Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-02-07 16:39:04    
Serikali ya mkoa wa Zhejiang, China yahimiza maendeleo ya shughuli za afya vijijini

cri

 

Habari zilizotolewa kwenye mkutano wa kazi ya usimamizi wa shughuli za afya wa mkoa wa Zhejiang, China zinasema, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2007 kazi ya usimamizi na utekelezaji wa sheria kwa shughuli za afya vijijini zitafanyika kwenye sehemu zaidi ya asilimia 98 za mkoa huo, na watu wanaoishi vijijini watapata uhakikisho wa usalama wa afya kama watu wa mijini.

Habari hizo zinasema hivi sasa kazi za kuanzisha mfumo wa usimamizi kwa shughuli za afya vijijini zinaendelea katika sekta mbalimbali mkoani Zhejiang. Hadi sasa idara 102 za usimamizi wa shughuli za afya za ngazi ya kimkoa, miji na wilaya zimeanzishwa. Wafanyakazi wanaoshughulikia usimamizi huo wamefikia 3390, na kila watu elfu kumi vijijini wanahudumiwa na mtumishi mmoja. Serikali imetenga fedha zaidi ya renminbi yuan milioni 25 kutoka kwenye bajeti ya mkoa, na kutoa magari zaidi ya 100 kwa idara za usimamizi kwa shughuli za afya, hatua hizo zimekidhi vizuri mahitaji ya kazi ya usimamizi kwa shughuli za afya.

Ili kuwawezesha watu wanaoishi vijijini kupata uhakikisho wa usalama wa afya kama watu wa mijini, serikali ya mkoa wa Zhejiang ilitilia mkazo kazi ya usimamizi kwa shughuli za afya vijijini na kuchukua hatua mbalimbali zikiwemo, kuanzisha ofisi za idara za usimamizi kwa shughuli za afya za ngazi ya wilaya kwenye vijiji na tarafa, na kumteua mfanyakazi mmoja kuwa mwendeshaji wa shughuli za afya za umma, kumchagua mtu mmoja kushughulikia mawasiliano, uratibu na uendeshaji wa shughuli za afya kwenye kila kijiji. Hivi sasa wilaya 55 za mkoa wa Zhejiang zimeanzisha ofisi ya usimamizi wa shughuli za afya kwenye vijiji na tarafa, na wilaya hizo zinachukua zaidi ya asilimia 60 katika wilaya zote za mkoa huo zinazopangwa kuanzisha ofisi hizo vijijini. Ofisi hizo zina waendeshaji zaidi ya 1400 wa shughuli za afya kwenye tarafa, na wafanyakazi wengine elfu 33 wanaoshughulikia mawasiliano ya kiafya kwenye vijiji. Mbali na hayo, serikali imeanzisha mfumo wa usimamizi na utoaji misaada kwa ajili ya shughuli za afya vijijini. Hadi sasa vituo vikuu 1200 na vituo 6789 vya huduma za afya kwenye miji na vijiji vimeanzishwa mkoani Zhejiang, na vituo hivyo vina madaktari elfu 26. Kazi za kutoa huduma za aina mbalimbali za afya kwa watu wa vijijini zimefanyika vizuri.

Kutokana na mpango uliopo, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2007, asilimia zaidi ya 80 za miji na wilaya mkoani Zhejiang zitamaliza kazi ya kuanzisha idara za usimamizi kwa shughuli za afya, kiasi cha usimamizi na utekelezaji wa sheria kwa shughuli za afya vijijini kitafikia zaidi ya asilimia 98, kiasi cha kushughulikia matukio ya chakula chenye sumu kufikia zaidi ya asilimia 98, na asilimia ya mikahawa na sehemu nyingine za umma zinazofikia vigezo vya afya itakuwa zaidi ya 75.

Idhaa ya Kiswahili 2007-02-07