Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-02-07 15:00:31    
Mpango wa 863 wahimiza maendeleo ya teknolojia ya juu nchini China

cri

Kwa wachina, nambari ya 863 ina maana maalum. Kwa kuwa mpango wa sayansi na teknolojia unaoitwa 863 ambao umeinua kikamilifu kiwango na uwezo cha utafiti wa kisayansi na kiteknolojia wa China katika miaka 20 iliyopita, na umepunguza pengo kati ya China na nchi zilizoendelea duniani.

Katika miaka ya 80 ya karne iliyopita, mkondo wa mageuzi ya teknolojia mpya za upashanaji wa habari na viumbe ulitokea kote duniani. Sekta ya teknolojia ya juu imekuwa mbinu muhimu katika ushindani wa kimataifa. nchi fulani ikikuwa na teknolojia ya juu, itachukua nafasi ya mbele kwenye sekta ya sayansi na teknolojia kote duniani.

Kutokana na hali hiyo, mwaka 1986, serikali ya China imeanzisha rasmi mpango wa utafiti wa teknolojia ya juu, yaani mpango wa 863. mpango huo uliweka mkazo katika kuendeleza teknolojia kuhusu sekta nane yaani viumbe, safari za anga ya juu, upashanaji wa habari, Laser, kujiendesha yenyewe, nishati na nyenzo mpya na teknolojia kuhusu mambo bahari. Waziri wa sayansi na teknolojia wa China Bw. Xu Guanhua alieleza kuwa, katika miaka 20 tangu mpango wa 863 ulipoanza kutekelezwa, umepata maendeleo makubwa katika teknolojia nyingi muhimu, umepata hataza zaidi ya 8000 za China na za nje, na kuweka vigezo vya kitaifa zaidi ya 1800. Bw. Xu Guanhua alisema:

"katika miaka 20 iliyopita, kwa jumla China ilitenga yuan bilioni 33 kwa ajili ya mpango huo, na kulikuwa na watafiti zaidi ya laki 1. 5 walioshiriki kwenye mpango huo. Mafanikio yaliyopatikana katika mpango huo yametoa michango muhimu katika kuinua uwezo wa uvumbuzi wa China, kuinua uwezo wa jumla wa ushindani wa China, na kuimarisha zaidi imani ya wananchi kwa taifa letu."

Bila shaka, mpango wa 863 ni moja ya miradi mikubwa ya sayansi tangu China mpya ilipoanzishwa. Maendeleo ya teknolojia nyingi muhimu yaliyopatikana katika mpango huo yameisaidia China kutafiti na kuzalisha bidhaa nyingi zenye hataza katika sekta mbalimbali za teknolojia ya juu zikiwemo dawa za viumbe, upashanaji wa habari na nyenzo mpya. kompyuta ya hali ya juu ya "Shu Guang" ni moja ya alama ya mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya teknolojia ya upashanaji wa habari.

Msanifu mkuu wa kompyuta hiyo Bw. Sun Ninghui alieleza kuwa, katika miaka ya 90 ya karne iliyopita, kutokana na uungaji mkono wa mpango wa 863, kompyuta ya hali ya juu inayoitwa Shuguang No.1 ilikamilika na imekuwa mafanikio ya kwanza yaliyopatikana China katika sekta ya utafiti wa kompyuta ya hali ya juu. Baada ya hapo, kila baada ya miaka kadhaa, shughuli za utafiti wa kompyuta ya hali ya juu nchini China zitapiga hatua kubwa, kasi ya kuhesabu imeongezeka kutoka mara bilioni 2.5 kwa sekundi, na kutoka mara bilioni 100 kwa sekondi, hadi mara bilioni 400 kwa sekondi, mpaka mara trilioni 10 kwa sekondi ya hivi sasa. Bw. Sun alisema:

"hivi sasa kote duniani kuna nchi tatu tu zinazoweza kutengeneza na kutumia kompyuta ya hali ya juu kama hiyo, yaani Marekani, Japan na China. Tunatumai kuwa China itaweza kutengeneza kompyuta yenye uwezo wa kuhesabu mara trilioni mia moja kwa sekondi ifikapo mwaka 2008."

Mbali na hayo, kompyuta hizo pia zinatumiwa kwenye miradi mingine ya upashanaji wa habari katika mpango wa 863, na mmojawapo ni mradi wa mtandao wa Grid wa taifa wa China.

