Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-30 16:25:32    
Udhibiti wa mpango mkuu wa uchumi wa taifa kwa mwaka 2006 ulipata ufanisi

cri

Mwaka 2006 ulikuwa ni mwaka wa kwanza wa kutekeleza mpango wa 11 wa maendeleo wa miaka mitano ya uchumi na jamii ya China. Katika mambo ya uchumi kwa mwaka huo, vitu viwili vilikuwa muhimu sana, ambayo ni "ongezeko la kasi" na "udhibiti wa mpango mkuu wa uchumi wa taifa". Tarehe 15 mwezi Novemba mwaka 2006, Benki kuu ya China iliinua kiwango cha fedha za akiba kwa benki za biashara nchini China hadi 9% ikiwa ni ongezeko la 0.5%. Hii ni mara ya tatu kwa benki kuu ya China kuinua kiwango cha akiba ya fedha kwa benki za biashara katika mwaka 2006, ambapo jumla ya ongezeko la kiwango kilichoinuliwa imefikia 1.5%, hili ni jambo lisilowahi kuonekana katika historia ya China kwa kutumia mbinu za sera za sarafu kudhibiti mambo ya uchumi.

Mwaka 2006, uchumi wa China uliongezeka kwa kasi ongezeko likiwa ni 10.3% katika miezi mitatu ya mwanzo, na ongezeko lilifikia 10.7% katika miezi 9 ya kwanza. Pamoja na mfululizo wa ongezeko la uchumi, manunuzi kwa wakazi wa mijini na vijijini yalipanuka kwa hatua madhubuti. Lakini nyuma ya ongezeko la kasi ilifichika hali ya hatari ikiwemo upungufu mkubwa wa malighafi na nishati, na hata kulikuwa na hatari ya mfumuko wa bei za vitu kutokana na benki kutoa mikopo mingi, ongezeko kubwa la uwekezaji na pato kubwa katika biashara ya nje.

Mtafiti wa idara ya utafiti wa mambo ya fedha ya taasisi ya sayansi ya jamii ya China Bw. Yin Jianfeng alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema, utekelezaji wa sera za sarafu ikiwemo kuinua kiwango cha fedha za akiba kwa benki za biashara ni umaalumu mkubwa wa udhibiti wa mpango mkuu wa taifa katika mwaka 2006, na lengo lake ni kuzuia ongezeko kubwa kupita kiasi la uwekezaji.

"Benki za biashara zina sababu za kutosha za kutoa mikopo, ambayo ni chanzo cha uwekezaji. Ili kudhibiti hamu ya benki za biashara ya kutoa mikopo na kudhibiti ongezeko la kasi la uwekezaji, Benki ya umma wa China ilitekeleza sera za kuinua kiwango cha fedha za akiba kwa benki za biashara, ambayo ni alama kubwa kwa wawekezaji, yaani kuwa katika wakati wa kutokea ongezeko kubwa la kupita kiasi la kiuchumi, idara husika ya serikali kuu itachukua hatua kali za kutatua tatizo hilo."

Sekta ya soko la nyumba ni moja ya sekta muhimu zinazohimiza uwekezaji kwa mali zisizohamishika. Tokea mwanzoni mwa mwaka 2006, bei za nyumba ziliendelea kupanda katika sehemu mbalimbali nchini, hali hiyo ilichangia ongezeko la kasi la uwekezaji kwa ujenzi wa nyumba na utoaji wa mikopo ya nyumba, ambayo mgogoro wa mambo ya fedha ulikuwa umefichika nyuma yake. Bei kubwa ya nyumba pia imebadilisha maisha ya watu. Mkazi wa mji wa Qingdao Bw. Zhang Ke ni mtu anayependa sana kufanya matembezi katika sehemu ya nje, lakini tangu aliponunua nyumba mpya, fedha za mkopo wa nyumba anazotakiwa kulipa kila mwezi zimezidi pato la mshahara wake wa kila mwezi, hivyo amelazimika kuzima shauku yake ya kutalii.

Kupanda kwa bei ya nyumba kumefuatiliwa sana na serikali ya China, idara husika imetoa sera sita husika, licha ya kutoa adhabu kwa ulanguzi wa nyumba, pia zinahakikisha wakazi wenye pato la wastani na dogo wanapata nyumba za kuishi.

Mwaka 2006 serikali iliinua kiwango cha kuanzia cha kutoza kodi, kuimarisha huduma za tiba na kutenga fedha nyingi katika utekelezaji wa sera za elimu za lazima, ambapo manunuzi ya wakazi wa China kuhusu nyumba, magari, simu za mkononi, kompyuta na gharama za elimu yaliongezeka. Inatarajiwa kuwa jumla ya uuzaji kwa rejareja wa vitu vya mahitaji ya watu katika maisha itaongezeka na kufikia Yuan trilioni 7.5 ikiwa ni ongezeko la 13%.

Hata hivyo nguvu inayohimiza ongezeko kubwa la uchumi wa China bado ni uwekezaji. Katika miezi tisa ya mwanzo ya mwaka 2006, kiasi cha mchango uliotolewa na uwekezaji kwa ongezeko la uchumi kilifikia 49.9%, lakini mchango wa manunuzi ya watu ulikuwa 35.7% tu. Aidha kutokamilika kwa mfumo wa huduma ya jamii, kunawafanya watu wa China wawe na uangalifu mkubwa wakati wa kufanya manunuzi.

Ingawa udhibiti wa mpango mkuu wa taifa ulipata ufanisi katika mwaka 2006, lakini baadhi ya mikoa ya China hivi sasa bado ina hamu kubwa ya uwekezaji. Hivyo mkazo utakaowekwa katika udhibiti wa uchumi ni kuleta uwiano kati ya manunuzi, uwekezaji na usafirishaji bidhaa kwa nchi za nje, na kufuatilia ubora na ufanisi wa ongezeko la uchumi.

Idhaa ya kiswahili 2007-01-30