Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-02-10 16:43:44    
Ziara ya rais Hu Jintao wa China nchini Shelisheli

cri

Kutokana na mwaliko wa rais James Alex Michel wa Shelisheli, tarehe 9 rais Hu Jintao wa China alifika Victoria, mji mkuu wa Shelisheli na kuanza ziara rasmi nchini humo. Shelisheli ni nchi inayozungukwa na bahari ya Hindi inayoundwa na visiwa 115. Nchi hiyo ina eneo la ardhi la kilomita 455 za mraba na watu zaidi ya elfu 80. Kutokana na raslimali nyingi za utalii na uvuvi, hivi sasa Shelisheli ni nchi tajiri kuliko nyingine barani Afrika, kiasi kwamba pato la taifa kwa wastani wa kila mwananchi limefikia dola elfu 8 za kimarekani.

Hu Jintao ni rais wa kwanza wa China kufanya ziara nchini Shelisheli, yeye pia ni rais wa kwanza mgeni kuizuru nchi hiyo katika miaka karibu 20 iliyopita. Serikali ya Shelisheli na watu wake walimlaki rais wa China kwa ukarimu mkubwa.

Rais James Alix Michel wa Shelisheli alimlaki rais Hu Jintao na msafara wake kwenye uwanja wa ndege, ambapo rais Hu Jintao alikagua gwaride la heshima.

Radio ya Shelisheli ilikuwa ikipiga nyimbo za Kichina zinazojulikana nchini China, hali ambayo inawafanya wageni wa China wahisi ukarimu mkubwa wa wenyeji.

Kwenye uwanja wa ndege, rais Hu Jintao wa China alitoa hotuba ya maandishi akisema, katika miaka 30 iliyopita tangu China na Shelisheli zianzishe uhusiano wa kibalozi, nchi hizi mbili zimekuwa zinaheshimiana na kutendana kwa usawa. Alisema China na Shelisheli zimepata maendeleo makubwa katika ushirikiano wa mambo halisi kati yao, na zimekuwa na mashauriano katika mambo ya kimataifa. Alieleza imani yake kuwa, ziara hiyo hakika itaimarisha urafiki uliopo kati ya China na Shelisheli, kupanua urafiki na ushirikiano kati ya nchi hizi mbili na kuhimiza maendeleo ya pamoja.

Tangu China na Shelisheli zianzishe uhusiano wa kibalozi mwaka 1976, zilisaini mapatano mbalimbali ya ushirikiano katika maeneo ya uchumi, teknolojia na uvuvi. Kati ya mwezi Januari na mwezi Novemba mwaka 2006, thamani ya biashara kati ya nchi hizi mbili ilifikia dola za kimarekani milioni 5.47. Mwandishi wetu wa habari aliyeambatana na rais Hu Jintao kwenye ziara hiyo Bibi Zhang Hui alieleza kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, kampuni za ujenzi za China zilikuwa zinatekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi nchini Shelisheli, wafanyakazi wa China walipata heshima kutoka kwa serikali ya Shelisheli kwa ustadi hodari na moyo wa kuchapa kazi.

Bibi Zhang Hui alisema, "Kampuni za ujenzi za China zinatekeleza miradi ya ujenzi wa shule na majengo ya ofisi. Kwa mfano jengo la ghorofa la idara ya vigezo ya taifa ya Shelisheli lililojengwa na kampuni ya ujenzi ya China, linasifiwa kuwa ni mfano wa kuigwa. Hadi kufikia mwezi Novemba mwaka 2006, kampuni za ujenzi za China kwa ujumla zilisaini mikataba ya kandarasi ya ujenzi yenye thamani ya dola milioni 273 za kimarekani."