Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-30 16:33:22    
China yashiriki kwenye makubaliano ya kimataifa kuhusu utoaji wa hewa inayosababisha kuongezeka kwa joto duniani

cri

Katika miaka ya karibuni utoaji wa hewa inayosababisha kuongezeka kwa dunia kuwa joto imekuwa ikifuatiliwa na watu wa nchi mbalimbali. "Mkataba wa Kyoto", ambao ulianza kufanya kazi mwaka 2005 unaagiza kuwa nchi zilizoendelea zinatakiwa kupunguza utoaji wa hewa inayosababisha kuongezeka kwa joto duniani, lakini haujatoa maagizo kwa nchi zinazoendelea. Katika hali hiyo, utaratibu wa ruhusa ya utoaji wa hewa zinazosababisha kuongezeka kwa joto duniani (CDM), unaanza kufuatwa na kuchukuliwa kuwa ni moja ya njia zenye ufanisi za kuzuia kuongezeka kwa hali ya joto duniani.

Mwezi Septemba mwaka 2006, shirika la utoaji misaada kuhusu hewa ya carbon dioxide lilisaini makubaliano kuhusu ruhusa ya utoaji wa carbon dioxide pamoja na kampuni ya chuma cha pua ya Nanjing, China kwa kupitia Benki ya Dunia. Kutokana na makubaliano hayo, kampuni ya chuma cha pua ya Nanjing imepata teknolojia ya kisasa pamoja na fedha za kutekeleza mradi wa kurudisha hewa inayotoka kwenye mtambo wa kubadilishia hewa, wakati kampuni iliyolipa gharama hiyo inapata ruhusa ya kutoa tani laki 6.5 za carbon dioxide katika miaka 10 ijayo. Mkurugenzi wa idara ya maendeleo ya kampuni ya chuma cha pua ya Nanjing Bw. Liu Yuejian alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, mradi huo unaweza kurudisha hewa iliyozalishwa katika uyeyushaji wa chuma cha pua, ambayo inaweza kutumika katika kuzalisha umeme, hivyo licha ya kuweza kuhifadhi mazingira ya asili, pia itaongeza nishati.

"Kampuni yetu itaongeza pato la Yuan milioni 32. sisi tukipiga hesabu kwa mitambo miwili ya kubadilisha hewa, gesi itakayozalishwa itaweza kutumiwa kuzalisha kilowatt milioni 150 za umeme kwa saa. Kampuni hiyo imekuwa mfano wa kuigwa kwa sekta ya chuma na chuma cha pua ya China."

Huo ni mradi wa kwanza wa uokoaji wa nishati wa mpango wa CDM kutokana na mkataba ya Kyoto. Mkataba wa Kyoto unaagiza kuwa, tokea mwaka 2008 hadi mwaka 2012, utoaji wa hewa inayosababisha kuongezeka kwa joto duniani kwa wa nchi 35 zilizoendelea zikiwa ni pamoja na carbon dioxide na hewa nyingine utapungua kwa 5.2% kuliko mwaka 1990, la sivyo zitapata adhabu kubwa. Kwa upande mwingine, mkataba wa Kyoto haujaweka kigezo kwa nchi zinazoendelea. Kwa kuwa hewa inayofanya dunia kuwa joto inahamahama, tena ni gharama kubwa kwa nchi zinazoendelea, hivyo jumuiya ya kimataifa imeweka utaratibu wenye unyumbufu kuhusu mpango wa CDM, ambao unaruhusu nchi za viwanda kuwa na mpango na nchi zinazoendelea kuhusu utoaji wa hewa inayofanya dunia kuwa joto.

Kutokana na mpango huo, nchi za viwanda zinatakiwa kutoa fedha na teknolojia husika kwa nchi zinazoendelea, kuziunga mkono kutekeleza miradi ya kupunguza utoaji wa hewa inayosababishwa kuongezeka kwa joto duniani ili kupunguza kiasi cha utoaji wa hewa huyo katika nchi zinazoendelea; Na nchi zinazoendelea zinaweza kupata nguvu kwa maendeleo endelevu kutokana na ushirikiano wa miradi husika. Kwa ufupi ni kuwa nchi zilizoendelea zinatakiwa kutoa fedha za kuzisaidia nchi zinazoendelea kupunguza utoaji wa hewa inayosababishwa kuongezeka kwa joto duniani, ili zifikie kwenye kiwango fulani cha utoaji wa hewa hiyo.

Serikali ya China imeweka lengo la kuokoa 20% ya nishati inayotumika katika uzalishaji mali. Pia inaeneza mpango wa nchi za viwanda kutoa msaada wa fedha na teknolojia ili zipate kiasi cha utoaji wa hewa ya carbon dioxide kunaendana na lengo hilo la China, na inasaidia kupunguza vizuizi vya upungufu wa rasilimali kwa maendeleo ya jamii na uchumi wa China. Kwa hiyo kampuni na viwanda vingi vya China vimeshiriki katika mpango huo wa kupunguza utoaji hewa ya carbon dioxide. Takwimu kutoka kamati ya maendeleo na mageuzi ya taifa zinaonesha kuwa, hivi sasa China inatekelezwa miradi 120 ya kupunguza utoaji wa hewa ya carbon dioxide, ambayo inapunguza tani zaidi ya milioni 600 za hewa ya carbon dioxide zinazotolewa, ambapo fedha zinazotumika katika mpango wa makubaliano hayo ni kiasi cha dola za kimarekani bilioni 3.5.

