Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-31 18:40:36    
Sekta ya kuunda ndege ya China yaweka mkazo katika uvumbuzi wa kujitegemea

cri

Hivi sasa idara husika za sekta ya viwanda vya kuunda ndege ya China zimeonesha rasmi ndege ya kivita ya aina mpya J-10 iliyosanifiwa na China kwa kujitegemea, na kutangaza hali halisi ya utafiti na tekenolojia yake. Baada ya hapo, sekta ya kuunda ndege ya China imefuatiliwa tena na pande mbalimbali duniani.

Hivi karibuni, "mapambano maalum" yalitokea angani mwa uwanja mmoja wa ndege nchini China, ndege mbili zilizotengenezwa na China zilikuwa zinapambana vikali na ndege 4 za maadui. Mweshowe ndege mbili za J-10 zilizosanifiwa na kutengenezwa na China kwa kujitegemea zilishinda mapambano hayo.

Bw. Song Wencong ni msanifu mkuu wa ndege hiyo. Alieleza kuwa, China ilianza utafiti wa ndege ya J-10 mnamo miaka ya 80 ya karne iliyopita, ndege hiyo ni moja ya mafanikio muhimu yaliyopatikana katika sekta ya kuunda ndege ya China kutokana na juhudi zake katika utafiti wa kujitegemea, mafanikio hayo yanainua zaidi uwezo wa ulinzi wa jeshi la anga la China. Bw. Song Wencong alisema:

"mafanikio ya utafiti wa ndege hiyo yana umuhimu mkubwa. Hii inamaanisha kuwa China imekuwa na ndege zake za kisasa za kivita zenyewe. Jambo muhimu ni kwamba ilipoanza kufanya utafiti inapaswa kulenga kiwango cha juu cha teknolojia duniani."

Ndege ya J-10 ikiwa ni ndege ya kivita ya ngazi mpya yenye uwezo wa aina mbalimbali, ina aina mbili yaani ndege ya kiti kimoja na ya viti viwili, na imechanganya usanifu mpya, teknolojia mpya na mbinu mpya za utengenezaji. Katika usanifu wa ndege hiyo, bodi la ndege na mabawa vimechanganywa pamoja, ili kuisaidia ndege hiyo ijsionekani kwenye radar na kuongeza ukubwa wa tanki yake ya mafuta. Usanifu huo umeboresha kwa kiasi kikubwa uwezo wake wa kuruka.

Aidha, ndege ya J-10 pia ina mfumo wa kisasa wa udhibiti wa urukaji. Bw. Song Wencong alieleza kuwa, mfumo huo unaweza kusafirisha ishara ya vitendo vya udhibiti vya rubani na data kuhusu hali halisi ya urukaji kwenye kompyuta ya udhibiti wa urukaji iliyoko kwenye ndege hiyo, baada ya kushughulikiwa na kompyuta hiyo, ishara za udhibiti zikatumwa kwa mabawa mbalimbali ya ndege hiyo. Teknolojia hii inaifanya ndege hiyo iweze kujikagua matatizo na kuunganisha zenyewe sehemu zisizo na matatizo ili kuihakikisha inafanya kazi bila matatizo.

Imefahamika kuwa, hivi sasa ndege ya kivita ya J-10 imeanza kutumika kwa wingi katika jeshi la anga la China. Mwenyekiti wa bodi wa Kampuni ya kuunda ndege ya Chengdu inayowajibika kuunda ndege za J-10 Bw. Luo Ronghuai alisema, ndege hiyo si kama tu ni mafanikio ya sekta ya viwanda vya kuunda ndege ya China, bali pia inasukuma mbele maendeleo ya sekta nzima ya viwanda ya China. Bw. Luo Ronghuai alisema:

"mafanikio ya usanifu wa ndege ya J-10 ni alama kuwa sekta ya kuunda ndege ya China imekamilisha mfumo wake wa utafiti kwa kujitegemea. Hili ni jambo muhimu. Nadhani kuwa kwa sekta ya kuunda ndege ya China na shughuli kuhusu teknolojia za majaribio, jambo hilo hata lina umuhimu mkubwa zaidi kuliko ndege hiyo yenyewe."

