Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-02-08 15:11:13    
Utamaduni wa China na utamaduni wa Afrika wasonga mbele kwa pamoja

cri

Rais Hu Jintao wa China ambaye yuko ziarani barani Afrika tarehe 7 alitembelea mabaki ya ustaarabu wa Maropeng nchini Afrika Kusini ambayo ni urithi wa utamaduni duniani yaliyorodheshwa na UNESCO, na kutangaza kuwa China itasaidia mfuko wa hifadhi ya urithi wa utamaduni barani Afrika kwa kutoa dola za kimarekani milioni moja, ili kuonesha urafiki wa watu wa Afrika na kuunga mkono hifadhi ya urithi wa utamaduni wa Afrika.

Mabaki ya ustaarabu wa Maropeng yenye eneo la hekta elfu 50 yako kwenye bonde la mlima uliopo upande wa magharibi wa mji wa Johannesburg, ni mabaki ya visukuku vya watu wa kale ndani ya Mapango ya Sterkfontein yenye vivutio zaidi 300.

Mkuu wa jimbo la Gauteng lenye mabaki hayo Bw. Mbhazima Shilowa alifahamisha kwamba neno maropeng lina maana ya chanzo cha binadamu, mwaka 1999 UNESCO iliorodhesha mabaki hayo kwenye orodha ya urithi wa utamaduni duniani. Alisema,

"Mabaki hayo yamethibitisha kuwa Afrika ni chanzo cha binadamu, miaka 12 kabla ya mabaki hayo kuorodheshwa kwenye orodha ya utamaduni duniani, mabaki ya fuvu la "Peking Man" pia yaliorodheshwa kwenye orodha ya urithi wa utamaduni duniani. Mabaki hayo mawili pamoja na mabaki mengine ya ustaarabu nchini China na Afrika Kusini yameimarisha uhusiano wa kiutamaduni na kisayansi kati ya China na Afrika Kusini."

Bw. Shilowa alieleza kuwa hivi sasa ingawa watu wa makabila tofauti wanatofautiana kwa lugha na imani ya dini, lakini wote wana chanzo kimoja na wana historia moja ya kale. Ingawa marafiki wa China mnatoka mbali lakini 'sote ni wa familia moja.' "

Baada ya ziara kwenye mapango hayo alisema visukuku vya wahenga vimethibitisha kuwa Afrika ni sehemu inayolea ustaarabu wa binadamu, na kwa uthabiti imethibitisha kuwa Afrika imetoa mchango mkubwa kwa ajili ya maendeleo ya binadamu. Alisema, ili kuunga mkono hifadhi ya utamaduni wa Afrika na kuonesha urafiki wa China kwa watu wa Afrika Kusini, serikali ya China imeamua kutoa msaada wa dola za kimarekani milionimoja kwa mfuko wa hifadhi ya urithi wa utamaduni wa Afrika. Alisema,

"Tunatumai kuwa wataalamu wa mambo ya kale wa China na Afrika Kusini wataimarisha maingiliano na ushirikiano, ili kufumbua siri za watu wa kale na kutoa mchango mkubwa zaidi. Naamini kuwa ustaarabu wa kale wa China na wa Afrika utaimarishwa na hakika utatoa mchango mkubwa kwa ajili ya amani na maendeleo ya binadamu."

Kwenye sherehe ya kutoa msaada, waziri wa utamaduni wa Afrika Kusini alisema, tokea China na Afrika Kusini zianzishwe uhusiano wa kibalozi tarehe mosi Januari mwaka 1998, ushirikiano wa kunufaisha pande mbili unaendelea vizuri, tunaishukuru China na hasa rais Hu Jintao kwa kuunga mkono sanaa na utamaduni wa Afrika Kusini. Mchango wa China kwa mfuko wa hifadhi ya urithi wa utamaduni wa Afrika kwa mara nyingine umethibitisha kuwa China, nchi iliyo kubwa, imekuwa inatimiza ahadi zake kwa Afrika. Alisema,

"Urithi wa utamaduni, utamaduni na sanaa zimekuwa zikitoa mchango maalumu kwa ajili ya maelewano ya jamii tofauti. Kwa hiyo kuhifadhi mabaki ya Maropeng sio muhimu kwa Afrika Kusini tu bali pia kwa nchi nyingine. Msaada wa fedha kwa ajili ya mfuko wa hifadhi ya urithi wa utamaduni umeonesha kuwa urithi wa utamaduni wa Afrika unaweza kuwaletea baraka binadamu na vizazi vyetu, kwa niaba ya watu wa Afrika Kusini natoa shukrani za dhati kwa msaada huo. Shukrani!"

Mfuko wa hifadhi ya utamaduni wa Afrika ulianzishwa mwaka 2006 ambao uko chini ya UNESCO, kazi yake ni kutoa fedha kwa ajili ya hifadhi ya urithi wa utamaduni kusini mwa Sahara. Imefahamika kuwa kati ya mabaki 65 ya utamaduni wa kale barani Afrika, 43% yamekuwa katika hatari ya kutoweka ambayo hatua za haraka ni lazima zichukuliwe ili kuyahifadhi.

Idhaa ya kiswahili 2007-02-08