Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-02-06 15:55:59    
China yaongeza masharti kwa magari yanayosafirishwa kwa nje

cri

Kuanzia tarehe 1 mwezi Machi mwaka huu, China itaanza kutekeleza utaratibu wa kuomba kibali kwa magari yanayosafirishwa kwa nchi za nje, ukiagiza kuwa ni kampuni bora na za kutoa huduma kamili kwa magari yanayouzwa tu, ndizo zinazoweza kupewa leseni ya kusafirisha magari  nchi za nje. Wataalamu wa magari wamesema kutolewa kwa kanuni hiyo kunaonesha kuwa, China imeongeza masharti kwa magari yanayosafirishwa kwa nchi za nje, ambapo hali ile ya kushiriki kwenye ushindani kwa bei ya chini itabadilika. Wataalamu pia walishauri kuwa, kampuni za magari ziimarishe nguvu ya utafiti na uvumbuzi na kuinua ubora wa magari ili kuwa na nguvu ya ushindani kwenye soko la kimataifa.

Kutumia utaratibu wa leseni kwa magari yanayosafirishwa kwa nchi za nje ni jambo moja muhimu katika utekelezaji wa kanuni mpya za usimamizi kwa magari yanayosafirishwa nchi za nje. Kanuni hizo mpya zinataka kampuni zinazosafirisha magari kwa nje, ziwe na uwezo wa kutoa huduma kulingana na magari yake yanayosafirishwa nchi za nje, na kutaka kuunda mfumo kamili wa utoaji huduma kwenye masoko muhimu ya magari.

Katika mwaka 2006, China ilisafirisha magari zaidi ya laki 3 kwa nchi za nje, nakuwa mwaka ambao China ilisafirisha magari mengi zaidi. Lakini kampuni nyingi za magari hazijawa na mfumo imara wa kutoa huduma kwa magari yaliyouzwa, hali ambayo imeathiri matumizi ya magari ya wateja wa nchi za nje, vilevile imeathiri sifa za magari ya China katika nchi za nje.

Mratibu mkuu wa taasisi ya uhandisi wa magari ya China Bw. Zhang Xiaoyu alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema, kanuni mpya zilizotolewa safari hiyo zitaondoa kampuni zile zinazojua kuuza magari na kutofahamu kutoa huduma kwa magari yaliyokwishauzwa.

"Kwa bidhaa ya magari, licha ya kuzingatia ubora wake, utoaji huduma ni muhimu sana, hususan kutoa vipuri vinavyohitajika katika matengenezo yake. Hivi sasa, kampuni zetu nyingi zinatoa huduma kwa kutegemea wafanyabiashara wa magari wa huko nchi za nje. Tukitupia macho mbali, ni vigumu kukidhi mahitaji ya wateja, na ni rahisi kuwaletea wateja baadhi ya matatizo. Hivyo hatuna budi kuanzisha mfumo kamili wa huduma kwa kushirikiana na wafanyabiashara wanaozalisha au kuuza magari wa huko nchi za nje."

Kwa hivi sasa tatizo lingine kubwa kwa soko la magari ya China yanayosafirishwa kwa nchi za nje ni kuwa kampuni zinazoshughulikia usafirishaji wa magari kwa nje, ni nyingi kupita kiasi, ambapo imeleta ushindani usio na utaratibu. Takwimu zinaonesha kuwa, mwaka jana zaidi ya kampuni 1000 zilishiriki katika usafirishaji magari kwa nchi za nje, hususan ni kuwa baadhi ya kampuni hizo ili kujipatia faida, zilifanya ushindani kwa kushusha sana bei, hali ambayo iliathiri vibaya maslahi ya kampuni na sekta ya magari ya China. Ili kutatua matatizo hayo, katika siku za baadaye China itafanya usimamizi kuhusu sifa za kampuni za magari, na kutekeleza utaratibu wa kutoa leseni ya kusafirisha magari kwa nchi za nje.

Mratibu mkuu wa taasisi ya uhandisi wa magari ya China Bw. Zhang Xiaoyu alisema, kanuni mpya zinazotolewa sasa hiyo zimeongeza masharti kwa magari ya China yanayosafirishwa nchi za nje, hatua ambayo inahakikisha ubora wa magari hayo. Hivi sasa, mengi ya magari ya China yanayosafirishwa kwa nchi za nje ni malori na magari ya bei rahisi, na yalisafirishwa kwa baadhi ya nchi zinazoendelea, wakati magari yaliyosafirishwa kwenye masoko ya Ulaya na Marekani ni machache sana. Bw. Zhang Xiaoyu alisema, kampuni za magari za China zikitaka kubadilisha hali hiyo, na kuinua usafirishaji magari kwa masoko ya Ulaya na Marekani, zinapaswa kuchukua hatua mpya za kutimiza masharti magumu ya masoko ya Ulaya na Marekani kuhusu teknolojia, uokoaji wa nishati na moshi unaotoka kwenye magari.

Aidha, Bw. Zhang Xiaoyu alizishauri kampuni za magari za China zifanye uvumbuzi zaidi, wala siyo kuiga kampuni za nchi za nje ili kuimarisha nguvu ya ushindani kwenye masoko ya magari duniani. Ikilinganishwa na baadhi ya makampuni maarufu ya kimataifa yaliyoanzishwa zaidi ya miaka 100 iliyopita, kampuni za magari za China zinapaswa kujenga sifa za magari yake.

Idhaa ya kiswahili 2007-02-06