Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-30 18:15:31    
Ushirikiano kati ya China na Cameroon wazaa matunda tele

cri

Kutokana na mwaliko kutoka kwa na rais Paul Biya wa Cameroon, rais Hu Jintao wa China atafanya ziara rasmi nchini Cameroon mwishoni mwa mwezi huu. Hii ni fursa nyingine tena ya kusukuma mbele uhusiano kati ya pande mbili hizo.

Tokea uhusiano wa kibalozi uanzishwe kati ya nchi mbili uanzishwe mwaka 1971, uhusiano huo umekuwa ukiendelea bila kusita katika uchumi, biashara, ujenzi wa miundombinu, kilimo, elimu na utamaduni.

Katika sekta ya biashara, thamani ya biashara kati ya pande mbili inaongezeka mwaka hadi mwaka. Mwaka 2005 thamani ya biashara kati ya nchi hizo ilifikia dola za kimarekani milioni 210, na katika thamani hiyo Cameroon iliiuzia China bidhaa yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 68 na ilinunua bidhaa yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 142 kutoka China. hivi sasa bidhaa za Cameroon zinazouzwa zaidi nchini China ni pamba, magogo na mbao, na bidhaa zinazonunuliwa kutoka China ni viatu, mashine na matrekta.

Miradi iliyosaidiwa na China ambayo imekwisha kamilika katika mji mkuu wa Cameroon ni jengo la bunge na hospitali ya wanawake na watoto. Jengo la bunge limekuwa moja ya majengo muhimu ya mji mkuu Yaounde, na hospitali ya wanawake na watoto imekuwa ni hospitali muhimu katika mji huo. Mbali na majengo hayo, uwanja wa michezo wa Yaounde ambao sasa unajengwa pia unawavutia sana watu wa sekta mbalimbali. Cameroon ni nchi ambayo wananchi wake wanapenda sana michezo, watu wa Cameroon wana hamu kubwa na uwanja huo na kuuita "Jumba la Michezo la China".

Katika miaka ya hivi karibuni makampuni ya China yameanza kuingia nchini Cameroon na yanatoa mchango katika kuendeleza uchumi na kuinua maisha ya wananchi wa nchi hiyo. Katika miaka ya karibuni mradi ulio mkubwa zaidi ni ujenzi wa barabara uliojengwa na Kampuni ya China ya Barabara na Daraja. Kwa kupitia zabuni kampuni hiyo imepata mradi wa kujenga barabara yenye urefu wa kilomita 12.8 na ilikamilisha ujenzi wa mradi huo mwezi Septemba mwaka 2006, kutokana na kutumia gharama ndogo na ubora mkubwa barabara imesifiwa sana na benki ya dunia, hivi sasa maduka kando ya barabara yamekuwa mengi.

Ushirikiano kati ya nchi mbili umeanza kuenea kwenye sekta ya matibabu, kilimo, elimu na utamaduni.

Kwenye sekta ya matibabu, China imetuma vikundi vya madaktari kwa miaka 31 nchini Cameroon, hivi sasa vikundi hivyo vinatoa huduma kwa watu wa Cameroon katika vituo vitatu.

Kwenye sekta ya kilimo, mwezi Januari mwaka 2006 mkoa wa Shanxi wa China ulisaini mkataba na serikali ya Cameroon. Kwa mujibu wa mkataba huo mkoa wa Shanxi utawekeza dola za kimarekani milioni 60.5 katika miradi ya mashamba ya mpunga, kazi ya kusindika mihogo na ufugaji wa mbuni. Hivi sasa ushirikiano wa ujenzi wa mashamba yaliyosaidiwa na China kwa fedha na teknolojia, na ardhi zilizotolewa na Cameroon ni nzuri.

Kwenye ekta ya elimu, kituo cha kufundisha Kichina kilichoandaliwa na Chuo Kikuu cha Ualimu cha mkoa wa Zhejiang na Chuo Kikuu cha Uhusiano wa Kimataifa cha Yaounde kimeandaa watu 300 wa shughuli za kidiplomasia, kiuchumi na kibiashara tokea kituo hicho kianzishwe mwaka 1997. Mwaka 2004 kituo hicho kilianza kufanya mashindano ya insha za Kichina, washindi wanapewa nafasi ya kuja China kushiriki kwenye mashindano ya mwisho. Mashindano hayo yamekuwa na athari kubwa siku hadi siku.

Kwenye sekta ya utamaduni, mwezi Septemba mwaka 2005 wizara za elimu za China na Cameroon kwa ushirikiano zilianzisha kundi la dansi ya kisasa la Cameroon, walimu wawili wa China wanaendelea kushughulika na uanzishaji na kufundisha wasanii. Hivi sasa kundi hilo limeimarika na lilionesha michezo iliyoshangiliwa katika mkutano wa mawaziri wa fedha wa Afrika uliofanyika mwaka 2006.