Naibu mkurugenzi wa ofisi ya mazingira ya dunia ya wizara ya sayansi na teknolojia ya China Bw. Lu Xuedu alisema, China ni moja ya masoko ambayo yatakuwa na uwezo mkubwa duniani katika siku za baadaye.

"Washiriki wanaweza kupata nafasi kubwa za biashara katika maeneo ya uokoaji nishati, nishati endelevu, urudishaji wa vumbi la makaa ya mawe na gesi ya asili."

Kanuni zinazotekelezwa duniani ni kuwa, katika miradi ya ushirikiano ya kupunguza utoaji wa hewa chafu inayosababishwa kuongezeka kwa joto duniani, kampuni na viwanda vya nchi zinazoendelea vikipunguza utoaji wa tani 1 ya hewa ya carbon dioxide, vinasaidiwa dola 10 za kimarekani na kampuni na viwanda vya nchi zilizoendelea. Wataalamu wamekadiria kuwa miradi ya kupunguza utoaji wa hewa inayosababishwa kuongezeka kwa joto nchini China, ina nafasi ya zaidi ya dola za kimarekani bilioni 10 kwenye soko la China. Mbali na hiyo, takwimu za Benki ya Dunia zinaonesha kuwa, hadi kufikia mwezi Septemba mwaka 2006 jumla ya thamani ya makubaliano kuhusu utoaji wa hewa inayosababishwa kuongezeka kwa joto duniani imechukua 84% ya jumla ya thamani ya makubaliano hayo duniani, ambapo ile ya China inaongoza katika soko hilo ikiwa ni 60% ya jumla ya thamani ya makubaliano hayo.

Ingawa soko linalohusu utoaji wa hewa inayosababisha kuongezeka kwa joto duniani lina nafasi kubwa katika siku za baadaye, lakini China inatakiwa kufanya juhudi kubwa katika upanuaji wa utekelezaji wa mbinu hiyo. Kutokana na matakwa ya idara ya usimamizi wa miradi husika ya Umoja wa Mataifa, uanzishaji wa miradi ya kupunguza utoaji wa hewa hiyo unapaswa kupitishwa katika hatua zaidi ya 6 hadi kutangazwa kwenye tovuti iliyothibitishwa na Umoja wa Mataifa, hatua hizo ni pamoja na majadiliano kuhusu uanzishaji wa mradi, kubuni aina ya waraka unaotakiwa, kuidhinishwa na idara husika ya nchi hiyo, kukaguliwa katika idara ya uthibitishaji ya nchi ya tatu na kusaini makubaliano, na muda wa kupitishwa katika hatua hizo 6 ni kiasi cha miaka miwili. Endapo viwanda vya China vinavyotaka kushiriki kwenye utaratibu wa makubaliano hayo, havitajua mchakato na matakwa ya utamaduni huo vitaingia katika hali ya kukiuka kanuni za kimataifa.

Naibu mkurugenzi wa kituo cha utekelezaji wa utaratibu wa ruhusa ya utoaji wa hewa inayosababishwa kuongezeka kwa joto duniani wa mkoa wa Sichuan, Bw. Sun Gaofeng alisema, ni muhimu sana kuzidisha ufahamu wa viwanda vya China kuhusu kanuni za makubaliano hayo.

"Sasa tunahitaji mashirika mengi ya wakala na baadhi ya wataalamu washiriki kwenye mradi huo, jambo ambalo linakwamisha maendeleo ya China katika mradi wa kupunguza utoaji wa hewa inayosababishwa kuongezeka kwa joto."

Hivi sasa mikoa ya Sichuan, Shandong na Jiangsu ya China imeanzisha vituo maalumu kuhusu miradi ya kupunguza utoaji wa hewa hiyo. Vituo hivyo vinashirikisha Benki ya Dunia pamoja na mashirika mengine ya kimataifa ili kutoa misaada ya fedha na teknolojia kwa viwanda vinavyotaka kushiriki kwenye miradi husika.

Tokea mwaka 2012, kuweza au la kwa nchi zinazoendelea kushiriki kwenye makubaliano kuhusu kupunguza utoaji wa hewa inayosababishwa kuongezeka kwa joto duniani, kutaamuliwa na mazungumzo ya kipindi cha pili kuhusu "Mkataba wa Kyoto". Mkurugenzi wa ofisi ya uratibu ya kamati ya maendeleo na mageuzi ya taifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa Bw. Gao Guangsheng alisema, kwa vyovyote vile China itafuata njia ya maendeleo endelevu na kutoa mchango wake kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ya dunia.

Idhaa ya kiswahili 2007-01-30