Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-31 19:55:13    
Mapishi ya tambi

cri

Mahitaji:

Kamba-mwakaje gramu 20, uyoga gramu 10, maharagwe gramu 10, yai moja, nyanya moja, tambi gramu 50, chumvi kijiko kimoja, chembechembe za kukoleza ladha kijiko kimoja, mchuzi wa sosi vijiko viwili.

Njia:

1. kata maharagwe yawe vipande, tia vipande vya vitunguu maji, vitunguu saumu na tangawizi, korogakoroga tia vipande vya maharagwe, chumvi na chembechembe za kukoleza ladha korogakoroga yapakue. Kata nyanya na uyoga uwe vipande. Koroga yai, pasha moto na mimina mafuta kwenye sufuria, halafu mimina yai, likaange upande mmoja halafu endelea kukaanga upande mwengine. Pakua halafu ulikate liwe vipande.

2. chemsha maji kwenye sufuria halafu weka tambi kwenye sufuria chemsha kwa mvuke kwa dakika 10, mimina mafuta kidogo kwenye sufuria, tia tambi kwenye sufuria korogakoroga kwa dakika moja halafu ipakue.

3. pasha moto tena, mimina mafuta kidogo, tia kamba-mwakaje korogakoroga halafu tia vipande vya nyanya na uyoga, tia chumvi na chembechembe za kukoleza ladha, korogakoroga na tia tambi korogakoroga. Zima moto, tia vipande vya maharagwe na yai, korogakoroga. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.