Mbali na hayo, katika mwaka mmoja uliopita, mafanikio mengi yakiwemo ndege ya J-10 yalitokea, na sekta ya kuunda ndege ya China imepata maendeleo matatu makubwa katika teknolojia za ulinzi.

Iemfahamika kuwa, maendeleo hayo matatu ni kuwa mafanikio ya usanifu wa ndege ya J-10 ni maendeleo ya kihistoria ya ndege za kivita za China kutoka ngazi ya pili hadi ngazi ya tatu; mafanikio ya usanifu wa ijini ya Taihang ni maendeleo ya ijini ya ndege za kivita kutoka ngazi ya pili hadi ngazi ya tatu; na mafanikio ya usanifu wa makombora ya anga kwa anga ya aina mpya ni alama ya maendeleo ya makombora ya anga kwa anga ya China kutoka ngazi ya tatu hadi ngazi ya nne. Naibu maneja mkuu wa kampuni ya kwanza ya kundi la kuunda ndege la China Bw. Di Ruguang alisema:

"kupatikana kwa maendeleo hayo matatu na kuboreshwa kwa mfumo wa udhibiti ulioko kwenye ndege, kumeifanya China iwe nchi ya nne duniani yenye uwezo wa kutafiti na kusanifu ndege za kisasa za kivita, ijini za ndege na makombora. Maendeleo hayo yamepunguza pengo kati ya China na nchi zilizoendelea. Mbali na hayo, mafanikio mengine kadhaa katika teknolojia muhimu na za kisasa yamepatikana. Teknolojia nyingi zaidi zimetumika katika uzalishaji mali. Aidha, China pia imejenga maabara mengi ya taifa. Uvumbuzi wa kujitegemea umetoa michango muhimu kwa ujenzi wa ulinzi wa kisasa na ujenzi wa uchumi wa taifa wa China."

Mbali na mafanikio katika vifaa vya ulinzi wa taifa, sekta ya uundaji ndege ya China pia imeshikilia uvumbuzi kwa kujitegemea katika utafiti na usanifu wa ndege za kiraia.

Bw. Di Ruguang alisema, ndege ya aina mpya inayotumiwa kwenye matawi ya njia kuu ARJ21 ambayo ilisanifiwa na kampuni hiyo imeanza kufanyiwa majaribio. Alisema, ndege hiyo si kama tu ina chumba kikubwa zaidi kuliko ndege nyingine za aina hiyo, bali pia inaweza kuruka na kutua katika uwanja wa ndege ulioko kwenye uwanda wa juu wa magharibi mwa China na kusafiri kwenye njia zenye utatanishi. Hivi sasa, ndege 71 ya aina hiyo imeagizwa. Kutokana na mpango uliowekwa, ndege ya ARJ21 itaruka kwa mara ya kwanza mwezi Machi mwaka kesho, na kutoa huduma kwa kwa wasafiri mwaka 2009.

Aidha, ndege ya aina nyingine inayotumiwa kwenye matawi ya njia kuu Xinzhou 60 ambayo ilisanifiwa na China hivi sasa imeuzwa kwa wingi kwa nje. Bw. Di Ruguang alieleza:

"katika shughuli za kuunda ndege za kiraia, ndege 71 aina ya ARJ21 inayotumiwa katika matawi ya njia kuu ambayo ilisanifiwa na kampuni ya kwanza ya kuunda ndege ya China zimeagizwa. Mwaka 2006, ndege 62 aina ya Xinzhou 60 inayotumiwa katika njia za matawi ziliagizwa na nchi 8 za Zimbabwe, Laos, Congo, Nepal, Indonesia, Cuba na Fiji katika mabara ya Asia, Afrika, Latin na Oceania."

Kutoka ndege za kijeshi hadi ndege za kiraia, sekta ya kuunda ndege ya China imejenga mfumo kamili wa utafiti, usanifu, utengenezaji na majaribio, na maabara ya taifa na miundombinu mingine ya kufanya majaribio. Wachambuzi wa sekta hiyo wanaona kuwa, maendeleo hayo yote yatakuwa nguvu muhimu ya kusukuma mbele ujenzi wa ulinzi wa kisasa na ongezeko endelevu la uchumi wa China.