Kwa ufupi, mradi wa mtandao wa Grid ni kuifanya mtandao nzima wa Internet kuwa kompyuta moja kubwa. Wataalamu wanaona kuwa, mtandao wa Grid unawakilisha teknolojia ya ngazi mpya ya mtandao wa Internet, teknolojia hiyo itafanya raslimali mbalimbali za Internet, zikiwemo raslimali za hisabiti, akiba, software na ujuzi, ziweze kutumikwa kwa pamoja. Hivi sasa, kwa kutumia kompyuta ya hali ya juu ya "Shuguang", mfumo wa Grid wa China umeanzisha vituo 8 vya uunganishaji katika miji mbalimbali ikiwemo Beijing, Shanghai na Hongkong, na unatoa huduma kwa shughuli za uchunguzi wa jiografia, uundaji wa ndege, utabili wa hali ya hewa, sekta ya misitu, elimu na mawasiliano ya mijini. Ofisa wa mradi wa utafiti wa kompyuta wa hali ya juu na software husika katika mpango wa 863 Bw. Qian Depei alieleza:

"kinadharia mtandao wa Grid unaweza kufanya raslimali mbalimbali za kompyuta ziweze kutumika kwa pamoja, zikiwemo uwezo mkubwa wa kuhesabu, akiba kubwa ya data, na uwezo wa kutafuta taarifa mmablimabli kwenye mtandao wa Internet. Kwa mfano, wakati wa kufanya uchunguzi wa kijiografia wa kutathmini raslimali ya maji iliyo chini ya ardhi, tukitumia mbinu ya kawaida, kazi hiyo itachukua muda wa miaka mitatu, lakini kama tukitumia mtandao wa Grid tutaweza kukusanya data za kijiografia za sehemu mbalimbali nchini China na kisha kuzisambaza data hizo ili zishughulikiwe katika kompyuta zilizoko sehemu mbalimbali kote nchini, kwa kutumia teknolojia hiyo, kazi hiyo inachukua muda wa miezi mitatu tu."

Imefahamika kuwa, mpango wa 863 pia utajitahidi kusukuma mbele utungaji wa vigezo vya kitekonolojia vya China, na kuandaa wataalamu na makundi ya uvumbuzi, ili kuhimiza moja kwa moja teknolojia za upashanaji wa habari zitumike kwa viwanda na kusukuma mbele ujenzi wa miradi muhimu ya matumizi ya teknolojia husika, na kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii ya China.

Mbali na hayo, teknolojia ya viumbe pia ni sekta muhimu iliyopata mafanikio makubwa kutokana na uungaji mkono wa mpango wa 863. tangu mpango huo uanze kutekelezwa, sekta ya teknolojia ya viumbe ya China ilithibitisha lengo la kuweka mkazo katika miradi ya kilimo na dawa za viumbe, hasa katika aina mpya za mazao ya kilimo, dawa, chanjo na matibabu mapya ya jini, na mradi wa utafiti wa protini.

Katika miaka 20 iliyopita, teknolojia ya viumbe ya China imepata maendeleo makubwa na imeumba sekta mpya ya teknolojia hiyo. Hivi sasa, pato la jumla la sekta hiyo ya China limefikia yuan bilioni 360 kwa kila mwaka.

Kutokana na uungaji mkono wa mpango wa 863, wanasayansi wa China pia walishiriki kwenye mradi wa ushirikiano wa kimataifa wa utafiti wa jini za binadamu, na kufanikisha kazi ya kuthibitisha utaratibu wa asilimia 1 ya jini za binadamu iliyokabidhiwa na mpango wa mradi huo. Hii inamaanisha kuwa shughuli za utafiti wa jini nchini China zinaenda sambamba na kiwango cha kimataifa. Bw. Yu Jun aliyeshiriki kwenye utafiti huo kwa muda mrefu alisema, kama kila mtu akiweza kuthibitishwa jini zake, atajua hatari kwake kupatwa magonjwa mbalimbali yanayohusiana na jini, yakiwemo shinikizo kubwa la damu, ugonjwa wa kisukari na saratani ya matiti, na ataweza kujikinga kwa ufanisi dhidi ya magonjwa hayo. Kwa hivyo kuwawezesha wananchi wa China wajikinge dhidi ya magonjwa kwa kutumia teknolojia hiyo kumekuwa lengo muhimu la utafiti huo. Bw. Yu Jun alisema:

"mwaka 1984, ziligharamiwa dola za kimarekani bilioni 3 kwa kutambua jini za mtu mmoja, mwaka 2004 ilihitaji dola za kimarekani milioni 30, kwa mwaka 2006 garama hizo ni dola za kimarekani milioni 1.5, na lengo letu ni kupunguza garama hizo kufikia dola elfu moja katika miaka kadhaa ijayo."

Kwa kweli kila mafaniko yaliyopatikana katika sekta ya teknolojia za juu ya China yanahusiana na mpango wa 863. uchunguzi husika umeonesha kuwa, pengo kati ya kiwango cha utafiti wa setka za teknolojia ya juu zilizoungwa mkono na mpango huo na kiwango cha kimataifa limepungua kidhahiri, na asilimia 60 ya teknolojia imefikia au kukaribia kiwango cha juu duniani.