Alasiri ya Tarehe 2 Februari Rais Hu Jintao ambaye yuko Sudan kwa ziara akiambatana na rais Omar Al Bashir wa Sudan alitembelea Kiwanda cha kusafisha mafuta cha Khartoum. Kiwanda hicho cha kisasa kilijengwa kutokana ushirikiano kati ya China na Sudan. Mwandishi wetu wa habari alisema:
Mwaka 1995, Rais Bashir wa Sudan aliitembelea China, ziara yake hiyo ilifungua mwanzo wa ushirikiano kati ya China na Sudan katika sekta ya mafuta. Mwezi Machi mwaka 1997, China na Sudan zilisaini rasmi makubaliano ya ushirikiano, tangu hapo nchi hizo mbili zikashirikiana na kubeba pamoja jukumu la kuanzisha shughuli za mafuta nchini Sudan. Mwaka 2000, Kampuni ya mafuta na gesi ya asili ya China na Wizara ya nishati na madini ya Sudan zilishirikiana kujenga kiwanda cha kusafisha mafuta cha Khartoum, ujenzi wa kiwanda hiki ulikamilika mwaka 2006, ambapo mfumo kamili wa viwanda vya kisasa vya mafuta ukakamilika nchini Sudan.
Rais Hu Jintao alipotembelea kiwanda hicho alisikiliza kwa makini ujulisho kuhusu kiwanda hicho, na baadaye alitoa hotuba akisema:
Ushirikiano kati ya China na Sudan katika sekta ya mafuta umekuwepo kwa miaka 10. Katika miaka 10 iliyopita, ushirikiano huo uliendelea vizuri na kupata mafanikio kemkem, pamoja na ufanisi mzuri wa kiuchumi na ufanisi wa kijamii. Ushirikiano huo si kama tu unasaidia maendeleo ya viwanda vya China, bali pia umeihimiza Sudan ikamilishe ujenzi wake wa mfumo kamili wa viwanda vya mafuta, ambao umechangia kazi za Sudan za kutumia kihalali maliasili, kuongeza nafasi za ajira, kuongeza mapato ya ushuru, na kubadilisha nguvu yake ya maliasili kuwa nguvu ya kuendeleza uchumi. Ukweli wa mambo umeonesha kuwa, ushirikiano kati ya China na Sudan unastahiki kusifiwa kuwa ni mfano wa kuigwa wa ushirikiano kati ya kusini na kusini.
China ni nchi kubwa kabisa inayoendelea duniani, na Bara la Afrika ni bara lenye nchi nyingi kabisa zinazoendelea duniani. Rais Hu Jintao alisema kuwaletea wananchi wa Afrika maslahi halisi ni kanuni ya kimsingi ya makampuni ya China kuanzisha shughuli barani Afrika na kufanya ushirikiano na makampuni ya Afrika. Rais Hu alisema:
Serikali ya China siku zote inayatia moyo na kuyaunga mkono makampuni ya China yenye nguvu halisi na sifa nzuri, yaende kwenye nchi za Afrika ikiwemo Sudan kuanzisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara wa aina mbalimbali, tena serikali ya China inayataka makampuni ya China yashikilie kanuni za kusaidiana na kunufaishana, ili kupata maendeleo ya pamoja, na pia yanatakiwa kutilia maanani heshima yao na sifa za kazi zao, kujitahidi kuishi kwa masikilizano na watu wa sehemu wanakoishi barani Afrika, kubeba kwa hiari jukumu la jamii, kufanya mambo mengi zaidi yanayoweza kuzisaidia nchi za Afrika ziongeze uwezo wa kujiendeleza, na kuwasaidia wananchi wa Afrika kuboresha maisha yao.
Rais Bashir wa Sudan alipotoa hotuba alieleza umuhimu mkubwa wa ushirikiano kati ya China na Sudan katika sekta ya mafuta. Alisema:
Ushirikiano kati ya Sudan na China kwenye sekta ya mafuta hauna maslahi yoyote ya maslahi ya binafsi katika mambo ya kisiasa, na hauna shinikizo lolote la kisiasa, ushirikiano huo umezifanya nchi nyingi za Afrika na za kiarabu zitupie macho kwa China.
Idhaa ya Kiswahili 2007-02-03
|