Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-02-09 15:06:59    
Rais Hu Jintao wa China aanza ziara yake nchini Msumbiji

cri

Kutokana na mwaliko wa rais Armando Guebuza wa Msumbiji, rais Hu Jintao wa China tarehe 8 aliwasili Maputo, mji mkuu wa Msumbiji na kuanza ziara ya kiserikali nchini humo.

Kabla ya Msumbiji kupata uhuru, China iliunga mkono Msumbiji katika mapambano ya ukombozi. Tarehe 25 Juni mwaka 1975 ni siku ambayo Musumbiji ilipata uhuru, katika siku hiyo China na Msumbiji zilianzisha uhusiano wa kibalozi. Katika muda wa miaka zaidi ya 30 iliyopita, watu wa China na Msumbiji wamejenga urafiki mkubwa. Hii ni ziara ya kwanza kwa rais wa China nchini Msumbiji, ziara yake imepokelewa kwa shangwe kubwa.

Rais Guebuza alimpokea rais Hu Jintao na msafara wake kwenye uwanja wa ndege na kumwandalia sherehe kubwa hapo uwanjani.

Umati wa watu wa Musumbiji waliovaa mavazi rasmi walimkaribisha rais Hu Jintao na msafara wake kwa nyimbo na ngoma uwanjani huku kukiwa na jua kali.

Msumbiji ni moja ya nchi maskini zilizotangazwa na Umoja wa Mataifa. Katika miaka mingi iliyopita China ilijitahidi kwa uwezo wake kuisaidia nchi hiyo jengo la bunge, makazi ya askari, jengo la wizara ya mambo ya nje na jengo la kimataifa la mkutano. Mwanzoni mwaka 2006 China ilikubali kuisaidia nchi hiyo kujenga uwanjwa wa taifa wa michezo.

Rais Hu Jintao alifanya mazungumzo na rais Guebuza. Baada ya mazungumzo marais hao wawili walihudhuria sherehe ya kusaini mikataba minane ya ushirikiano inayohusu uchumi, teknolojia, kilimo, elimu na michezo, na kufanya mkutano na waandishi wa habari. Rais Hu Jintao alisema,

"Lengo la ziara yangu hapa nchini Msumbiji ni kutimiza makubaliano ya mkutano wa wakuu wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika mjini Beijing, kuimarisha urafiki wa jadi kati ya China na Msumbiji, kupanua ushirikiano na kusukuma maendeleo ya pamoja. Hivi punde nilifanya mazungumzo na rais Guebuza, na kuafikiana kuhusu kuimarisha urafiki na ushirikiano. Tumekubaliana kwamba pande mbili zidumishe maingiliano ya ngazi ya juu, kuimarisha kwa kina ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara, kupanua maingiliano ya utamaduni na kuzidi kusawazisha misimamo katika masuala ya kimataifa. Mikataba iliyosainiwa ni uthibitisho wa kuimarisha ushirikiano huo wa pande mbili."

Rais Hu Jintao alitangaza kuwa ili kutimiza mafanikio ya mkutano wa wakuu wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, kusaidia Msambiji kuinua uchumi na kuboresha maisha ya wananchi, China imeamua kuifutia Msumbiji madeni yasiyo na riba, kuongeza aina za bidhaa zinazosamehewa ushuru wa forodha zinazouzwa nchini China, na China itasaidia Msumbiji kujenga kituo cha teknolojia ya kilimo, kuongeza kujenga shule vijijini, kituo cha kinga na tiba ya malaria na kufungua zaidi soko kwa Msumbiji. Rais Hu Jintao alisema,

"Nina uhakika kwamba kutokana na juhudi za pamoja, urafiki na ushirikiano kati ya China na Msumbiji utakuwa mzuri zaidi."

Rais Guebuza alisema,

"Ziara ya rais Hu Jintao ni matokeo ya urafiki wa miaka mingi kati ya nchi hizo mbili, na imeonesha kuwa China inaithamini Msumbiji. Katika miaka iliyopita China ilitusaidia sana katika sekta nyingi. Tulibadilishana maoni kuhusu hali ya kimataifa, na pande mbili zimekubaliana kufanya juhudi zaidi kwa ajili ya amani na usalama duniani, kwani amani na usalama duniani ni mazingira ya lazima kwa ajili ya maendeleo ya jumuiya ya kimataifa na maisha bora ya watu, na sisi pia tunakubaliana kuimarisha uhusiano wa pande mbili. Mikataba iliyosainiwa leo itakuwa ni mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa na kukomesha umaskini nchini Msambiji.

Idhaa ya kiswahili 2007-02-09