ya China yamesaini mikataba ya miradi mingi katika nchi za Afrika, kama vile mradi wa kuweka mabomba ya kupitisha mafuta nchini Sudan, kujenga uwanja wa michezo ya riadha nchini Mali, kujenga majumba ya serikali nchini Namibia, Msumbiji na Uganda, kuanzisha kijiji cha pwani cha kuwapokea wageni na kiwanda cha kutengeneza matrekta huko Sierra Leone. Kuongezeka kwa thamani ya biashara kati ya China na nchi za Afrika na ongezeko la uwekezaji kutoka China, vimeleta ongezeko la kiuchumi la zaidi ya asilimia tano kwa nchi za Afrika mwaka 2005, na kupunguza kiwango cha mfumuko wa bei za vitu na kufikia kiwango cha chini kabisa katika miaka 25 iliyopita. Mitaji ya nje iliyoingia barani Afrika kwa njia ya uwekezaji, kwa mara ya kwanza ilizidi mitaji ya nje iliyoingia katika nchi za Afrika kwa njia ya misaada katika historia ya Afrika. Watu wengi wameona kuwa hii itakuwa na mabadiliko makubwa katika historia ya bara la Afrika, kama waziri wa mambo ya nje wa Nigeria alivyosema, huu ni mwanzo wa zama mpya kwa nchi za Afrika.

Bwana Diter Snarth alipomalizia makala yake alisema: si wajibu wa China kuzihimiza nchi za Afrika kutumia vizuri fursa hiyo ya kihistoria ya kushiriki katika utandawazi wa uchumi duniani. Lakini ni wachina ambao wametoa fusra nzuri kwa watu wa Afrika kushika hatamu za maisha yao kwa mara ya kwanza.

Gazeti la the Guardian la Uingereza lilichapisha makala kuhusu jinsi makampuni ya China yalivyoshindana na nchi za Ulaya katika soko la Afrika ikisema kuwa, katika miaka ya hivi karibuni wachina wameingia kwenye soko la Afrika kwa kiwango kikubwa, walikuwa hawazingatii sababu ya kisiasa au ya kijiografia, wanawekeza katika nyanja zote za uchumi kama vile mawasiliano ya simu, misitu na ujenzi wa miradi ya umma. Wachina wanazingatia zaidi ufanisi wa uwekezaji kuliko mambo mengine.

Kwa mfano, Jamhuri ya Afrika ya kati imekuwa maskini sana baada ya kukumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka mingi, wakati shirika la fedha duniani, benki ya dunia na mashirika mengine ya kimataifa yalikuwa yanasitasita kutoa mikopo kwa nchi hiyo, serikali ya China ilikuwa imetoa misaada mingi na kuwekeza vitega uchumi katika sekta mbalimbali za nchi hiyo kama vile mambo ya fedha, utafutaji na uchimbaji wa mafuta na kiwanda cha kuzalisha saruji, nchi hizo mbili pia zimesaini makubaliano ya ushirikiano katika kilimo na mambo ya ulinzi.

Mwaka 2002 Zimbabwe ilianza kutekeleza sera ya mageuzi ya ardhi, hatua hiyo ilipingwa na kuwekewa vikwazo na nchi kadhaa za magharibi, lakini wafanyabiashara wa China walienda nchini humo kufanya biashara na kuwekeza vitega uchumi na kupata mafanikio. Mwishoni mwa miaka ya 90 ya karne iliyopita, vita kati ya Ethiopia na Eritrea iliwafanya waingereza na wamarekani wazikimbie nchi hizo haraka. Lakini serikali ya China ilitoa misaada, mikopo na kupeleka watu wanaojitolea nchini Ethiopia, watu wa China wamechangia maendeleo ya huko, pia wamenufaika kutokana na kufanya hivyo.

Idhaa ya kiswahili 2007-01-26