Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-02-07 21:19:24    
Kuimarisha mshikamano na ushirikiano na kuhimiza ujenzi wa dunia yenye masikilizano

cri

Rais Hu Jintao wa China anayefanya ziara nchini Afrika ya kusini, tarehe 7 ametoa hotuba kwenye Chuo Kikuu cha Pretoria akifafanua mapendekezo ya China ya kuimarisha urafiki wa vizazi baada ya vizazi kati ya China na Afrika na kuhimiza ujenzi wa dunia yenye masikilizano. Katika hotuba yake, rais Hu Jintao alikumbusha namna wananchi wa China na wa Afrika walivyosaidiana katika mapigano ya ukombozi wa kitaifa, kufanya ushirikiano wa dhati katika njia ya maendeleo na ustawishaji wa nchi, na kuungana mkono katika mambo ya kimataifa. Alisema:

Ingawa China na Afrika ziko mbali sana, lakini urafiki kati ya China na Afrika ulianzia tangu enzi na dahari. Katika miaka mingi iliyopita, wananchi wa China na Afrika wamekuwa na urafiki mkubwa kama chanda na pete, ambapo walikabiliwa na ajali za namna moja na walielewana moyo kwa moyo. Wananchi wa China wanaona majivuno kuwa na urafiki wa dhati wa wananchi wa Afrika. Katika siku zilizopita, wakati wa hivi sasa na siku za mbele, wananchi wa China daima ni marafiki wazuri wanaotendeana kwa dhati na wananchi wa Afrika kwa usawa na uaminifu, ni wenzi wazuri wanaposaidiana na kufanya ushirikiano wa kunufaishana ili kupata maendeleo ya pamoja, vilevile ni ndugu wazuri wanaokabiliana na shida kwa pamoja. Wananchi wa China na waafrika wanapaswa kuwa na urafiki vizazi hadi vizazi, na hakika watadumisha urafiki vizazi hadi vizazi.

Katika hotuba yake rais Hu Jintao amejulisha matokeo yaliyopatikana kwenye mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, na amesisitiza kuwa sera na hatua 8 zilizotangazwa na serikali ya China kwenye mkutano huo kuhusu kuongeza misaada kwa Afrika, kufuta madeni inayozidai nchi za Afrika zenye madeni mazito na nchi za Afrika zilizoko nyuma kabisa kimaendeleo, kufungua soko kwa Afrika na kuimarisha ushirikiano kwenye sekta za uchumi na jamii kati ya China na Afrika, zote hizo ni kwa ajili ya kuzisaidia nchi za Afrika kuongeza uwezo wa kujiendeleza, ili kuleta manufaa zaidi kwa wananchi wa Afrika. Lakini Rais Hu pia hakukwepa matatizo kadhaa yaliyoko kwenye ushirikiano kati ya China na Afrika. Akisema:

Kweli si rahisi kuepusha matatizo mapya katika ushirikiano unaoendelea kwa kasi kati ya China na Afrika. Lakini yakilinganishwa na mambo makuu ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili, matatizo hayo ni matatizo yaliyotokea katika njia ya kusonga mbele, ambayo kabisa yanaweza kutatuliwa baada ya kufanya mashauriano ya kirafiki na kuzidisha ushirikiano. China inatilia maanani sana masuala yanayofuatiliwa kuhusu miundo ya kibiashara isiyo halali sana, na maeneo ya uwekezaji bado si makubwa na kadhalika, na itaendelea kujadiliana na marafiki wa Afrika ili kuchukua hatua za kuyatatua.

Rais Hu Jintao pia amejulisha mafanikio yaliyopatikana nchini China tokea ianze kufanya mageuzi na ufunguaji mlango mwaka 1978. Amesisitiza kuwa maendeleo ya China ni maendeleo ya amani, maendeleo ya kufungua mlango, maendeleo ya ushirikiano na maendeleo ya masikilizano. China inafanya juhudi kujenga jamii yenye masikilizano nchini, na pia China inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali duniani kuhimiza ujenzi wa dunia yenye amani ya kudumu na ustawi wa pamoja.

Rais Hu Jintao pia amewaambia vijana wa Afrika ya kusini kuwa, siku za mbele za Afrika ya kusini itawategemea vijana, na matumaini ya ustawi wa Afrika yanategemea vijana wote wa nchi za Afrika. Vijana wa China na Afrika ni nguvu kubwa ya kudumisha urafiki kati ya China na Afrika.

Idhaa ya Kiswahili 2007-02-07