Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-02-01 17:19:26    
China ilivyoweka lengo kuu la kujenga jamii yenye masikilizano

cri

Katika mwaka 2006 tuliouaga hivi karibuni, China ilipata ongezeko kubwa la uchumi kiasi kwamba, pato la taifa katika kipindi cha miezi 9 ya kwanza ya mwaka 2006 liliongezeka kwa wastani wa asilimia 10.7. Hata hivyo maendeleo yanayowavutia watu wengi si maendeleo katika sekta ya uchumi tu, bali ni kutokana na serikali ya China kuweka bayana lengo la kujenga jamii yenye masikilizano na tayari imechukua hatua halisi. Sasa juhudi hizo zimeanza kuzaa matunda.

Bw. Sun Jianhua mwenye umri wa miaka 30 ni mkulima, anaishi huko Ningyang, mkoani Shandong, mashariki mwa China. Katika miaka minane iliyopita, alikuwa anafanya kazi mjini. Bw. Sun alisema katika miaka ya hivi karibuni, serikali ilikuwa imetoa sera zinazowanufaisha wakulima wanaofanya kazi mijini, sasa pato lake limeongezeka kutoka Yuan mamia kadhaa kwa mwezi hadi Yuan zaidi ya elfu 2 kwa mwezi na watoto wa wakulima wanasoma katika shule za mijini bila kulipa ada za nyongeza. Hata hivyo Bw. Sun alieleza vitu ambavyo bado haridhiki navyo.

Alisema "Sisi hatuna bima ya matibabu, tukiumwa sana tunashindwa kulipa matibabu. Tena hatulindwi na bima ya uzee, tuna wasiwasi kuhusu maisha baaada ya kuzeeka. Aidha tunabadilisha ajira mara kwa mara, kama tukipata ajira mpya taratibu za kuendeleza bima zinatusumbua sana."

Wasiwasi wa Bw. Sun utaweza kuondolewa hivi karibuni. Serikali ya China imetambua kuwa, sambamba na ongezeko la kasi la uchumi, matatizo mbalimbali yameibuka kama vile mifumo isiyokamilika ya huduma za jamii isiyokamilika na pengo la maendeleo linalozidi kupanuka kati ya sehemu tofauti za China. Ili kuleta maendeleo ya madhubuti ya jamii, miaka mitatu iliyopita chama cha kikomunisti cha China ambacho ni chama tawala nchini China kilitangaza mkakati wa kujenga jamii ya ujamaa yenye masikilizano, na kutoa uamuzi rasmi kwenye kikao cha chama hicho mwaka 2006.

Je, nini maana ya jamii yenye masikilizano? Kwa mujibu wa ufafanuzi wa chama hicho, katika jamii yenye masikilizano haki na maslahi ya wananchi yanaheshimiwa na kulindwa kihalisi; mfumo wa huduma za jamii unaowanufaisha wananchi wote wanaoishi mijini na vijijini uwe umekamilika kimsingi; mwelekeo wa kuzidi kwa pengo la maendeleo kati ya miji na vijiji na kati ya sehemu tofauti utakuwa umezuiliwa; mfumo wa msingi wa utoaji huduma kwa jamii utakamilishwa; kiwango cha elimu, sayansi na utamaduni cha wananchi wote kitakuwa kimeinuka kwa dhahiri; na hali ya mazingira itakuwa imeboreshwa kwa udhahiri.

Profesa Ye Duchu wa chuo cha chama chama kimonunisti cha China alieleza ufahamu wake kuhusu lengo hilo la kujenga jamii yenye masikilizano, akisema  "lengo hilo lina pointi 9 na linahusu pande 9. Kinachonivutia ni kwamba, kulinda haki ya wananchi kumewekwa kuwa ni lengo la kwanza, yaani ni lazima kuheshimu, kulinda na kuhakikisha haki na maslahi ya wananchi. Kati ya vipengele hivyo 9, lengo hilo ni la maana."

Profesa Ye alisema katika juhudi za kujenga jamii yenye masikilizano, kukamilisha mfumo wa huduma za jamii ni sehemu muhimu ya kulinda haki za wananchi. Katika kipindi cha miaka zaidi ya 20 iliyopita tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji milango, imeanzisha mfumo wa huduma za jamii unaojumuisha bima ya ueeni, bima ya matibabu na bima ya kukosa ajira. Lakini mfumo huo una kasoro fulani, kwa mfano huduma zinazotolewa zimeshindwa kukidhi matakwa ya wananchi, na wananchi wachache wamenufaika na mfumo huo. Hivi sasa idara za kazi na huduma za jamii zinachukua hatua za kukabiliana na kasoro hizo.

Naibu waziri mkuu wa China Bw. Huang Ju hivi karibuni kwenye mkutano mmoja alisema "Tunapaswa kupata ufumbuzi wa matatizo makubwa yanayoukabili mfumo wa huduma za jamii, na kuanzisha mfumo utakaoleta maendeleo endelevu. Tunajitahidi kupanua wigo wa mfumo huo ili wananchi wengi zaidi wanufaike, aidha inapaswa kuvutia mitaji ya pande mbalimbali, kuimarisha usimamizi wa mfumo huo na kuwapa wananchi huduma bora."

Kwa mfano wa Bw. Sun na wakulima wenzake wanaofanya kazi mijini, hivi sasa idara zinazoshughulikia mambo ya kazi na huduma za jamii zinajitahidi kuwasaidia kutatua kero mbalimbali, ikiwa ni pamoja na tatizo linalowakabili la kupata matibabu wakipata majeruha kazini, namna ya kuwahakikisha wanapata huduma za afya na matibabu, na kuwashirikisha kwenye bima ya uzeeni. Kwa mujibu wa sera mpya iliyotolewa na serikali ya China, Bw. Sun anaweza kupata bima ya matibabu inayolipwa na kampuni anayofanya kazi, na suala la bima ya uzeeni pia linatarajiwa kutatuliwa hivi karibuni.

Katika juhudi za China kujenga jamii yenye masikilizano, suala jingine kubwa ni kutokuwepo kwa uwiano wa maendeleo kati ya miji na vijiji na kati ya sehemu mbalimbali.

Idhaa ya kiswahili 2007-02-01