Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-02-07 19:48:52    
Rais Hu Jintao ahudhuria mazungumzo na wawakilishi wa kampuni za China zilizoko barani Afrika

cri

Kabla ya kuwasili nchini Afrika ya Kusini, rais Hu Jintao wa China tarehe 6 mwezi Februari huko Namibia alishiriki kwenye mazungumzo na wawakilishi wa kampuni zenye mitaji ya China zilizoko barani Afrika, na alitoa hotuba muhimu. Rais Hu Jintao alisema lengo la ziara yake barani Afrika ni kufanya marafiki wa Afrika na jumuiya ya kimataifa waone kuwa China inatekeleza ahadi ilizotoa, kufuatilia ufanisi na moyo wa dhati na usawa katika miradi ya ushirikiano na nchi za Afrika.

China ni mwenzi muhimu wa Afrika katika shughuli za biashara, takwimu mpya zilizotolewa na wizara ya biashara ya China zinaonesha kuwa, thamani ya biashara kati ya China na nchi za Afrika ilifikia dola za kimarekani bilioni 55.5 mwaka 2006 ikiwa ni ongezeko la 40% kuliko mwaka uliotangulia. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2006, jumla ya thamani ya uwekezaji wa China katika nchi 49 za Afrika ilifikia dola za kimarekani bilioni 6.64. Kabla ya kumaliza ziara ya kiserikali nchini Namibia, tarehe 6 asubuhi rais Hu alikuwa na mazungumzo na wawakilishi wa kampuni za China zilizoko barani Afrika. Wawakilishi wa kampuni ya mafuta ya petroli na gesi ya asili ya China, kampuni ya ujenzi wa majengo ya China, kampuni ya Hisense, kampuni ya dawa ya Huali na kampuni ya CIETCO walitoa maelezo kwenye mazungumzo kuhusu shughuli zao barani Afrika. Rais Hu alisikiliza maelezo yao kwa makini, na alitoa maoni na mapendekezo na kuwasifu kuwa ni wachina wenye ufahamu mwingi kuhusu Afrika. Alisema,

"Katika mwanzo wa mwaka mpya, nimechagua kufanya ziara barani Afrika, lengo langu ni kuimarisha urafiki wa jadi kati ya China na Afrika, kutekeleza uamuzi wa mkutano wa Beijing wa baraza la ushirikiano wa China na Afrika, kupanua ushirikiano, kuhimiza maendeleo ya pamoja na kufanya marafiki wa Afrika na jumuiya ya kimataifa waone China ni nchi inayotekeleza ahadi ilizotoa, kufuatilia ufanisi, moyo wa dhati na usawa."

Rais Hu Jintao alisema, nchi nyingi zinazoendelea ziko barani Afrika, bara ambalo lina umuhimu mkubwa wa kimkakati kwa China kuendeleza uhusiano wa kirafiki na ushirikiano.

"Maendeleo ya mwafaka na yenye ulingano ya dunia yanahusiana sana na maendeleo ya mwafaka ya China na Afrika, maendeleo ya mwafaka kati ya China na Afrika yataleta mazingira bora kwa ujenzi wa dunia ya kupatana, ushirikiano wa mambo ya kiuchumi ni muhimu katika uendelezaji wa uhusiano mpya wa wenzi wa kimkakati wa China na Afrika, na pia ni msingi wa kuimarisha uhusiano na nchi za Afrika. Kuendeleza uhusiano mpya wa wenzi wa kimkakati kati ya China na Afrika kwa kufanya ushirikiano wa kiuchumi kunahitaji kukukubaliwa na China na nchi za Afrika, ili kuwa na ushirikiano mkubwa kati ya wanaviwanda wa pande zote mbili."

Hivi sasa nchi za Afrika zinaweka mbele kukuza uchumi na kuboresha maisha ya watu, katika hali hiyo ushirikiano wa kiuchumi unafanya kazi kubwa kuimarisha uhusiano wa pande hizo mbili. Katika mchakato wa kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na Afrika, kampuni za China zilizoko barani Afrika zinabeba jukumu muhimu, Rais Hu Jintao alieleza matarajio yake matatu,

"Kwanza ni mkumbuke vizuri jukumu lenu, na kutenda vitendo kwa kuzingatia majukumu yenu muhimu; Pili, kutia mkazo katika kuongeza sifa na ubora wa kazi; Tatu, kuhimiza maendeleo ya mwafaka na kupatana, na kunufaisha umma."

Rais Hu Jintao alisema, kampuni zenye mitaji ya China zilizoko barani Afrika ni sehemu muhimu ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na nchi za Afrika, kitu zinachowakilisha siyo kampuni zao tu, bali zaidi ni taifa la China, watu wa Afrika wataunganisha ubora wa kazi, bidhaa na huduma za kampuni pamoja na nchi ya China. Aliongeza,

"Mnatakiwa kufanya kila kitu kwa kuzingatia maendeleo ya muda mrefu ya ushirikiano kati ya China na Afrika, kubeba majukumu ya jamii ya nchi za Afrika, yakiwa ni pamoja na kuongeza ajira, kuboresha maisha ya watu, na kufundisha watu wengi zaidi."

Wawakilishi wa kampuni hizo walisema, watatoa mchango mkubwa zaidi kwa maendeleo ya ushirikiano wa pande hizo mbili.

Idhaa ya Kiswahili 2007-02-07